Monday, March 11, 2024

TISA WAFA AJALINI BAGAMOYO

WATU tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster kugongana uso kwa uso na lori.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SACP Pius Lutumo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea Machi 10 majiira ya saa 11:15 jioni huko Kiromo Wilaya ya Bagamoyo barabaraba kuu ya Bagamoyo Dar es Salaam.

Lutumo amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi hilo dogo lenye namba za usajiliT676 DSM likiendeshwa na dereva aitwaye Juma Mackey akitokea Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo ambapo dereva huyo na yule wa lori ni miongoni mwa waliofariki dunia.

Ametaja gari lingine lililohusika na ajali hiyo kuwa ni lori aina ya Howo mali ya VGK Limited lenye namba za usajili T 503 DRP na tela namba T 733 DUa likierndeshwa na dereva aitwaye Apolo Mgomela (52) mkazi wa Kibaha likitoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam.

Waliokuta ni wanaume saba na wanawake yawawili ambapo majeruhi walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa matibabu na pamoja na marehemu," amesema Lutumo.

Ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa lori kuyapita magari menginep asipokuchukua tahadhari na kuligonga basi ambalo lilikuwa linakuja mbele yake ambapoa metoa wito kwa wananchi na watumiaji wote wa barabara hasa madereva kufuata sheria zau salama barabarani ili kuepusha ajali zinazogharimu maisha ya watu.

No comments:

Post a Comment