WAVAMIZI WA SOKO LA WAMACHINGA COMPLEX DODOMA WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
Na
Wellu Mtaki,Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Sinyamule amewakata wale
wasio na sifa za machinga wasiingie kwenye soko la Wamachinga Complex kwani soko
hilo limejengwa kwa ajili ya wamachinga.
Sinyamule ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati wa kusikiliza kero za wamachinga Dodoma kuhusu changamoto
zinazowakabili.
Sinyamule amesema kuwa baadhi wamefanya maombi kwa kudanganya
taarifa ili wapate nafasi ndani ya soko hilo na wakibainika hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
"Jiji endeleeni kutatua kero zitakazojitokeza ili
wafanyabiashara wadodo wadogo waendelee kufanya biashara kwa amani na endapo
kama kutajitokeza upungufu wa vizimba watapangiwa maeneo mengine,"amesema
Sinyamule.
Aidha ametangaza kuwa tatehe rasmi ya Wamachinga kuingia kwenye soko
hilo ni tarehe Oktoba 28 na 30 mwaka huu na kuwataka viongozi wa Halmashauri ya
Jiji kukaa eneo hilo siku zote kwa ajili ya kusimamia zoezi hilo na kuwataka
LATRA kuhakikisha Daladala zinapitika njia ya soko hilo ifikapo Novemba Mosi na
kunakuwa na kituo cha kupitia na kushushia abiria.
"Wamachinga fedha za mikopo
zipo bali changamoto ya mikopo ni kuwa baadhi ya watu wanaunda vikundi vya watu
watano ambapo ndani ya kundi hilo hakuna machinga hivyo ni vigumu kupata mkopo
huo hivyo nawataka Wamachinga kuwa waaminifu kwenye zoezi la kukopa na waunde
vikundi kwani fedha za mikopo zipo,"amesema Sinyamule.
Kwa upande wake Katibu
tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema Kuwa kuna mifuko zaidi ya 69
inatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na kuna taasisi za fedha hivyo
mikopo ipo kila mmoja atapata mkopo huo kwa kufuata taratibu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment