Saturday, March 9, 2024

BAWACHA YAWATAKA WANAWAKE WANAOLEA WATOTO PEKE YAO KUOMBA MSAADA


Na, Wellu Mtaki, Dodoma 

Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA (BAWACHA) Sharifa Suleiman amewakumbusha wazazi wanaoleo watoto peke yao kuomba msaada wa malezi  kwani kumekuwa na wimbi kubwa la watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili

Bi. Sharifa ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya  siku ya Wanawake Duniani ambapo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma huku akiongeza kuwa suala la malezi na makuzi linahitajika kwa pande zote mbili kwani wanategemeana kwenye malezi.

Aidha ameongeza kuwa changamoto ya afya ya akili imefanya wazazi wengi kukimbia familia zao jambo linalofanya hali ya familia kwasasa kuwa katika hali mbaya.

Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amewasisitiza wanawake kuwa na udhubutu wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi serikalini.

Nao baadhi ya wahudhuriaji katika maadhimisho hayo wamezungumzia kuhusiana na kitu kinachosababisha wanaume wengi kukimbia familia zao na kushindwa kutimiza jukumu lao la malezi.

No comments:

Post a Comment