MKURUGENZI wa Kampuni ya Njuweni Ltd Alhaj Yusuph Mfinanga ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni tano kwa mwanafunzi atakayefaulu na kuongoza kitaifa kwenye mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kutoka shule tatu zinazomilikiwa na kampuni hiyo.
Sunday, September 17, 2023
MWANAFUNZI ATAKAYE ONGOZA KITAIFA DARASA LA SABA KIPS KUPATA MILIONI TANO
MKURUGENZI wa Kampuni ya Njuweni Ltd Alhaj Yusuph Mfinanga ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni tano kwa mwanafunzi atakayefaulu na kuongoza kitaifa kwenye mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kutoka shule tatu zinazomilikiwa na kampuni hiyo.
Tuesday, September 12, 2023
*ASKARI WA TAWA WAMUOKOA MTOTO WA TEMBO ALIYETUMBUKIA SHIMONI*
Na Beatus Maganja, TAWA
Askari wahifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) septemba 11, 2023 walifanikiwa kumuokoa mtoto wa tembo anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki nne (4) aliyezama katika shimo lenye matope katika Kijiji cha Kwamsanja kilichopo kata ya kibindu halmashauri ya Chalinze jirani na Pori la Akiba Wamimbiki.
Taarifa za Mtoto huyo wa tembo aliyetelekezwa na kundi lake kutumbukia shimoni zilitolewa na raia mwema aitwaye Manase Thomas Baha mkazi wa Kijiji cha Kwamsanja na kumlazimu Kamanda wa Pori la Akiba Wamimbiki Emmanuel Lalashe kutuma timu ya askari wanne (4) walioshirikiana na askari wa Jeshi la Akiba (migambo) sita (6) kwa ajili ya zoezi zima la kumuokoa mtoto huyo wa tembo.
Akizungumza baada ya zoezi la uokoaji, Kamanda Emmanuel Lalashe aliwashukuru wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi ya Wamimbiki kwa ushirikiano wanaoutoa katika kulinda rasilimali za Nchi yetu zilizopo katika hifadhi hiyo hususan rasilimali Wanyamapori ambazo ni chachu ya shughuli za Utalii na Pato la Nchi.
Mahusiano mazuri yaliyojengwa kati ya wahifadhi wa hifadhi ya Wamimbiki na wananchi wanaoishi vijiji Jirani na hifadhi hiyo umekuwa na manufaa makubwa siku za hivi karibuni kwani wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika shughuli za uhifadhi.
*DKT JAFO AFUNGUA MRADI WA MAJI KITUO CHA AFYA MZENGA*
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa RAIS Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo amefungua Mradi wa Maji katika Kituo Cha Afya Mzenga na kuwataka wananchi kuutunza Mradi huo 12.09.2023.
Akiziungumza wakati wa kufungua Mradi huo wa Maji alisema ni wajibu wa wananchi Hao wa Mzenga kuitunza miundombinu ya Mradi ili uweze kudumu kwa Muda mrefu huku ukiwahudimia wananchi mbalimbali na wale wanaofika Katika kituo cha Afya Mzenga,
*"Ndugu wananchi nimehangaika sehemu mbalimbali kutafuta wafadhili na kuwapata Hawa ndugu zetu Afrika Relief ambao wameweza kutusaidia kutatua hii kero ya maji hapa Mzenga niwashukuru sana Hawa afrika Relief kukubali kutujengea Mradi Huu mkubwa alisisitiza Mhe Dkt Jafo*"
Nae Meneja wa Taasisi ya Afrika Relief Kanda ya Tanzania Mohamed Gewily alishukuru kisarawe kwa kupokea msaada wa Mradi huo wa Maji huku akitaja umegarimu Shilingi Milioni Tisa na Laki Tatu na Elfu Hamsini hivyo akatoa wito zaidi kwa Wanakisarawe hasa Mzenga kuitunza miundombinu ya Mradi ili idumu na Kuendelea Kutoa huduma kwa Muda mrefu,
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya kisarawe katika ufunguzi wa mradi wa Maji Ndg Nancy Kasamala Alisisitiza kuhifadhi miundombinu ya Mradi pamoja na Kutoa wito kwa Jamii Kuendelea kuzitumia vyema Kamati za maji za Vijiji katika kusimamia Mradi,
*"Ndugu zangu tuliopo hapa naomba niwakushe jambo Moja kuna bodi ya maji Vijijini Hivyo nashauri mshirikiane na Uwongozi wa kituo Cha Afya Mzenga kwa kuendesha Mradi huu ambao umejengwa hapa kituoni badala ya Kijijini alishauri Ndugu Kasamala*"
Mradi Huu wa maji katika Tarafa ya Mzenga kata ya Mzenga Kijiji Cha Mzenga umefadhiliwa na Taasisi ya Afrika Relief umegarimu dhamani ya Milioni Tisa na Laki Tatu na Elfu Hamsini unategemea kuwahudumia watu Elfu Moja mia Nne na Sitini na Tatu pamoja watu mbalimbali wanaofika kituo Cha Afya Mzenga,
Aidha Mradi huo pia Unategemea kwa Raia kuchangia Bei ya Maji kwa Ndoo Moja ya lita Ishirini kwa Shilingi Arobaini Tu kwa Mujibu wa muongozo ili uweze kuendesha Miundombinu mbalimbali pamoja na Kukarabati.
WATOTO ZAIDI YA LAKI 4 KUPATA CHANJO YA POLIO MKOA WA SONGWE
Na. WAF - Songwe
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amebainisha kuwa zaidi ya watoto laki Nne wanatarajia kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio katika Mkoa wa Songwe.
Waziri Ummy ameyasema hayo Septemba 11, 2023 wakati akianza ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ambapo ameanza kutembelea katika Hospitali ya Wilaya hiyo, Zahanati ya Mbala pamoja na Kituo cha Afya Mbuyuni kilichopo katika Wilaya hiyo.
“Baada ya kupatikana kwa mtoto Mmoja mwenye ugonjwa wa Polio tumeamua kutoa chanjo ya ugonjwa huo ambapo kwa Mkoa wa Songwe tunatarajia kuchanja watoto takribani Laki Nne ambao wana umri chini ya Miaka Nane”. Amesema Waziri Ummy
Amesema, Mwaka 2015 Shirika la Afya Duniani (WHO) iliitangaza Tanzania kuwa ni nchi ambayo imetokomeza ugonjwa Polio, Mwaka huu 2023 Tanzania imepata Mtoto mwenye ugonjwa huo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkaoni Rukwa.
“Baada ya Miaka 8 toka WHO iitangaze Tanzania kumalizika kwa ugonjwa wa Polio, Mwaka huu 2023 tumepata mtoto mmoja kutoka Mkoa wa Rukwa ambaye ana virusi vya ugonjwa wa Polio (aina ya Pili)”. Amesema Waziri Ummy
Aidha, Waziri Ummy amesema kutokana na hatari iliyopo, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeamua kuendesha kampeni maalumu ya kutoa chanjo ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Amesisitiza kuwa, chanjo hiyo itatolewa katika Mikoa Sita iliyopo mipakani ambayo ni Mkoa wa Songwe, Kigoma, Rukwa, Katavi, Mbeya pamoja na Kagera.
“Mikoa Sita itafikiwa na zoezi hili na lengo ni kuwafikia zaidi ya watoto Mil. 3.5 ambao wana umri chini ya Miaka Nane kwa sababu watoto wote waliozaliwa kuanzia Mwaka 2016 walipata chanjo ya Polio ya kukinga kirusi aina ya kwanza”. Amesema Waziri Ummy
Pia, Waziri Ummy amesema zoezi hilo la utolewaji wa chanjo litaendeshwa kwenye vituo vya kutoa huduma za Afya, mashuleni, nyumba kwa nyumba, sehemu za ibada na vilabuni.
“Wakati wa zoezi hili tutawatumia watu Watatu Watatu katika kila timu ambao watapita kama ni mashambani, mashuleni au masokoni kwa ajili ya kuwapa watoto chanjo hiyo dhidi ya ugonjwa wa Polio ili tuwakinge watoto wetu na ugonjwa huo”. Amesema Waziri Ummy
KIBITI WAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO NYERERE SUPER CUP
Picha ya matukio ya Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani ikiwakirishwa na Ndugu Omary Punzi Katibu wa Taasisi hiyo wakikabidhi Tshirt na Mipira ya zawadi ya mashindano ya NYERERE SUPER CUP 2023 Kwa Mhe Kanali Joseph kolombo Mkuu wa wilaya ya Kibiti Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Tarehe 23.9.2023 na kutamatisha 12.10.2023 yakishirikisha Timu 12 Timu 6 kutoka Kibiti na Timu 6 kutoka Rufiji wadhamini wa mashindano ni NSSf,NBC BANK na TANGANYIKA ORGANIC Kauli mbiu ya mashindano AMANI NA UMOJA VITAWALE MITANO TENA
Saturday, September 9, 2023
NYERERE SUPER CUP TIMU ZAKABIDHIWA VIFAA
MTANZANIA ALICE GYUNDA AOMBA APIGIWE KURA MRS/MISS AFRICA UK 2023
MSHIRIKI wa shindano la Miss/Mrs Africa UK 2023 kutoka Tanania Alice Gyunda amesema kuwa endapo atafanikiwa kushinda taji hilo atajenga studio kwenye baadhi ya shule a msingi a Jijini Dar es Salaam ili kuzalisha vipaji vingi vya waimbaji waweze kuitangaa nchi kupitia muziki.