RAIS DR SAMIA ANA LENGO LA KUIFANYA SEKTA YA AFYA KUWA YA MFANO ZAIDI KISARAWE -DR JAFO
Na Mwandishi Wetu, Kisarawe
WAZIRI wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira (Mb) Jimbo la Kisarawe Mhe Dkt. Selemani Said Jafo amekabidhi vifaa mbalimbali vya afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuboresha huduma za afya katika wilaya hiyo kwa Vijiji 66 Fedha ikiwa ni kutoka kwa Mhe Rais Samia na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika Kutekeleza ilani ya 2020-2025.
Katika makabidhiano ya vifaa hivyo Mhe Dr Jafo amewapongeza watendaji wa Idara ya afya katika hospitali hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuwahudumia wagongwa na pia ameahidi kuwa nao karibu ili kutatua baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika utoaji wa huduma kwa ujenzi wagonjwa.
Aidha wananchi wameishukuru serikali kwa kuwasaidia upatikanaji wa vifaa hivyo kwani vita saidia kupunguza usumbufu wa upatikanaji wa huduma ya matibabu hospitalini hapo
Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita Kwa kupendelea zaidi Kisarawe katika Upatikanaji wa Huduma ya Afya Kwa kuipatia Vifaa Tiba na fedha mbalimbali kwa Ajili ya Afya ambayo inaifanya Halmashauri ya Wilaya Kisarawe kuwa Nzuri katika Huduma za Afya.
No comments:
Post a Comment