Na Wellu Mtaki, Dodoma
Bonanza la mpira wa miguu, kuvuta kamba na mpira mikono limefanyika leo Jijini Dodoma likiwashirikisha watumishi mbalimbali wa Wizara ya Fedha kutoka Bara na Visiwani.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala rasilimali watu Wizara ya Fedha Lusius Mwenda amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kudumisha ushirikiano na undugu kati yao.
Na kusema kuwa kuna tija inayopatikana ikiwemo kuimarisha urafiki wa pande zote mbili, kufahamiana na kuimarisha afya za Watumishi.
"Lengo kubwa katika mashindano ni Ushirikiano kati yetu,sisi huku Tanzania Bara na wenzetu wa Zanzibar".
"Tija kubwa ambayo inapatikana ni pamoja na watumishi kuimarisha afya, kufahamiana na kuwa na urafiki wa pande zote mbili, kwa mfano kwa sisi kwenda kule Zanzibar na wao kuja huku kama ambavyo tumekuwa tukifanya".
Akizungumza Mwakilishi kutoka Zanzibar Bwana Rajab Uweje ofisa Uendeshaji Ofisi ya Raisi fedha na mipango Zanzibar amesema kuwa Tamasha hilo ni ishara nzuri tumelikuta na hivyo tuliendeleze.
"Kwanza bonanza hili tunajenga uhusiano baina yetu nichukue nafasi hii kuzishukuru Taasisi zetu mbili kutudhamini katika Tamasha hili na hiki ni kitu chema sana tumekikuta na hivyo kwahiyo tukiendeleze kwa vizazi vyetu".
Mwenyekiti wa Hazina Sports Club Mugusi Musita amezungumzia suala la mikakati ya uboreshaji wa Tamasha hili kwa muda mrefu ikiwemo kuongeza wigo wa timu shiriki katika Tamasha hili ambapo kwa mwaka huu wamefaniki na kuweza kuongeza timu mpaka kufika sita.
"Kawaida huwa tunacheza Hazina ya Tanzania Bara na Zanzibar lakini mwaka huu tumekuwa na timu sita kwa hiyo mikakati tuliyoiweka ni kuboresha kama kuongeza timu umeona kama polisi walikuwepo hapa lakini kujenga mahusiano mazuri na wenzetu sisi kama Wizara za Kimuungano wenzetu wa visiwani tunafanya kazi moja na ndo tunaboresha mahusiano na kuboresha afya".
Tamasha hili la Pasaka limekuwa likifanyika kwa zaidi ya miaka ishirini mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment