Na Mwandishi Wetu Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Doroth Gwajima amewataka wanawake wahakikishe wanatumia huduma za mitandao ili kufikia usawa wa kijinsia kwenye maendeleo kwa kupata taarifa mbalimbali za kijamii kama Afya, Elimu, Kilimo, biashara na zinginezo.
Gwajima ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayofanyika March 8 mwaka huu.
Amesema kuwa pengo la wanawake kumiliki simu na kutumia Mtandao linaongezeka zaidi kwa wanawake wenye umri mkubwa ( wazee) , wanawake wanaoishi vijinini, pamoja na wanawake wenye ulemavu Mwaka 2022 takwimu zinaonesha asilimia 63 ya wanawake duniani walitumia Mtandao ukilinganisha na asilimia 69 ya wanaume.
Aidha amesema kuwa kwa kushirikiana na jamii yenyewe serikali itaendelea kuelimisha na kufanyia kazi kuondoka vikwazo vyote vinavyozuia mwanamke kutumia Teknolojia ya kidigitali.
Pia ametoa wito kwa wanawake na jamii kwa ujumla kujitokeza kuadhimisha sikukuu ya wanawake duniani chini ya uongozi wa waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na ameimiza wanawake kujiunga na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi yaliyo ngazi zote Hadi vijinini Ili kunufaika na uwezeshaji wa serikali na wadau wake.
No comments:
Post a Comment