MKUU WA MKOA WA DODOMA MAZISHI MTUMISHI MDH ALIYEFARIKI AJALI YA NDEGE.
Na Wellu Mtaki, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameshiriki ibada ya mazishi ya Marehemu Neema Samwel aliyefariki kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air Mkoani Kagera ambapo mazishi hayo yaliofanyika nyumbani kwao Ilazo Jijini Dodoma.
Marehemu Neema alikuwa anafanya kazi shirika (Management and Development for Health) (MDH) ambapo alikuwa anaelekea kwenye ziara ya kikazi mkoani Kagera na kukutwa na umauti.
Senyamule ameshiriki ibada ya mazishi na kuwapa pole familia ya Marehemu akiwemo mume wa Marehemu,wazazi na ndugu wa Marehemu Kwa kupatwa na msiba huo.
Aidhaa Senyamule amesema kuwa mkoa wa Dodoma umepatwa na misiba miwili kati ya waliofariki kwenye ajali hiyo ambapo Serikali ya Dodoma iliwajibika kushiriki msiba mwingine uliofanyika Wilayani Kondoa.
"Nafahamu Watanzania wengi tumeumia na msiba huu lakini kama mnavyofahamu kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo tuhakikishe tunashirikiana na tunawapumzisha wenzetu walio tangulia mbele za haki ndio maana nami nipo hapa kuwakilisha Serikali kama tulivyoelekezwa na Rais hivyo nawapa pole wazazi, mume na ndugu kwa msiba mzito uliowapata kubwa ni kuhakikisha tunaendelea kuwaombea katika sala zetu za kila siku,"amesema Senyamule
Pia Sinyamule ametoa pole nyingi kwa shirika la (MDH) kwa kuwapoteza wafanyakazi wengi katika ajali hiyo ya ndege na amesema shirika hilo limekuwa likishirikiana na serikali kufanya kazi mbalimbali za afya hapa nchini.
Neema Samwel alizaliwa Oktoba 26 mwaka 1994 ambapo alifariki katika ajali ya Ndege ya shirika la Precision Air iliyotokea Novemba 6 ziwa Victoria Bukoba Mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 19 huku watu 26 wakinusurika kwenye ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment