Friday, December 30, 2022

DOREFA YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA



DOREFA YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2022

Na Elizaberth Paulo, Dodoma.

VIONGOZI wa michezo na wanamichezo nchini wameaswa kupambania tasnia ya michezo ili iwe na thamani na kupewa kipaumbele kama tasnia zingine ili ichangiae katika ukuaji wa uchumi wa nchini kama nchi zilizowekeza kwenye michezo Duniani. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa michezo Nchini Ally Mayai Tembele wakati akizungumza na wadau wa soka kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Chama Cha Mpira wa Miguu Dodoma(DOREFA).

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuweka wazi mambo yaliyofanywa na kamati tendaji tangu kuingia madarakani pamoja na changamoto zilizowakumba katika utendaji wao.

Mayai amesema kuwa ili tasnia hii ya michezo iendelee kukua ni wajibu wa kila mwanamichezo kuwajibika kwa nafasi yake katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na Umuhimu wa michezo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya zetu hata uchumi wetu hii itasaidia kukua kwa tasnia hii bila kusahau kuwa na nidhamu kwa kila mmoja kumuheshimu mwenzake bila kujali cheo.

“Nawapongeza chama cha soka cha Mkoa wa dodoma kwa kuweza kufanya kazi bila kuwa na tofauti katika utendaji na hii itasaidia soka la Dodoma kuweza kukua kwa kasi kwani maendeleo bora huletwa na viongozi bora,"amesema Mayai

Ameongeza kwa kupongeza mkoa wa Dodoma kwa kuwa na programu ya vijana chini ya miaka 17 kwani itawasaidia vijana kukua kisoka na kuweza kuvumbua vipaji wakiwa bado na umri mdogo.

"Milango ya serikali ipo wazi kwa yeyote mwenye nia njema na tasnia hii na tunawakaribisha wadau wote kuweza kujitokeza kusapoti vipaji vya watoto wetu kwani kila mtu anaelewa mpira ni ajira kwa ajili ya kukuza uchumi na kuondokana na umasikini na kila mtu ameshuhudia namna ambavyo familia nyingi zimejikwamua kiuchumi kupitia michezo,"amesema Mayai.

Aidha ametoa rai kwa wadau wa mpira wa miguu kupambania haki za watoto katika kupata maeneo ya wazi ya watoto hao kufanyia mazoezi ya michezo yao ikiwa ni haki ya msingi ya mtoto na serikali imetoa maeneo ya wazi katika kila mtaa kwaajili ya michezo na shughuli zingine za kijamii.

“Ndugu zangu wanamichezo tuingie mitaaani kwenda kusaka vipaji, tukaelimishe jamii kuhusiana na haki za watoto wetu katika suala zima la michezo alafu kuna maeneo ya wazi ambayo hayatumiki kwa kazi zilizopangwa sasa hili nawaachia fuatilieni maeneo ya wazi kwaajili ya hiyo michezo alafu huko mitaani ndiko kwenye chimbuko la mpira wa miguu na hata historia ya watu wengi maarufu waliofanikiwa kwenye soka historia yao inaonyesha wametokea mitaani,"amesema Mayai

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Dodoma (DOREFA) Mohamed Aden amesema kuwa anawashukuru wadau wa soka jijini hapa kwa kuendelea kutoa maoni na ushauri ili kuhakikisha wanaboresha sekta ya michezo haswa mpira wa miguu jijini Dodoma.

Naye mwakilishi wa wanamichezo Jijini Dodoma amesema sekta ya michezo iko vizuri ila wanaiomba serikali chini ya Waziri wa Michezo Mohamed Mchengerwa kuwatatulia changamoto inayojitokeza ya mara kwa mara ya uwanja wa Jamhuri kufungiwa mara kadhaa kutokana na matumizi mengine ambayo ni tofauti na michezo hivyo kufanya wapenzi wa soka Jijini hapa kukosa burudani ya mpira wa miguu na kutumia viwanja vingine vilivyopo nje ya Dodoma.


Friday, December 23, 2022

RAIS DK SAMIA ATOA VYAKULA VITUO VYA WATOTO

RAIS DK SAMIA ATOA ZAWADI VYAKULA KWA NYUMBA MALEZI YA WATOTO MKOA WA PWANI

Na John Gagarini Kibaha

RAIS wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi vyakula vya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya makundi maalumu ili nao washerehekee kama walivyo watoto wanaoishi na wazazi.

Akimwakilisha Rais kukabidhi katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu cha Makao ya Malezi Madina kilichopo Mtaa wa Vikawe kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kituo hicho kinawakilisha vituo 37 vilivyopo mkoa mzima.

Kunenge alisema kuwa Rais kwa kutambua makundi maalum ametoa zawadi hizo ili watoto hao washeherekee kama watakavyosheherekea wengine ambao wanaishi kwa furaha na familia zao.

"Nimekuja hapa kumwakilisha Rais wetu  amewaletea zawadi pamoja na salamu za sikukuu ya Christmas na mwisho wa mwaka ambapo amewaletea mbuzi wawili, mchele kilo 60, maharage kilo 40, mafuta lita 20, juisi na viungo mbalimbali,"alisema Kunenge.

Alisema kuwa wadau wa maendeleo na wenye uwezo kujenga tabia ya kujitolea kwa vituo vya watoto wenye mahitaji ambapo vitu vilivyotolewa ni pamoja na vitoweo ,mchele , maharage,mafuta ya kupikia ,vinywaji na viungo vingine mbalimbali vya kupikia.

Kwa upande wao watoto wa Makao ya Madina Zainab Athuman na Jumanne Manzi walimshukuru Mungu kwa kumwezesha Rais kupata na kuweza kuwapa zawadi hizo.

Naye Mlezi wa watoto Makao Malezi ya Madina Fatma Abdilai alisema kuwa wananchi waendelee kumuombea Rais Samia kwa mengi anayofanya nchini na kutekeleza ilani kwa kutambua makundi maalum.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka alimshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Samia kwa kuitendea haki ilani ya Chama na kujali watoto .

Mkoa huo una jumla ya makao ya malezi 37 yenye jumla ya watoto 1,301 na kituo hicho cha Madina kina watoto 30.


Mwisho

Saturday, December 10, 2022

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUWA WANYENYEKEVU

 


UNYENYEKEVU KWA WAJASIRIAMALI NI MSINGI WA BIASHARA-MAVUNDE

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri  wa Kilimo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini amewaasa wajasirimali wadogo wadogo kujifunza unyenyekevu pindi wanapokuwa katika shughuli zao. 

Mavunde ameyasema hayo katika ziara aliyoifanya pamoja na wajasirimali (Mama Lishe ) Mkoani Dodoma walipotembelea katika mashamba ya Waziri Mkuu Mstaafu Peter Pinda na kuishukuru  familia hiyo kwa ukarimu wao. 

Ziara hiyo ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika na ambapo Naibu Waziri Mavunde aliitumia siku hiyo kwa kusaidia kuwaongezea mama lishe ujuzi katika ujasiriamali wao.

"Lipo jambo la kujifunza kwa sisi viongozi na kwenu nyie mliofika hapa tujifunze unyenyekevu jamani ukiagalia Waziri Mkuu Mstaafu Pinda kwa nafasi alizozishika lakini leo amekubali nimekuja na mama lishe na akakubali kututembeza shamba lote kwahiyo hapa ndipo tunajifunza Unyenyekevu,"alisema Mavunde.

Alisema kuwa ukiwa kiongozi ukiona watu hawaji kwako hata kuomba maji  ujue unashida kwani kiongozi maana yake ni kupokea watu hivyo Pinda na familia yake wana mioyo ya kipekee na ukarimu mkubwa sana. 

Aidha Mavunde ametumia ziara Hiyo kutangaza January kufanyika kongamano kubwa la siku ya MWANAMKE DODOMA JIJI ili kutathimi makubaliano ya mwaka mzima yalipofikia.

" Mimi nimejiitolea  kulilea  hili kundi ili nione mafanikio yao kila mmoja kwa nafasi yake nataka nione wanapiga hatua kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine Serikali ya  CCM chini ya uongozi wa Rais Dk Samia imefanya kazi kubwa ya kuendeleza Dodoma inakuwa makao makuu  fursa zipo nyingi nataka nione akina mama  wa Dodoma wakichangamkia hizi fursa,"alisema Mavunde.

 "Siyafanyi haya ili mnichague kuwa mbunge wenu, Sifanyi siasa nafanya haya kwasababu niliomba dhamana ya kuwa kiongozi nina wajibu wa kuwasaidia watu wangu,"alisema Mavunde. 

Naye Waziri mkuu Mstaafu Mizengo Peter Pinda amewasihi kushirikiana kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani kwani kila mtu mmoja akipanda mti itakua na mwonekano mzuri hiyo hudhihirishwa baada ya mvua kunyesha Dodoma inakuwa na muonekano mzuri.

Pinda alisema kuwa washirikiane katika kupanda miti ili kuifanya Dodoma ipendeze kwani mji ukiwa na kijani kingi ni mji unaovutia sana na kitu kingine yeye huwa anapenda kusema mjasiri wa mali na siyo mjasiriamali kwani ukishakua mjasiri wa mali utakuwa mbali kimaendeleo.

Alimwomba Mavunde amshirikishe kwenye hilo kongamano litakalofanyika Januari ili aweze kuhamasisha washiriki hao kupanda miti.
 
Nao baadhi ya wajasirimali waliozungumza kwa nyakati tofauti wametoa shukrani zao kwa Mavunde kwani hakuna mbunge aliyeifanya tukio kama hilo kwa kuwakutanisha na kuwapeleka katika mashamba ya Pinda kwani wamejifunza vitu vingi na kuahidi kwenda kufanyia kazi.

Mwisho. 

Monday, December 5, 2022

MIPANGO YAANDAA WATAALAMU


WAHITIMU WAANDALIWA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI.

Na Wellu Mtaki, Dodoma

CHUO cha Mipango na Maendeleo Vijijini kimejikita katika utoaji wa Elimu na vitendo katika kuhakikisha wanatoa wahitimu ambao watakaokwenda kujiajiri wenyewe na kuajiriwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi Jenifa Omolo akiwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Lameck Nchemba katika mahafali ya 36 ya chuo hiki cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Bi Omolo amesema kuwa kutokana na Mafunzo yanayotokana katika chuo hiko Wahitimu Watatumia ujuzi huo waliopata katika Kujiajiri wenyewe na kwenda Kuisaidia jamii.

Aliwataka wahitimu na wale wanafunzi watakaoendelea na mafunzo kwa ngazi ya juu kuwa na chachu ya kuendelea kujifunza ili kuongeza maarifa,ujuzi na ubunifu unaohitajika katika kuboresha utendaji wao wa kazi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Mipango Vijijini Prof. Hozen Mayaya ameeleza mafanikio waliyoyapata kwa mwaka 2021/2022 katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Mabweni na Kumbi za mihadhara kwa kutumia fedha za vyanzo vya ndani ya chuo na Ruzuku kutoka Serikalini na kueleza matarajio yao ya 2022/2023 ya kujenga Maktaba kubwa na ya kisasa pamoja na bweni la wanafunzi katika eneo la Kisesa Jijini Mwanza.

Akisoma hotuba kwa niaba ya wanafunzi wenzake muhitimu Gift Kyando ameishukuru Serikali na Wizara ya Fedha na Mipango ambayo ni Wizara Mama ya chuo chao na kuomba Chuo kuendelea kuwasaidia ili waweze kusonga mbele zaidi hasa wanapohitaji kupata Barua za uthibitisho kutoka Chuoni .

Mahafali ya 36 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ya mwaka 2022 yana jumlaya wanafunzi 6,225 waliohitimu wakiwemo wanaume 2,722 na wanawake 3,502 katika fani mbalimbali za Maendeleo vijijini.

Mwisho.

Wednesday, November 30, 2022

WAWEKA MIKAKATI KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA

WADAU WAENDELEA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA WILAYA YA KIBAHA



 IMEELEZWA kuwa uanzishwaji wa madawati kwenye shule na makundi mbalimbali ya jamii kutasaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa matukio yanayohusiana na vitendo hivyo.


Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na mwanasheria wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) Tanzania Zakia Msangi wakati wa kupita msafara unaotoa elimu ya kupambana ukatili wa Kijinsia ikiwa ni sehemu ya siku 16 za kupinga vitendo hivyo.

Alisema kuwa moja ya makundi yanayoathirika na vitendo hivyo ni watoto ambapo madawati hayo yataundwa kwa kushirikiana na walimu wa malezi kwenye shule.

"Madawati haya yatakuwa yakitoa elimu juu ya kupambana na ukatili wa Kijinsia na kuripoti vitendo hivyo kwenye vyombo husika ikiwemo dawati la jinsia na vyombo vingine vya sheria,"alisema Msangi.

Msangi alisema kwa shule kutakuwa na wanafunzi wawili vinara ambao watakuwa na ujasiri wa kujieleza na wenye usiri pia kutakuwa na sanduku la siri la kutolea maoni.

"Makundi mengine ndani ya jamii kama vile waendesha pikipiki nao wataunda madawati kwa ajili ya kupambana na matukio hayo ambapo itasaidia kukabili kwani ni kundi linalokumbana na mambo mengi,"alisema Msangi.

Aidha alisema kuwa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) Tanzania ni waratibu wa kampeni hiyo ambapo wameungana na Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) ambao ndani yake kuna mashirika zaidi ya 100 kupambana na suala hilo.

Kwa upande wake ofisa Mawasiliano wa Shirika linalosaidia mashirika yanayotoa msaada wa sheria (LSF) Wilson Mtapa alisema kuwa wamewezesha msafara huo ili kupinga vitendo hivyo kwa kutoa elimu ya kupinga vitendo hivyo kwa kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo.

Mtapa alisema kuwa elimu hiyo inatolewa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na mashuleni madokoni na kwa vikundi vya waendesha bodaboda kwenye Wilaya msafara huo utakapopita kauli mbiu ikiwa ni Kila uhai unathamani tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Alisema kuwa mashirika hayo mbali ya kupambana na vitendo hivyo pia yanatetea haki za binadamu ambapo wanatoa elimu ya namna ya kukabiliana na vitendo hivyo ndani ya jamii na msafara huo ulioanzia Dar es Salaam Pwani utapita mikoa ya Morogoro, Singida, Shinyanga, Arusha na Musoma.

Naye mwakilishi wa Shirika la Maendeleo kwa Vijana YPC ambalo liko chini ya MKUKI ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa msafara huo Fred Mtei alisema kuwa ujumbe uliotolewa wa kukabiliana na vitendo vya ukatili umewafikia watu wengi.

Mtei alisema kuwa wao kama wana harakati wataendelea kutoa elimu na kuielimisha jamii namna ya kukabiliana na vitendo hivyo.

Mkurugenzi wa Kituo Cha Msaada wa Kisheria Kibaha (KPC) Catherine Mlenga alisema kuwa wamekuwa wakipokea wateja ambao wengi wao ni wa vitendo vya ukatili wa Kijinsia.

Mlenga alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na vyombo vya sheria ikiwemo Polisi na mahakama kupambana na vitendo hivyo kwenye Wilaya na Mkoa mzima wa Pwani na wanatoa elimu kwenye maeneo mbalimbali na makundi ya kijamii.

 Kwa upande wake Mratibu wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Tanzania kwa Mkoa wa Pwani Honorina Kambadu alisema kuwa wanazingatia haki na usawa mbele ya sheria na kukabili matukio ya ukatili wa Kijinsia.

Kambadu alisema kuwa baadhi ya matukio ni kama vile vipigo, unynyasaji na mauaji na kunyimwa haki zingine kwa wanawake na watoto ambao ndiyo waathirika wakuu wa vitendo hivyo.

Mwisho.

Tuesday, November 29, 2022

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASEMA VIJANA WANAAJIRIKA


Na John Gagarini, Mkuranga

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa nchi inauwezo wa kuzingatia Utumishi kwenye sekta binafsi ili wawekezaji watumie vijana wa hapa nchini na kuachana na mawazo ya kuleta wafanyakazi kutoka nje ya nchi kwani Watanzania wanaajirika na ni waaminifu.

Majaliwa aliyasema hayo Kisemvule Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani alipokuwa anazindua kiwanda na mabati cha Lodhia Group of Company na kusema kuwa vijana wa Kitanzania wanauwezo wa kufanya kazi na hakuna sababu ya wafanyakazi kutoka nje ya Tanzania.

Alisema kuwa vijana wa Kitanzania wanaajirika na wanafanya kazi kwa bidii na kwa sasa hata vitendo vya kutopenda kufanya kazi hilo halipo tena wanawajibika ipasavyo. 

"Waajiriwa zaidi ya 3,000 kitendo cha kutoa ajira umesaidia sana tutakuunga mkono uendelee kutoa vijana ambao wako mtaani itasaidia kufanya nchi kuwa na amani nchi imepanua wigo na fursa za uwepo wa viwanda,"alisema Majaliwa.

Aidha alisema uwepo wa kiwanda hicho umesaidia kutoa ajira na hiyo ni fursa kwa wengine inasaidia kuzalisha na kupanua wigo ili kusaidia watu wengine zaidi hapa ni ajira zaidi ya 2,500 hilo ni jambo kubwa.

"Serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kuja kuwekeza kwa wale wa ndani na nje maelekezo tuliyopewa kuanzia kuomba kuwekeza na kuanza uwekezaji ni kuhakikisha hawapati shida wala kikwazo chochote ili kila upande unufaike mwekezaji na mwananchi,"alisema Majaliwa. 

Aliongeza kuwa kampuni hiyo ni moja ya kampuni inayolipa kodi kubwa nchini ambapo inalipa zaidi ya bilioni 40 kwa mwezi ni kama lulu watatatua changamoto zinazoikabili kwani nachangia pato la serikali na kusaidia huduma za jamii na inamuunga mkono Rais kwa kupunguza changamoto ya ajira.

"Hapa Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji tunatambua na tunaheshimu uwekezaji huu kwani huyu ni wa kuenziwa na Halmashauri ili wapate fedha zaidi na hatimaye nchi inufaike hakika leo nimefurahi sana kutembelea kiwanda hichi ambapo Arusha nlitembelea walikuwa na kiwanda kidogo sana uwekezaji mkubwa na malengo kuweka mradi mkubwa zaidi naifurahi kutembelea,"alisema Majaliwa.

Alibainisha kuwa kiwanda hicho kinachozalishwa chuma mbalimbali zikiwemo nondo ni kikubwa kuliko viwanda vyote alivyotembelea na kuweka jiwe la msingi la kiwanda ukubwa wake ni hekari nane na nusu kitatengeneza bati.

"Uwepo wa viwanda vya nondo, plastiki, mabomba ya maji na bati itasaidia bidhaa kwani zitapatikana hapa nchini badala ya kuagiza nje na pia zina ubora bado eneo dogo kufikia kiwanda cha Afrika Mashariki itafikia hatua hiyo na kuwa kiwanda kikubwa hapa Afrika Mashariki,"alisema Majaliwa.

Aliongeza kuwa uwepo wa viwanda vijana Teknolojia na hilo limepewa kipaumbele ili wajifunze kupitia mitambo hiyo ya kisasa ni faida ya uwepo wa viwanda nchi itakuunga mkono na milango itakuwa wazi na azma ya kutembelea ni kuangalia uwekezaji unaofanywa ukiwemo kwenye mabomba ya maji na serikali inaona kuwa anafunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan alisema na kuwahakikshia kuwa uwekezaji hautakwama hata kidogo.

Kwa upande wake Mwenyekiti na mwanzilishi wa kampuni hiyo Haroun Lodhia alisema kuwa kiwanda chao kinalipa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 22 kwa ajili ya umeme na gesi ambapo baadaye watakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 40,000 za chuma kwa mwezi.

Lodhia alisema kuwa kwa siku za baadaye watazalisha umeme wao wenyewe ambapo wataanza kuzalisha megawati tano na baadaye kva 25 na wanaishukuru serikali kwa kuwawekea mazingira mazuri kuendesha shughuli zao.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdala Ulega alisema kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliopo kwenye Wilaya ya Mkuranga na wingi wa magari yanayokwenda mikoa ya Kusini wangeomba barabara ya Kusini ipanuliwe na kuwa ya barabara nne.

Ulega alisema kuwa barabara hiyo kuanzia Mbagala Rangitatu kwenda Mwandege Vikindu na kuendelea ingepanuliwa ili bidhaa ziweze kwenda kwa urahisi na pia hapo Mkuranga viwanda vingi tumia umeme mkubwa na hakuna gari la Zimamoto ikitokea moto itakuwa ni shida sana hivyo wapatiwe huduma ya gari hilo.

Mwisho.


Friday, November 25, 2022

CHANJO COVID-19


VIJANA WAJITOKEZE KUCHANJA COVID-19

VIJANA nchini wametakiwa kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa COVID 19 na waachane na dhana potofu kuwa hawawezi kuambukizwa ugonjwa huo.

Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Mtaalam wa chanjo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Caroline Akim alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na chanjo ya COVID 19. 

Akim alisema kuwa moja ya kundi kwenye jamii ambalo halijitokezi kuchanja wakidhani kuwa hawawezi kupatwa na ugonjwa huo hivyo kuwa hatarini kuambukizwa ugonjwa huo.

"Vijana wanadhana kuwa hawawezi kupata ugonjwa huo kwani baadhi hawana dalili ya maambukizi licha ya kuwa wao ndiyo wenye pilika pilika nyingi,"alisema Akim.

Alisema kuwa vijana ni kundi ambalo linahimizwa kupata chanjo kutokana na kuwa na mizunguko mingi kwenye jamii na kuwa rahisi zaidi kueneza ugonjwa huo pale wanapoupata.

"Wajawazito pia wanahimizwa kupata chanjo ya COVID-19 kwani wakipata ugonjwa huu wako kwenye hatari ya mimba kutoka au mtoto kuzaliwa kabla ya wakati na hata wanaonyonyesha wanakumbushwa kuwa chanjo ni salama kwao haina madhara kwa mtoto" alisema.

Aidha alisema kuwa waandishi wanatakiwa  sasa kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kuchanja lakini pia faida zake ili kuepuka kuingia kwenye athari wanapopata ugonjwa huo.

Naye Mratibu wa chanjo mkoa wa Pwani Abas Hincha alisema kuwa wanatarajia kuanza kampeni ya chanjo ya COVID-19 inaanza Novemba 25 na watawafikia wananchi ambao bado hawajapata chanjo.

Hincha alisema kuwa Mkoa huo unatarajia hadi kufikia Desemba 30 kuwafikia wananchi 757,465 na kwamba hadi kufikia Novemba 22 walengwa 468,187 tayari wamepata chanjo sawa na asilimia 63.

Saturday, November 19, 2022

SAMIA AASA VIONGOZI WA DINI JUU YA AMANI



Wellu Mtaki, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaasa viongozi wa dini hapa nchini kuendelea kushikamana na serikali kudumisha uzalendo na amani ya nchi .

Amebainisha hayo leo Novemba 19.2022 Jijini Dodoma katika sherehe ya Jubilee ya miaka 50 ya Kanisa la Waadventista Wasabato Jiji la Dodoma ambapo amesema amani ndiyo msingi wa utulivu wa nchi.

Ametumia fursa hiyo kulipongeza Kanisa la Waadventista Wasabato kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha amani na kuendelea kushirikiana na serikali kwa miradi mbalimbali ya huduma za kijamii ikiwemo katika sekta za afya,elimu na kusaidia wenye uhitaji.

Aidha amekipongeza kikundi cha uimbaji cha watoto wa shule ya Msingi na awali cha Ellen White pamoja na Kwaya ya Nyarugusu SDA kutoka mkoani Geita kwa kuimba wimbo wenye uzalendo na upendo wa taifa la Tanzania.

Kuhusu suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii Rais Samia amewaasa viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na serikali kukemea vitendo viovu ikiwemo kushirikiana katika mapambano ya dawa za kulevya na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Amesema suala la mabadiliko ya nchi ya ukosefu wa mvua katika baadhi ya maeneo amewaasa viongozi wa dini na washarika kwa ujumla kuliombea Taifa huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kuwa mabalozi kuelimisha jamii kuhusu madhara ya uharibifu wa mazingira.

Hata hivyo Rais Samia amehitimisha kwa kusema kuwa ni muhimu sana kutegemea neema na Baraka za mwenyezi Mungu kama isemavyo Zaburi 127:1.

Naye Mwenyekiti Kanisa la Waadventista Wasabato Union ya Kusini mwa Tanzania [STU] Mch.Dkt.Godwin Lekundayo amemhakikishia Rais Samia kuwa Kanisa litaendelea kushirikiana na serikali katika kuwajengea maadili vijana .

Mch.Lekundayo ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa serikali ya Tanzania kwa ajali ya ndege ya Precision Air iliyoua watu 19 hivi karibuni mkoani Kagera huku akisisitiza kuwa kanisa litaendelea kuiombea Tanzania kuepusha majanga.

Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kusini mwa Tanzania[STU] Mch.Jeremiah Izungo amesema wao kama kanisa wataendelea kushirikiana na serikali kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo katika sekta za elimu na afya.

Mch Izungo amesema kanisa linaendelea kusisitiza afya ya jamii ikiwemo kuzingatia kanuni bora za afya,lishe na kuchangia damu salama ambapo huwa kuna utaratibu wa kuchangia damu salama kila mwaka mwezi Machi.

Amesema changamoto zinazolikabili Kanisa ni pamoja na usaili wa nafasi za kazi serikalini siku ya Jumamosi ya ibaada ambapo hukosesha vijana nafasi za ajira serikalini pamoja na mitihani shuleni kufanyika siku ya Jumamosi ya ibaada.

Ameiomba serikali kuwapatia wataalam wabobezi katika hospitali za Kanisa huku akiweka msisitizo kuwa Kanisa linajitegemea haliko kwenye muunganiko wa wa Umoja wa Kikristo Tanzania [CCT].


Wednesday, November 16, 2022

WALIMU WAKUU KUPATIWA MAFUNZO NA ADEM


ADEM KUTOA MAFUNZO YA UONGOZI

Na Wellu Mtaki, Dodoma

WAKALA wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) imesema imejipanga kutoa Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Shule kwa Walimu Wakuu 17,000.

Aidha itatoa mafunzo ya utawala Bora kwa wasimamizi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt Siston Masanja akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wakala hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/2023.

Dkt Masanja amesema katika mwaka huu wa fedha wa 2022/2023 wakala hiyo imejipanga kudahili Walimu 2,343 katika kozi mbalimbali pamoja na kuandaa kitabu cha kiongozi cha Mwalimu Mkuu na kuandaa Mwongozo wa Utawala Bora kwa viongozi wa Serikali za Mitaa.

Dkt.Masanja amesema moja kati ya malengo ya Wakala hiyo ni kuimarisha usimamizi wa utoaji wa elimu bora shuleni kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na miongozo ya elimu, kuziba ombwe la maarifa na ujuzi ambalo kiongozi au mtendaji hakupata katika mafunzo ya awali ya Ualimu na kuongeza idadi ya viongozi wenye maarifa ya uongozi na usimamizi wa elimu.

Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema kuwa Serikali imeweka fedha nyingi kwenye sekta ya elimu nchini ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/23 sekta ya elimu pekee imetengewa Shilingi trilioni 5.8.

Aidha, Msigwa ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuwaruhusu viongozi wa taasisi za elimu pamoja na wakuu wa shule kwenda kusoma ADEM.

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu - ADEM ulianzishwa Agosti 31, 2001 ukiwa na majukumu ya kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu kwa viongozi na watendaji mbalimbali wa elimu katika ngazi zote na kutoa ushauri wa kitaalamu katika mambo yanayohusu uongozi na usimamizi wa elimu.

Mwisho. 

Friday, November 11, 2022

MABILIONI YATOLEWA KUBORESHA AFYA

SERIKALI YATOA BILIONI 200 UNUNUZI VIFAA TIBA NA DAWA

Na Wellu Mtaki, Dodoma

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Aidha tayari bilioni 74.3 zimetolewa katika kumaliza changamoto ya upungufu wa dawa na vifaa tiba nchini.

Dkt. Mollel amesema hayo leoJijini Dodoma Novemba 11,2022 wakati akijibu swali la Mhe. Ghati Zephania Chomete, Mbunge wa viti maalumu katika kikao cha kumi cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Amesema, Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kutatua changamoto za huduma za afya kwa wananchi, huku kiasi cha shilingi Bilioni 74.3 zikiwa tayari zimetolewa kati ya Bilioni 200 zilizotengwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya ununuzi wa dawa pamoja na vifaa tiba.

"Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga bajeti ya shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba na hadi kufikia tarehe 30 Oktoba, 2022 Serikali imekwisha toa jumla ya shilingi bilioni 74.3 kwa ajili ya manunuzi ya dawa na vifaa tiba ili kuimarisha upatikanaji wake katika ngazi zote za utoaji wa huduma za Afya,"amesema Dkt. Mollel. 

Amesisitiza kuwa, Serikali itaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya nchini kwa kuboresha miundombinu ikiwemo kuweka vifaa tiba vya kisasa, kuajiri Wataalamu wa Afya pamoja na kuwapandisha madaraja ili kuongeza morali ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Akijibu swali la nyongeza Dkt. Mollel amesema, Serikali imepeleka vifaa vyenye thamani ya shilingi Bilioni 3 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara - Kwangwa vitavyosaidia kutatua changamoto ya wananchi kwenda mikoa ya mbali kutafuta huduma hizo.

Ameendelea kusema kuwa, ifikapo Desemba 12, 2022 hospitali hiyo itaanza kutoa huduma zote, huku akisisitiza tayari CT-SCAN imeshafungwa na MRI ikisubiri chumba kikamilike ili huduma hiyo nayo ianze kuwanufaisha wananchi wa Mkoa wa Mara na nchi za jirani.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, Serikali imejipanga katika udhibiti wa dawa kwa kutengeneza mfumo mzuri kutoka zinapotoka ngazi ya taifa mpaka zinapofika katika kituo husika, huku akisisitiza ushirikiano baina ya viongozi, kamati za afya na wananchi katika kusimamia dawa ili ziweze kuwafikia walengwa. 

Pia, ameelekeza hospitali kutumia mapato ya ndani kutatua changamoto za dawa endapo zitajitokeza ili kutatua changamoto hizo kwa wagonjwa wanaoenda kupata huduma katika maeneo hayo ya kutolea huduma. 

MTUMISHI KUKATWA MSHAHARA


BARAZA LA MADIWANI LATOA ADHABU KWA MTUMISHI WA HALMASHAURI KUKATWA MSHAHARA.

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha limemchukulia hatua Mhandisi wake Brighton Kishoa kwa kumkata asilimia 15 ya mshahara kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kushindwa kusimamia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi.

Akitoa maazimio ya kikao hicho cha baraza la madiwani cha robo mwaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Musa Ndomba alisema kuwa mtumishi huyo alisababisha mradi huo kuwa na gharama kubwa.

Ndomba alisema kuwa moja ajenda iliyojadiliwa na baraza hilo ni makosa ya kinidhamu ya kiutumishi yaliyofanywa na Mhandisi huyo wa Halmashauri hiyo ambaye hakufuata utaratibu wa manunuzi (BOQ) ya ujenzi wa nyumba hiyo.

"Kutokana na kutofuata taratibu za manunuzi kulitokea changamoto kwenye ununuzi wa vifaa kwani haukufuata bajeti iliyopangwa hivyo gharama za ujenzi kuwa kubwa,"alisema Ndomba.

Alisema baada ya changamoto hiyo kutokea ilibainika kuwa katika usimamizi wa miradi ilionekana kuna maeneo kafanya uzembe hivyo baraza la madiwani na kamati ya fedha ziliamua kumchukulia hatua za kinidhamu.

"Taratibu zote zimefuatwa kwa kamati za uchunguzi na kufanya kazi yake na zikapendekeza adhabu hiyo na hilo litakuwa fundisho kwa watumishi wengine kwa kutakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazowaongoza," alisema Ndomba.

Aidha alisema kuwa anawakata watumishi wote kuanzia Halmashauri hadi kwenye Mtaa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na wasipingane na miongozo ya kazi zao kwani miradi ya maendeleo itakuwa haina tija na kurudisha nyuma utoaji huduma kwa wananchi.

"Sisi kama baraza hatutarudi nyuma kwani tutachukua hatua kali kadiri inavyowezekana kwa mtumishi yoyote atakayeonyesha utovu wa nidhamu katika utendaji kazi wake na tutatoa adhabu kali zaidi kwa mtumishi atakayekwenda kinyume na taratibu za kazi yake na kuzorotesha utoaji huduma kwa makusudi,"alisema Ndomba.

Alibainisha kuwa hawapendi kutumia muda mwingi kujadili mtu bali wanapenda muda mwingi wautumie kujadili masuala ya kuwaletea maendeleo wananchi.


RC MADARASA YAKAMILIKE


MKUU WA MKOA ATAKA MADARASA YAKAMILIKE NOVEMBA 20

Na Wellu Mtaki, Dodoma

MKUU wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wakuu wa shule zote waliokabidhiwa fedha za ujenzi wa madarasa katika mkoa wa Dodoma kukamilisha miradi hiyo ifikapo Novemba 20 mwaka huu.

Senyamule ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya shule kuona muendelezo wa hatua zilizofikiwa katika shule hizo huku akifafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fedha kwa ajili ya kuwawezesha watoto wanaokwenda kidato cha kwanza mwaka 2023 wasikose madarasa ya kusomea.

Amesema kuwa mkoa wa Dodoma ulipata shilling billion 6.7 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 339 ambapo fedha hizo zimegawanywa katika shule mbalimbali mkoani hapo.

Aidha amewataka walimu wa Shule ya Sekondari Zuzu kuongeza juhudi ya ufundishaji katika shule hiyo ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Zuzu Hezron Lupondo amesema kuwa shule yake ilipata shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa na ofisi huku akimuhakikishia Mkuu wa mkoa wa Dodoma kuwa watafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo pamoja na kuongeza ufaulu katika shule hiyo.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Mnadani Claudian Kabuyombo amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuendelea kuimarisha sekta ya elimu.

BODI YA WAHANDISI YASEMA MIRADI YA KIMKAKATI IMEWAONGEZEA UJUZI

Na Wellu Mtaki, Dodoma

BODI ya Wahandisi Nchini (ERB) imesema kuwa uwepo wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa hapa nchini imekuwa na manufaa kwa Wahandisi wazawa hasa vijana kupata ujuzi na teknolojia mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma wakati akielezea shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 Msajili wa Bodi hiyo Mhandisi Bernard Kavishe amesema kuwa miradi hiyo imekuja na teknojia mpya kabisa.

Mhandisi Kavishe amesema kuwa kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya Wahandisi 33,773 kati yao 26,000 wapo katika soko la ajiri huku wenye leseni za Uhandisi wakiwa ni 10,000 na wengi wao wanashiriki kwa namna moja au nyingine katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa inayoendelea.

Amesema kuwa malengo ya Bodi hiyo ni kuongeza ushiriki wa bidhaa za ndani (Local content) katika miradi yote inayoendelea hapa nchini ambapo matarajio makubwa ya Bodi hiyo ni kujenga kituo Cha Umahiri Jijini Dodoma.

Aidha amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa Vijana wengi wenye mawazo ya kibunifu ila wanakosa namna ya kuendeleza mpaka kufika sokoni hivyo kituo hicho kitakuwa eneo sahihi la kuendeleza mawazo hayo.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema kuwa kwa sasa nchi ina miradi mingi hivyo Bodi ya Wahandisi ina nafasi kubwa katika kutoa ushauri wa namna nzuri ya kutekeleza miradi hiyo kwa uhakika.




Thursday, November 10, 2022

PSSSF YAPATA FAIDA KUBWA


PSSSF YAPATA FAIDA YA MABILIONI.

Na Wellu Mtaki, Dodoma

KWA mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022 mfuko wa PSSSF umepata faida ya uwekezaji kiasi cha shilingi bilioni 581.7.

Hayo yameelezwa na CPA Hosea Kashimba Mkurugenzi mkuu Psssf wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya mfuko huo.

Kashimba amesema kutokana na uwekezaji huu,mfuko hupata faida ya uwekezaji ( return on investment) wastani wa asilimia 8 kwa mwaka,ambayo ni juu ya mfumuko wa bei na hivyo kufanya uwekezaji huu kuwa na tija.

Amesema kuwa mfuko wa Psssf ni mmoja ya waendelezaji milki (real estate developers) wakubwa nchini,mfuko unamiliki majengo ya kupangisha katika miji mbalimbali ambayo hutumika kwa shughuli za kibiashara asilimia 72,ofisi na makazi asilimia 98.

Aidha amesema kuwa wakati wa kuunganisha mifuko psssf ilirithi madeni ya serikali yaliyohakikiwa yenye thamani ya Tsh 731.40 bilioni,mpaka sasa kiasi cha Tsh 500 bilioni kimelipwa na serikali.

“Nirudie kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutambua deni la michango kabla ya 1999 maarufu kama (pre 99 liability) ambalo ni shilingi trilioni 4.6 kwa kutoa hati fungani maalum zenye thamani ya shilingi trilioni 2.1 haya yote yanaleta matumaini ya kuwa na mfuko wenye ustahimilivu na endelevu kwa ustawi wa wanachama,”amesema Kashimba.

Alibainisha kuwa wakati wa kuunganisha mifuko,kiasi kilichokuwa kinalipwa kama pensheni kwa mwezi kwa wastaafu kilikuwa shilingi bilioni 34 lakini mpaka kufikia sasa wastani wa kiasi cha shilingi bilioni 60 kinalipwa bila kukosa kwa wastaafu zaidi ya 150,000 kila ifikapo tarehe 25 kila mwezi.

"Mfuko umewekeza shilingi trilioni 4.5 katika hatifungani za serikali,pamoja na kuleta faida ya uwekezaji kwa mfuko kupitia riba na uwekezaji huu unauwezesha mfuko kutekeleza majukumu yake ya msingi,"amesema Kashimba.

Amesema vilevile mfuko umewekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika soko la hisa la DSM kupitia makampuni mbalimbali yaliyoorodheshwa,uwekezaji huu mkubwa wa mfuko unasaidia kukuza soko la mitaji nchini na kuchochea uchumi na maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja.

“Zaidi ya bilioni 400 zimewekezwa katika amana za muda (fixed deposit) katika benki mbalimbali hapa nchini,uwekezaji huu pia kwa mabenki kutoa mikopo mbalimbali kwa Watanzania na hivyo kuharakisha azma ya serikali kukuza uchumi na kuinua,”amesema Kashimba.

Kwa upande wake Msemaji mkuu wa serikali Ndg.Gerson Msigwa amewapongeza Psssf kwa taarifa za kukua kwa mfuko kwa asilimia 8 na kusema ni jambo zuri na inaonyesha jinsi gani mfuko umeweka mazingira mazuri kwa wanachama.

Msigwa amesema kuwa amepata nafasi ya kutembelea ofisi za Psssf na ameridhishwa na namna ambavyo mfuko unafanya kazi zake na kuimarisha huduma kwa wafanyakazi,pia wafanyakazi ni muhimu kufuatilia michango yao inapowasilishwa na kujiridhishwa.


Wednesday, November 9, 2022

RC ASHIRIKI MSIBA WA MTUMISHI MDH ALIYEFARIKI AJALI YA NDEGE


MKUU WA MKOA WA DODOMA MAZISHI MTUMISHI MDH ALIYEFARIKI AJALI YA NDEGE.

Na Wellu Mtaki, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameshiriki ibada ya mazishi ya Marehemu Neema Samwel aliyefariki kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air Mkoani Kagera ambapo mazishi hayo yaliofanyika nyumbani kwao Ilazo Jijini Dodoma.

Marehemu Neema alikuwa anafanya kazi shirika  (Management and Development for Health) (MDH) ambapo alikuwa anaelekea kwenye ziara ya kikazi mkoani Kagera na kukutwa na umauti.

Senyamule  ameshiriki ibada ya mazishi na kuwapa pole familia ya Marehemu akiwemo mume wa Marehemu,wazazi na ndugu wa Marehemu Kwa kupatwa na msiba huo.

Aidhaa Senyamule amesema kuwa mkoa wa Dodoma umepatwa na misiba miwili kati ya waliofariki kwenye ajali hiyo ambapo Serikali ya Dodoma iliwajibika kushiriki msiba mwingine uliofanyika Wilayani Kondoa.

"Nafahamu Watanzania wengi tumeumia na msiba huu lakini kama mnavyofahamu kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo tuhakikishe tunashirikiana na tunawapumzisha wenzetu walio tangulia mbele za haki ndio maana nami nipo hapa kuwakilisha Serikali kama tulivyoelekezwa na Rais hivyo nawapa pole wazazi, mume na ndugu kwa msiba mzito uliowapata kubwa ni kuhakikisha tunaendelea kuwaombea katika sala zetu za kila siku,"amesema Senyamule

Pia Sinyamule ametoa pole nyingi kwa shirika la (MDH) kwa kuwapoteza wafanyakazi wengi katika ajali hiyo ya ndege na amesema shirika hilo limekuwa likishirikiana  na serikali kufanya kazi mbalimbali za afya hapa nchini.

Neema Samwel alizaliwa Oktoba 26 mwaka 1994 ambapo alifariki katika ajali ya Ndege ya shirika la Precision Air iliyotokea Novemba 6 ziwa Victoria Bukoba Mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 19 huku watu 26 wakinusurika kwenye ajali hiyo.

WADAU WATAKIWA KUDHIBITI VITENDO VYA UKATILI

PUNGUZENI VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA MIMBA ZA UTOTONI

Na Wellu Mtaki, Dodoma

MKURUGENZI wa shirika la Kivulini linalojishughulisha na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni Yasini Ally amesema kuwa hali ya vitendo vya ukatili na mimba za utotoni katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ipo kwa kiwango cha juu hivyo serikali na wadau wote hawana budi kushirikiana ili kuweza kukabiliana na tatizo.

Ally amesema hayo Jijini Dodoma alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari juu ya utendaji kazi wa shirika lake.

Amesema kuwa Utafiti uliofanywa na shirika hilo umebaini katika kipindi cha mwaka 2015/ 2016 vitendo vya ukatili wa kijinsia ulikuwa wa hali ya uu ambapo mkoa wa Shinyanga ni asilimia 78, mkoa wa Mwanza asilimia 60 , mkoa wa Kigoma asilimia 61 na mkoa wa Mwanza pia una asilimia 25 kwa vitendo vya mimba za utotoni.

Aidha amefafanua kwamba hali hiyo pia inaweza kusababishwa pale jamiii ya kanda ziwa inapokuwa na hali nzuri ya kiuchumi kwa mfano wakati wa mavuno baadhi ya watu hutelekeza familia na kwenda kwenye mambo ya starehe.

Mkurugezi huyo ameongeza kuwa shirika Ilo limefanya kazi kubwa ya kujenga uwezo kwa klabu za wanafunzi Ili kudhibiti mimba za utotoni.


Friday, November 4, 2022

LAINI 58.1 ZASAJILIWA


WATUMIAJI WA SIMU WAONGEZEKA NCHINI 

Na Wellu Mtaki, Dodoma

SEKTA ya Mawasiliano ya Simu nchini imeendelea kukua hadi kufikia Septemba 2022 kulikuwa na laini za simu za milioni 58.1 idadi hiyo inahusisha laini zinazotumiwa na watu pamoja na zinatotumiwa kwa ajili ya Mashine (M2M).

Aidha takwimu zinaonesha mikoa mitano inayoongoza nchini kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika (Active SIM-Cards) hadi kufikia Septemba mwaka huu ni Dar es Salaam laini milioni 9.7, Mwanza milioni 3.7, Arusha 3.4, Mbeya 3.08 na Tabora 3.06.

Akizungumza jiijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo ,Dk. Jabir Bakari amesema kuwa wanawatoa huduma sita kwenye soko lao ambao ni Airtel, Vodacom, Halotel, Ttcl, Tigo na Smile.

Dk. Bakari ameeleza kuwa mgawanyo wa asilimia za soko kwa kila mtoa huduma ni kwamba Vodacom asilimia 30, Airtel asilimia 28, Tigo asilimia 26, Halotel asilimia 13, Ttcl asilimia 3 na Smile asilimia 0.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa takwimu zinaonesha matumizi ya Intaneti yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka milioni 29 hadi kufikia 31. 12 mwezi Septemba mwaka huu.

Amefafanua kuwa ongezeko la matumizi ya Intaneti limechangiwa na matumizi ya kiswahili na kwamba maudhui hayo kwenye Intaneti yanaongezeka kwa kasi na program tumizi (applications), kwa lugha ya kiswahili nazo zimeongezeka.


KITUO CHA TAALUMA USAFIRI WA ANGA


KITUO CHA TAALUMA USAFIRI WA ANGA KUBORESHWA

Na Wellu Mtaki, Dodoma

TAKRIBANI shilingi bilioni 49 zimekopwa tutoka benki kuu ya Dunia kwa ajili ya kituo cha umahiri cha mafunzo ya taaluma za usafiri wa anga kwa ajili wa utekelezaji wa miundombinu ya chuo hicho.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) Prof.Zacharia Mganilwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mganilwa amesema kuwa fedha hizo zimegawanyika katika upande wa ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kufundishia wataalam ambapo jumla ya majengo matano yatajengwa Dar- es Salaam kwa gharama ya shilingi bilioni 21 na baadaye kujenga majengo mkoa wa kilimanjaro kwa sababu lazima marubani wafundishwe ndani ya viwanja vya ndege.

Amesema kuwa chuo kimenunua ndege mbili zenye injini moja za mafunzo ambazo ziko njiani zinatazamiwa kuletwa Tanzania kwa gharama ya shilingi dola za Marekani milioni 12 huku akieleza kwamba kumfundisha rubani mmoja nje ya nchi ni shilingi milioni 200 hivyo Serikali inapofanya uwekezaji huu inalifanya shirika la ndege nchini kuleta matumaini ya nchi katika kukuza utalii na uchumi kwa sababu wataalam wa usafiri wa anga watafundishwa hapa hapa nchini.

Aidha amesema kuwa Tanzania ina zaidi ya ndege 400 zilizosajiliwa na mamlaka ya usafiri wa Anga ambapo asilimia 60 ya marubani ni wageni,hivyo ndege hizi zitakapofika vijana wa kitanzania wenye sifa za kusomea urubani watafundishwa na kupata ajira ndani ya nchi.

Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23 chuo kinanunua tena ndege yenye injini mbili kwa ajili ya mwanafunzi kukamilisha mafunzo yake kwa sababu mafunzo ya urubani yanamtaka mwanafunzi ajifunze ndege yenye injini moja na injini mbili.

NIT watawawezesha vijana wengi kunufaika na miradi mikubwa inayoendelea nchini mathalani ndege tano zinatarajiwa kuja nchini,ambapo kwa mwaka 2023 ndege nne zitaingia nchini.


Thursday, November 3, 2022

WIZARA AFYA KUDUMISHA HUDUMA ZA AFYA


WATUMISHI KUWA WAKUTOSHA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

Dodoma,

Katibu Mkuu,Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema Wizara ya Afya inaendelea kuimarisha huduma za afya kwa kuwa na watumishi wa kutosha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Prof. Makubi amesema hayo leo tarehe 3 Novemba, 2020 wakati wa kikao cha Sekretarieti ya maandalizi ya Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote na Menejimenti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikiwa ni kuelezea hatua iliyofikiwa pamoja na nini kifanyike kama sekta moja endapo Muswada huo utapitishwa na Bunge na kuwa Sheria.

Aidha, Prof. Makubi amesema Wizara ya Afya inaendelea kuboresha upatikanaji wa Dawa, vifaa tiba na vipimo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili huduma zinazotolewa ziwe bora.

"Afya ni kitu muhimu na ndio haki ya kwanza ambayo Mungu amempa Mwanadamu hivyo kila mmoja lazima athamini uhai wake kwa kuwa na Bima ya Afya".

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alisema dhana ya bima ya afya kwa wote ni kuchangiana pindi mmoja anapougua aweze kupata matibabu bila kuwa na kikwazo cha fedha.

Naye, Naibu Katibu Mkuu-Afya kutoka TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amesisitiza utoaji wa elimu kwa wananchi ngazi zote ili waelewe zaidi dhana nzima ya Bima ya Afya kwa Wote.

HUDUMA ZA NDEGE ZAONGEZEKA NCHINI.

VIWANJA VYA NDEGE VYAONGEZA HUDUMA ZA NDEGE NCHINI.


Na Wellu Mtaki, Dodoma

JUMLA ya ndege 40,323 zilihudumiwa katika kipindi cha mwaka 2021/2022 ikilinganishwa na huduma iliyotolewa mwaka 2020/2021 sawa na ongezeko la asilimia 13. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Huduma za Utabiri - Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/23 katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Novemba 2, 2022 Jijini Dodoma.

Dkt Kabelwa amesema kuwa sekta ya usafiri wa anga inaendelea kukua kutokana na kuzingatiwa kwa mfumo wa kudhibiti ubora wa huduma na ongezeko hilo linatokana na jitihada za kuifungua nchi zinazofanywa na serikali, pamoja na kuendelea kukidhi viwango vya Kimataifa na kuihakikishia dunia usalama wa anga la Tanzania katika masuala ya hali ya hewa kwa ndege zote za kimataifa.

Amesema kuwa mamlaka hiyo katika mwaka 2021/22 iliendelea na utengenezaji wa rada mbili zitakazofungwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) na cha Jiji la Dodoma ambao umefikia asilimia 45.

Ameongeza kuwa Mamlaka imeendelea kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake iliyopewa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani ya kuwa Kituo cha kutoa mwongozo wa utoaji wa utabiri wa hali ya hewa kwa nchi za ukanda wa Ziwa Victoria (Regional Specialized Meteorological Centre) kwa nchi zilizopo Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa ametoa wito kwa Wananchi kujenga utaratibu wa kutumia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Majukumu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)yamegawanyika katika sehemu kuu tatu ambapo sehemu ya kwanza ni kutoa huduma za hali ya hewa; sehemu ya pili ni kudhibiti shughuli za hali ya hewa hapa nchini kwa mujibu wa Kifungu cha (14) na sehemu ya tatu ni kuratibu shughuli za hali ya hewa nchini Tanzania kulingana na Kifungu cha (5) cha Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na.2 ya Mwaka 2019.

Mwisho

Sunday, October 30, 2022

JWT PWANI YAITA WAFANYABIASHARA KUJIUNGA NA JUMUIYA




WAFANYABIASHARA PWANI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KWENYE JUMUIYA 

Na John Gagarini

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Pwani imewataka wafanyabiashara kujiunga ili wanufaike na fursa mbalimbali zilizopo kwenye Jumuiya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekekezaji wa majukumu ya taasisi hiyo pamoja na fursa zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo katibu wa JWT Mkoa Wellu Mtaki amesema kwenye Jumuiya hiyo kuna fursa nyingi.

Mtaki amesema kuwa Jumuiya hiyo inamuwezesha mfanyabiashara kutatua changamoto zake na mfanyabiashara anauwezo wa kutoa kero maoni na mapendekezo yanayohusu biashara na taasisi ikafikisha sehemu husika kwa ajili ya utatuzi tofauti na mtu kupeleka kero yake mwenyewe.

"Lengo la Jumuiya ni kuwaunganisha kwa pamoja wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwawezesha kutoa mawazo na maoni yao kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa na kuziwasilisha serikalini,"amesema Mtaki

Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kutengeneza mazingira bora ya kufanya biashara nchini Tanzania na moja ya huduma ni kuwaunganisha na bima za aina tofauti ambazo zimeanza kutolewa kwa wanachama.

"Huduma za bima zinazotolewa ni pamoja na bima ya Elimu au Carrier Life Plan kupitia shirika la bima la Jubilee ambalo linamsaidia mtoto wa mwanachama kunufaika kwenye elimu, bima ya Afya ambayo ina kifurushi cha aina tatu ambacho Scare individual and Family health insurance, pamoja Afya, Jubilee Afya na huduma ya bima ya nafaka," Amesema Mtaki.

Ametoa wito kwa wafanyabiashara wote mkoani Pwani kuhakikisha wanafuata taratibu na miongozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) ili kepuka changamoto zitakazojitokeza.

Aidha amesema kuwa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania haijihusishi wala kufungamana na udini, ukabila, siasa, wala ushabiki wa michezo.


RAIS SAMIA KUZINDUA MATOKEO YA SENSA


RAIS SAMIA KUTANGAZA MATOKEO YA SENSA KESHO.

Na Wellu Mtaki, Dodoma.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kutangaza matokeo ya Sensa ya watu na Makazi Oktoba 31 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Juma ameyasema hayo Jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwenye kikao maalumu cha wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa tukio hilo.

Juma amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa tukio la kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na anwani za makazi yamekamilika.

Ameeleza kuwa kazi kubwa ya kuratibu na kusimamia imefanywa na viongozi wa mkoa wa Dodoma na kilichobaki watakuwa wamekamilisha Oktoba 30.

Aidha amesema kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi la mwaka huu limefanyika kisasa zaidi tofauti na miaka ya nyuma na litaisaidia Serikali katika kupanga mipango yake ya kiuchumi,kijamii na maendeleo. Zoezi la sensa ya watu na makazi lilifanyika hivi karibuni.

Saturday, October 29, 2022

MATRILIONI YATENGWA MIRADI YA BARABARA NCHINI


TANROADS YATENGA TRILIONI 3.8 UTEKELEZAJI MIRADI YA BARABARA 

Na Wellu Mtaki, Dodoma

WAKALA wa Barabara Nchini (TANROADS) imetenga kiasi cha shilling trilioni 3.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja makubwa nchi nzima.

Hayo yamesemwa leo na mtendaji mkuu wa Tanrods injinia Rogatus Mativila alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanywa na wakala.

Mativila amesema kuwa tayari wakala wa barabara imefanya usanifu wa miradi hiyo ambayo baadhi ni madaraja makubwa sita ikiwa ni pamoja na daraja la bwawa la Mtera Mkoani Dodoma , daraja la Jangwani Mkoani Dar - es- Salam, daraja la mkoa wa Simiyu, daraja la Mzinga, daraja la Mtoroni na makaravati sehemu mbalimbali nchini.

Amesema kuwa mradi mwingine mkubwa utakaotekelezwa ni ule wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ataweka jiwe la msingi Oktoba 30 mwaka huu.

Ametoa wito kwa Watanzania hasa madereva wa magari kuitunza miradi hiyo kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kugharamia miradi hiyo.

UVCCM YAPONGEZA SHULE KUFUTA ZIRO


Na John Gagarini Kibaha

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Mkuza Wilaya ya Kibaha Mjini imetoa fedha na vyeti vya pongezi kwa walimu wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Nyumbu kwa kufanya vizuri kwenye baadhi ya masomo na kuondoa ziro kwenye shule hiyo.

Akizungumza kwenye mahafali ya 16 ya shule hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mkuza Hashim Kibonge alisema kuwa wameamua kuwapa motisha walimu ili waendelee kufanya vizuri ili kuongeza ufaulu shuleni hapo.

Kibonge alisema kuwa walimu hao wametekeleza vema ilani ya CCM juu ya masuala ya Elimu ikiwa ni moja ya vipaumbele vilivyopo kwenye ilani ya chama juu ya uboreshaji wa elimu.

"Tumetoa vyeti kwa walimu wa masomo ya Kiingereza, Baiolojia na Kiswahili walimu wote wamefanya vizuri lakini masomo haya tumeona tuwapongeze hawa lakini wote wamepambana kuleta mafanikio shuleni,"alisema Kibonge.

Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mkuza Matata Ngolo alisema kuwa wamekuwa wakiifuatilia shule hiyo na kuona jinsi inavyopambana kuhakikisha watoto wanapata elimu inayostahili.

Ngolo alisema shule hiyo licha ya kuwa na wanafunzi wengi lakini imeendelea kufanya vizuri kwenye Halmashauri ya Mji wa Kibaha ambapo ufaulu kwa mwaka jana ilikuwa asilimia 99.

Naye Mgeni rasmi Naibu Kamishna wa Elimu Bahati Chikwindo alisema kuwa Wizara itasaidia shule hiyo kuhakikisha inakabili changamoto za shule hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo la utawala.

Chikwindo alisema kuwa watasaidia pia upatikanaji wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili wanafunzi waweze kupata elimu hiyo ambayo ni muhimu kwa kipindi hichi cha utandawazi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Juma Mrope alisema kuwa shule hiyo ndiyo shule inayoongoza kwenye Mkoa huo ambapo ina wanafunzi 2,136 huku wahitimu wa kidato cha nne walikuwa ni 460.

Mrope alisema kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni kutokuwa na jengo la utawala hali ambayo inasababisha watumie madarasa matatu hivyo kusababisha mlundikano wa wanafunzi kwani kuna upungufu wa madarasa unaofanya wanafunzi wasome kwa awamu mbili.

Akisoma risala ya wahitimu wa kidato cha nne Ahmed Kikoto alisema kuwa wanahitaji viti na meza zaidi ya 300, wanahitaji maktaba, ukarabati wa sakafu na kuomba kujengewa ukumbi.

Kikoto alisema kuwa wanawashukuru wadau mbalimbali kwa kuwapatia miradi mbalimbali ikiwemo wa Tehama na serikali kujenga shule shikizi ya Sofu ambapo imepunguziwa wanafunzi 75.

WATANZANIA WATAKIWA KULA NYAMA


DKT. MUSHI AMEWASISITIZA WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KULA NYAMA

Na Wellu Mtaki, Dodoma

MSAJILI wa bodi ya nyama nchini Dkt Daniel Mushi amewasisitiza Watanzania kujenga utamaduni wa kula nyama ili kukabiliana na utapiamlo.

Aidha utafiti unaonyesha Mtanzania mmoja hula kilo 15 za nyama badala ya kilo 50 kama inavyotakiwa

Ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo .

Dkt Mushi amesema kwamba utafiti uliofanywa na bodi hiyo umebaini baadhi ya nchi za Ulaya na nyinginezo mtu mmoja anakula kilo hadi 100 kwa mwaka.

Amepinga kauli ya watu kuwa nyama nyekundu ni hatari bali mlaji anatakiwa kuandaa nyama vizuri kuanzia katika kuipika hadi kwenye ulaji.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa kwa sasa wana mipango thabiti ya kutafuta masoko ya uhakika kwani mahitaji ya nyama nje ya nchi ni makubwa lakini Tanzania inasafirisha nyama kwa kiwango kidogo.



MADAKTARI BINGWA KUSOMESHWA


WIZARA YA AFYA YAANDAA MPANGO WA KUSOMESHA MADAKTARI BINGWA NA WABOBEZI.

Na Wellu Mtaki, Dodoma 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetoa ufadhili wa shilingi bilioni nane kwa kuwasomesha madaktari bingwa na wabobezi ili kukabiliana na uhaba wa wataalamu hao.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Waziri Ummy amesema mpango huo unaojulikana kama Samia Scholaship utasomesha madaktari ngazi za ubingwa 139 watasoma nje ya nchi na wengine 318 watasomea hapa nchini.

Mwalimu amesema kuwa mpango huo utakuwa ni kwa seti akitolea mfano daktari bingwa wa magonjwa ya figo atakwenda kusoma pamoja na muuguzi na mtaalamu wa dawa ya usingizi ambapo jumla watakuwa watatu katika ugonjwa mmoja.

Amefafanua kuwa katika mpango huo tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameikabidhi Wizara ya afya kiasi cha shilingi bilioni nane ambazo zitatumika kama ada na posho nyingine watakapokuwa mafunzoni.

Ameongeza kuwa Serikali imeamua kufanya hivyo baada ya kuona nchi inakabiliwa na upungufu mkubwa wa huduma za kibingwa na ubobezi.




Friday, October 28, 2022

WAVAMIZI WAMACHINGA KUCHUKULIWA HATUA










WAVAMIZI WA SOKO LA WAMACHINGA COMPLEX DODOMA WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA 

Na Wellu Mtaki,Dodoma. 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Sinyamule amewakata wale wasio na sifa za machinga wasiingie kwenye soko la Wamachinga Complex kwani soko hilo limejengwa kwa ajili ya wamachinga.

 Sinyamule ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati wa kusikiliza kero za wamachinga Dodoma kuhusu changamoto zinazowakabili. 

Sinyamule amesema kuwa baadhi wamefanya maombi kwa kudanganya taarifa ili wapate nafasi ndani ya soko hilo na wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. 

"Jiji endeleeni kutatua kero zitakazojitokeza ili wafanyabiashara wadodo wadogo waendelee kufanya biashara kwa amani na endapo kama kutajitokeza upungufu wa vizimba watapangiwa maeneo mengine,"amesema Sinyamule. 

Aidha ametangaza kuwa tatehe rasmi ya Wamachinga kuingia kwenye soko hilo ni tarehe Oktoba 28 na 30 mwaka huu na kuwataka viongozi wa Halmashauri ya Jiji kukaa eneo hilo siku zote kwa ajili ya kusimamia zoezi hilo na kuwataka LATRA kuhakikisha Daladala zinapitika njia ya soko hilo ifikapo Novemba Mosi na kunakuwa na kituo cha kupitia na kushushia abiria.

"Wamachinga fedha za mikopo zipo bali changamoto ya mikopo ni kuwa baadhi ya watu wanaunda vikundi vya watu watano ambapo ndani ya kundi hilo hakuna machinga hivyo ni vigumu kupata mkopo huo hivyo nawataka Wamachinga kuwa waaminifu kwenye zoezi la kukopa na waunde vikundi kwani fedha za mikopo zipo,"amesema Sinyamule.

Kwa upande wake Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema Kuwa kuna mifuko zaidi ya 69 inatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na kuna taasisi za fedha hivyo mikopo ipo kila mmoja atapata mkopo huo kwa kufuata taratibu. 

Mwisho

Thursday, October 27, 2022

WAVAMIZI SOKO WAMACHINGA KUCHUKULIWA HATUA KISHERIA HATUA

WAVAMIVI WA SOKO LA WAMACHINGA COMPLEX DODOMA WATACHUKULIWA HATUA YA KISHERIA Na Wellu Mtaki, Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Sinyamule amewakata wale wote ambao awana sifa za machinga wasiingie kwenye soko ilo kwani soko limejengwa KWa ajiiri ya wanachinga tu KWa yoyote atakayebainika ameingia bila sifa za umachinga hatua za kisheria zitachukuliwa. Pia amewataka wamachinga kuamia kwenye soko ilo KWa amani ,Uaminifu na uhadilifu pasipo kuibiana Pamoja na kuzingatia usafi wa Mazingira. Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa huyo wakati wa kusikiliza kero za wamachinga jijini dodoma kuhusu changamoto zinazowakabili wamachinga dodoma. Sinyamule amesema Kuwa wapo ambao wamefanya maombi KWa kudanganya taarifa ili wapate nafasi ndani ya soko ilo, endapo wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa. Aidha amewataka halmashauri ya jiji kutatua kero zote zinazojitokeza na ambazo zitajitokeza hapo baadae " Jiji endeleeni kutatua kero hizi na zitakazojitokeza Ili kuhakikisha wafanyabiashara wadodo wadogo wanafanya biashara KWa amani na endapo kama kutajitokeza upungufu wa vizimba watapangwa maeneo mengine"Amesema Sinyamule. Pamoja hayo Sinyamule ametangaza rasmi tarehe 28 hadi 30 octpbar mwaka huu ndiyo siku ya kuaza kuingia wamachinga kwenye soko ilo uku akiwataka viongozi wa Halmashauri ya jiji kukaa eneo ilo siku zote KWa ajiiri ya kusimamia zoezi ilo pamoja na kuwataka LATRA kuhakikisha kuwa kufikia tarehe 1 November daladala zinapitika njia ya soko hilo na kunakuwa na kituo cha kupitia na kushushia abiria. Pia Sinyamule amewahakikishia Wamachinga fedha za mikopo zipo bali changamoto ya mikopo ni kuwa baadhi ya watu wanaunda vikundi vya watu watano ambapo ndani ya kundi ilo hakuna machinga hivyo ni vigumu kupata mkopo huo hivyo amewataka Wamachinga kuwa wahaminifu mwenye zoezi la kukopa na waunde vikundi fedha za mikopo zipo. Kwa upande wake Katibu tawala Mkoa wa dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema Kuwa kuna mifuko zaidi ya 69 inatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo pia kuna taasisi za fedha hivyo mikopo ipo kila mmoja atapata mkopo huo kwa kufata taratibu zilizopo. Mwisho

BMH YATOA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO

Na Wellu Mtaki, Dodoma BMH IMEAZA KUTOA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO. HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH), imeanza kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto waliobainika kuzaliwa na matatizo ya moyo ambapo tayari watoto 10 wameshahudumiwa. Pia Serikali imeokoa zaidi ya Shilingi bilioni 2.3 kutokana na huduma za upandikizaji wa figo kwa wagonjwa 31 ambao wametibiwa kwa gharama ya Shilingi milioni 25 ambapo wangeenda kutibiwa nje ya nchi ingegharimu milioni 100 kwa mtu mmoja. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Oktoba 26, 2022,Mganga mkuu wa BMH Dk. Alphonce Chandika wakati akitoa taarifa ya utekelezaji na vipaumbele vya hospitali hiyo kwa mwaka 2022/ 2023 amesema wamefanikiwa kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa kuwa na maabara maalum inayotumika katika kutoa matibabu ya moyo pasipo kufungua kifua. Dk. Chandika ameeleza kuwa kuna wagonjwa nane ambao mapigo yao ya moyo yanashuka sana, walihudumiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kupandikizwa betri kwenye moyo na kupitia maabara hiyo wameweza kuhudumia watoto 14 waliozaliwa na matatizo ya moyo. Amesema wagonjwa 39 waliobainika kuwa na matatizo makubwa ya moyo wamehudumiwa kwa kuwekewa vipandikizi na kati ya 39, wagonjwa wawili kati yao walihudumiwa kwa dharura ambapo kama ingekuwa ni kusafirishwa kwenda kupatiwa matibabu Dar es Salaam wangepoteza maisha. Ameongeza kuwa hospitali BMH ni ya pili hapa nchini kutoa huduma hiyo na kwamba tangu mwaka 2019, na kwamba jumla ya wananchi 715 wamehudumiwa kwa kuchunguzwa. Daktari huyo amebainisha kuwa tangu mwaka 2020, Hospitali ilifanikiwa kuanzisha upasuaji wa nyonga na magoti kwa kuweka vipandikizi na tayari wagonjwa 56 wamewekewa vipandikizi hivyo kwa wastani wa gharama ya shilingi milioni 12 ambapo gharama za huduma hizo nchi za nje ni takriban milioni 35. Aidha ameongeza kuwa huduma hiyo imeshatolewa kwa wagonjwa 148 kwa gharama ya Shilingi milioni 1.2 kwa mgonjwa mmoja, kwa nje ya nchi gharama ni zaidi ya milioni 7 huku akieleza kwamba wagonjwa hao 148, Serikali imeokoa zaidi ya Shilingi milioni 850. Ikumbukwe kuwa jitihada za Serikali kuhakikisha inawaletea wananchi huduma za afya zilizo bora, ilidhamiria kuiwezesha Hospitali ya Benjamini Mkapa kuwa na vifaa tiba vya kisasa na vinavyotumia teknolojia ya kisasa ili iweze kukidhi adhma yake ya kuwahudumia wananchi hao kwa kuwapatia matibabu ya kiwango cha juu. Mwisho

HAZINA YAKUSANYA BILIONI 852.9

SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina katika mwaka wa fedha 2021/22 imekusanya 852.9 sawa na asilimia 109.5 ya lengo kutoka katika kampuni ambazo serikali inamiliki hisa. Imesema ongezeko hilo linatokana na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ni zaidi ya kiasi kilichokusanywa Juni 30 mwaka jana ambacho ni sh. bilioni 638.87. Hayo yalibainishwa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), Lightness Mauki, wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa ofisi hiyo katika mwaka huu wa fedha. Alisema fedha hizo zimekusanywa katika mapato yasiyo na kodi ambayo yanajumuisha gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi na mapato mengineyo kutoka katika taasisi 287 zilizo chini ya ofisi ya msajiri. “Kuongezeka kwa makusanyo hayo kunatokana na kuimarisha usimamizi,ufuatiliaji na tathmini ya uwekezaji wa mitaji ya umma pamoja na hatua ambazo zilichukuliwa katika kukuza mapato na kudhibiti matumzi. Aliongeza kuwa:"Hadi kufikia Juni 30 mwaka huu Ofisi ya Msajili wa hazina ilikuwa inasimamia mashirika ya umma 287 Kati ya mashirika hayo 237 serikali ina hisa zaidi ya asilimia 51, taasisi 40 serikali inahisa chache na 10 za nje ya Nchi ambazo serikali imeweka uwekezaji. Lightness alisema serikali imewekeza kwenye mashirika hayo fedha sh.trilioni 70. Alisema kuwa serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imeendelea na juhudi za kusimamia utendaji wa kampuni ambazo serikali inaumiliki wa hisa chache. Pia, alisema serikali inafanya majadiliano na wabia wenza na kusimamia kwa ukaribu matumizi yasiyo ya lazima, hivyo kuchangia ongezeko la gawio. "Mathalani mafanikio ya jitihada hizo yamejidhihirisha katika utendaji wa Banki ya NBC ambayo imeongeza faida kabla ya kodi kutoka sh. bilioni 7 mwaka 2020 hadi sh. bilioni 60 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 757, ukuaji huu wa faida umewezesha benki kutoa gawio kwa serikali sh. bilioni 4.5 kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa,"alieleza. Akitaja mafaniko ya Ofisi hiyo Lightness alisema wameweza kufanya upanuzi wa kiwanda cha sukari cha Kilombero ambacho serikali inamiliki asilimia 25 ya hisa. Alisema kutokana na kukua kwa mahitaji ya sukari nchini kulikuwa na uhitajio wa kupanua kiwanda cha sukari hicho ili kutimiza mahitaji. “Bodi ya wakurugenzi baada ya kufanya upembuzi yakinifu iliwasilisha mapendekezo ya kupanua kiwanda hicho ambapo sh. bilioni 571.6 zilitumika, uwekezaji huo unatarajia kuongeza kiwango cha uzalishaji sukari hadi kufikia tani 271,000 kutoka tani 127,000 za sasa,” alisema. .

Friday, May 20, 2022

KEDA YATOA MSAADA WA MARUMARU ZA MAMILIONI KWENYE SHULE ZA SEKONDARI

KIWANDA cha kutengeneza Marumaru cha Keda (T) Ceramics Co. Ltd kilichopo Pingo Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani kimetoa Marumaru zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kwa shule za Pera na Msata. Akizungumza mara baada ya kuzikabidhi shule hizo Ofisa Tawala wa kiwanda hicho George Lulandala alisema kuwa maramaru hizo ni kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya usomaji kwa wanafunzi. Lulandala alisema kuwa wametoa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha mchango wao kwa jamii ambapo wamekuwa wakishiriki shughuli za wananchi ili kuwaletea maendeleo. "Tumeamua kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwani ameonyesha kuwajali wananchi wakiwemo wanafunzi ambapo amefanya mambo mengi kwenye sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa na miundombinu,"alisema Lulandala. Alisema kuwa wameamua kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha mazingira ya elimu ili wanafunzi wasome katika mazingira mazuri ambayo yatawafanya wapate uelewa vizuri. "Sekondari ya Msata imepatiwa maboksi 203 huku Pera Sekondari wakipata maboksi 100 na bado tutaendelea kutoa misaada mbalimbali ili kuhakikisha kuboresha sekta mbalimbali,"alisema Lulandala. Aidha alisema kuwa kwa kipindi cha nyuma walisaidia kituo cha afya cha Pera na huduma mbalimbali kwa wananchi kwenye maeneo mbalimbali kwenye wilaya na mkoa. "Tunafanya jitihada mbalimbali kusaidia masuala ya jamii hivyo hata wadau wengine nao wanapaswa kuisaidia serikali ili iweze kuwahudumia wananchi wake,"alisema Lulandala. Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Iddi Ng'oka alisema kuwa wanashukuru kiwanda hicho kwa msaada walioutoa kwani bila ya kuweka Marumaru sakafu imekuwa ikiharibika mara kwa mara. Ng'oka alisema kuwa wanaomba wapewe tena maramaru kwani kuna baadhi ya madarasa hayana Marumaru pamoja na ofisi hivyo wakipatiwa nyingine itasaidia sana. Mwisho.