CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Picha ya Ndege Wilayani Kibaha imewataka watu wanaojifanya madalali wa watu wanaotaka kugombea nafasi za uenyekiti wa serikali za mitaa waache kwani muda wa viongozi walio madarakani haujaisha.
Wednesday, March 13, 2024
MADALALI WA KUPIGIA DEBE WAGOMBEA WATAKIWA KUACHA MARA MOJA
Tuesday, March 12, 2024
WAFANYABIASHARA WA DODOMA WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BIASHARA
Na Anna Misungwi, Dodoma
EWURA KUMTUA MWANAMKE KUNI KICHWANI
Na Wellu Mtaki, Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,amesema mamlaka hiyo ina wajibu kuhakikisha wanamtua mwanamke kuni na mkaa kichwani kwa kuhakikisha wanatoa leseni kwa wakati kwa wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza katika nishati safi ya kupikia.
Dkt. Andilile ameyasema hayo Machi 9,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.
Amesema taifa bado linatumia nishati isiyosafi kwa kupikia hivyo EWURA itahakikisha ina wajibu wa kuhakikisha inatekeleza mikataba ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ikiwemo uharibifu wa mazingira na madhara ya afya yanayosababidhwa na moshi wakati wa matumizi ya kuni na mkaa.
“EWURA tutahakikiha tunahamasisha uwekezaji katika nishati safi kwa kutoa leseni kwa wawekezaji kwa wakati ili wawekeze katika eneo hilo, pia tunaangalia upatikanaji wake katika maeneo mengi kwa kuangalia mwenendo wa bei za bidhaa hiyo,” amesema Dkt. Andilile.
Ameongeza kuwa:”Sisi kama EWURA tutahakikisha kama ilivyo dhamira ya Rais kumtua ndoo mama kichwani, tutamtua mwanamke kuni kichwani kwa kuhakikisha anatumia nishati ambayo itamrahisishia kupata maendeleo badala ya kuhangaika na nishati chafu ya kupikia,”.
Monday, March 11, 2024
TISA WAFA AJALINI BAGAMOYO
WATU tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster kugongana uso kwa uso na lori.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SACP Pius Lutumo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea Machi 10 majiira ya saa 11:15 jioni huko Kiromo Wilaya ya Bagamoyo barabaraba kuu ya Bagamoyo Dar es Salaam.
Lutumo amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi hilo dogo lenye namba za usajiliT676 DSM likiendeshwa na dereva aitwaye Juma Mackey akitokea Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo ambapo dereva huyo na yule wa lori ni miongoni mwa waliofariki dunia.
Ametaja gari lingine lililohusika na ajali hiyo kuwa ni lori aina ya Howo mali ya VGK Limited lenye namba za usajili T 503 DRP na tela namba T 733 DUa likierndeshwa na dereva aitwaye Apolo Mgomela (52) mkazi wa Kibaha likitoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam.
Waliokuta ni wanaume saba na wanawake yawawili ambapo majeruhi walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa matibabu na pamoja na marehemu," amesema Lutumo.
Ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa lori kuyapita magari menginep asipokuchukua tahadhari na kuligonga basi ambalo lilikuwa linakuja mbele yake ambapoa metoa wito kwa wananchi na watumiaji wote wa barabara hasa madereva kufuata sheria zau salama barabarani ili kuepusha ajali zinazogharimu maisha ya watu.
KATA YA MAILI MOJA WAELEZEA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
KATA ya Maili Moja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani imeelezea mafanikio na changamoto huku wakiitaka Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kukarabati miundombinu ya barabara ambayo imeharibika vibaya.
Saturday, March 9, 2024
BAWACHA YAWATAKA WANAWAKE WANAOLEA WATOTO PEKE YAO KUOMBA MSAADA
Na, Wellu Mtaki, Dodoma
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA (BAWACHA) Sharifa Suleiman amewakumbusha wazazi wanaoleo watoto peke yao kuomba msaada wa malezi kwani kumekuwa na wimbi kubwa la watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili
Bi. Sharifa ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma huku akiongeza kuwa suala la malezi na makuzi linahitajika kwa pande zote mbili kwani wanategemeana kwenye malezi.
Aidha ameongeza kuwa changamoto ya afya ya akili imefanya wazazi wengi kukimbia familia zao jambo linalofanya hali ya familia kwasasa kuwa katika hali mbaya.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amewasisitiza wanawake kuwa na udhubutu wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi serikalini.
Nao baadhi ya wahudhuriaji katika maadhimisho hayo wamezungumzia kuhusiana na kitu kinachosababisha wanaume wengi kukimbia familia zao na kushindwa kutimiza jukumu lao la malezi.
Friday, March 8, 2024
WANAWAKE WATAKIWA KUWA NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA
Na Wellu Mtaki, Dodoma
WANAWAKE nchini wametakiwa kutambua suala la matumizi sahihi ya fedha ili kuweza kujiongezea kipato zaidi na kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Mkurugezi Msaidizi sehemu ya usimamizi Rasilimali watu Wizara ya fedha Bi, Faudhia Nombo wakati akimwakilisha katibu mkuu wizara ya fedha katika maonesho ya banda la wizara hiyo leo Machi 7 siku ya ufunguzi wa maonyesho ya wanawake kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Nombo amesema wizara inaendelea kutoa Elimu kwa wanawake kujiandaa wakati wa kustafu kazi katika kipindi cha uzee pamoja na suala la kutunza fedha
"Wizara haitokaa kimya ila itahakikisha inaendelea kutoa Elimu kwa wanawake ili pindi wanapostafu kazi wapate fedha za kujikimu kipindi chote cha uzee , wapo wanawake wanatumia fedha katika majukumu ambayo si sahihi na mwisho wa siku fedha hupotea na kuelekea mwisho mbaya uzeeni," amesema Nombo.
Aidha amesema kuwa wanawake wengi wanatamani kuingia katika vikoba ili kuweza kujikimu kiuchumi ila wanashidwa kutambua namna ya utunzaji wa fedha hivyo wizara imeona watoe mafunzo ya namna ya kutunza fedha katika maonesho ya siku ya wanawake Dunia.
Pia ametoa wito kwa wanawake wa Dodoma kutambua fursa zilizopo katika wizara hiyo na kutumia kiusahihi ili kufanikisha shughuli zao za kiuchumi.