TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imebaini uwepo wa kamati hewa kwenye baadhi ya miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Wednesday, August 16, 2023
TAKUKURU PWANI YABAINI MIRADI KAMATI HEWA MIRADI YA HALMASHAURI
MKUU WA MKOA WA PWANI ABUBAKAR KUNENGE AZINDUA MPANGO WA UKUSANYAJI MAPATO
WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MBEGU ZILIZOTHIBITISHWA NA WAKALA WA MBEGU (TOSCI)
Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima na jamii kwa ujumla watumie Mbegu zilizothibitishwa ili kuongeza mavuno tija na kipato.
Hayo amesemwa Mkurugezi mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania Patrick Ngwediagi Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mwaka wa fedha 2022/2023 na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 ya taasisi hiyo.
Amesema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 12 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuendelea na uboreshaji wa shughuli za uthibiti na usimamizi wa ubora wa mbegu pamoja na utekelezaji mradi wa kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi ( AFDP) kwa kujenga Maabara ya Mbegu.
Aidha amesema kuwa jukumu kubwa la Taasisi hiyo ni kusimamia shughuli za uzalishaji wa Mbegu na biashara ya Mbegu Ili kuhakikisha wakulima na Wadau wengine kuwa Mbegu wanazouziwa zenye Lebo ya TOSCI ni sahihi kwa matumizi.
Pia amesema kuwa matumizi ya Lebo za ubora za TOSCI kumesababisha kupungua kwa tatizo la uwepo wa Mbegu feki na zilizo na ubora hafifu hapa nchini.
Monday, August 14, 2023
DAWASA KUBORESHA HUDUMA KUPITIA MIRADI SABA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kupitia utekelezaji wa miradi Saba ya kimkakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda, mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha maji wa Rufiji na mradi wa maji Kwala.
Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Mkuu was DAWASA Kiula Kingu Leo Agosti 11,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.
Kingu amesema Miradi iliyotekelezwa imegharimu shilingi bilioni 425.9 inalenga kuongeza wingi wa maji yanayozalishwa na DAWASA, kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji, kuimarisha mfumo wa usambazaji maji na kuimarisha huduma katika maeneo ambayo hayana mtandao hasa ya pembezoni.
Aidha Kingu ameeleza pamoja na kuwekeza nguvu katika utoaji wa huduma za majisafi, DAWASA imejipanga kikamilifu na kuchukua hatua za makusudi za kuboresha usafi wa mazingira kupitia miradi mikubwa na midogo. Hii ni kwa sababu upatikanaji wa maji unapoongezeka unapaswa uambatane na usimamizi madhubuti wa usafi wa mazingira.
Hata hivyo Mradi mwingine ni wa kujenga mfumo wa kukusanya majitaka na maeneo nufaika ambapo katika awamu hii ni Mbezi beach, Kilongamwima, baadhi ya maeneo ya Kawe na Salasala. Utekelezaji wa mradi umeanza na Wakandarasi wanaendelea na shughuli za maandalizi ya ujenzi.
DAWASA pia imekuja na ubunifu wa kujenga mifumo na mitambo midogo midogo ya kuchakata majitaka inayojengwa maeneo ya pembezoni ambapo zaidi ya lita 780,000 za majitaka zitakuwa zikichakatwa kwa siku. Miradi hii itajumuisha ujenzi wa vyoo vya umma 30 ambavyo vitasaidia kuboresha usafi wa mazingira.
Ameeleza kwamba miradi hii itasaidia wananchi kupata huduma za usafi wa mazingira kwa gharama nafuu karibu pia Wakandarasi wanaendelea na ujenzi na gharama za miradi ni jumla ya shilingi bilioni 25.7 na wanufaika wanakadiriwa kufikia milioni 1.8.
Alimalizia kwa kusema Miradi hii ni ya kisasa na mfumo wake wa uchakataji majitaka itatoa gesi asilia kwa ajili ya kupikia, itatoa mbolea itakayoweza kutumika katika kustawisha bustani za miti na majani pia maji yatakayochakatwa yataweza kutumika kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji, usafishaji wa barabara na mitaro ama kupoozea mitambo.
TUME YA MAENDELEO USHIRIKA TANZANIA YAONDOA BODI 55
Tume ya maendeleo ya Ushirika Tanzania imeondoa bodi za vyama vya Ushirika 55 ambazo hazikufuata kanuni na taratibu za Ushirika,na kupeleke masuala 30 polisi na masuala 47 Takukuru kwaajili ya kuyafanyia Kazi.
Hayo yameelezwa na Mrajisi wa vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya maendeleo ya Ushirika Tanzania Dkt Benson Ndiege katika mkutano wake Jijini Dodoma akieleza utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Aidha Dkt Ndiege amesema katika kuhakikisha Maafisa Ushirika wanaweza kubaini na kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili vyama wameamua kutoa mafunzo kwa Maafisa hawa.
Hata hivyo tume hiyo ufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara katika vyama vya Ushirika ikiwa lengo ni kubaini uzingatiwaji wa matakwa ya Sheria kanuni na miongozo mbalimbali inayohusiana na utendaji wa vyama vya Ushirika.
TAASISI YA MWALIMU NYERERE YATOA MISAADA KWA JAMII.
TAASISI ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Chuo cha Afya cha St David cha Jijini Dar es Salaam wametoa misaada ya kadi za bima ya afya ya jamii (CHF) vifaa vya shule na vyakula kwa wanafunzi wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Friday, August 11, 2023
HOSPITALI YA MUHIMBILI KUPANDIKIZA MIMBA
Katika kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi hospital ya Taifa Muhimbili inampango wa kuanzisha huduma za kupandikiza mimba na upandikizaji Figo, uloto na vifaa vya usikivu ambapo wakati wowote kwa Wanawake ambao wana matatizo ya kutopata ujauzito watapata huduma hiyo.
Hayo amesemwa Agosti 10, 2023 Mkurugezi Mtendaji wa hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema kuwa hospital ihiyo imeona iazishe huduma hizo ili kupunguza wingi wa watu wanaokwenda nje ya inchi kwa ajili ya kupata huduma hiyo.
Pia amesema kuwa hospitali hiyo imeanzisha utaratibu wa kulipia huduma ya maegesho ilii isaidie kupunguza msongamano wa magari ndani ya hospitali kutokana na watu kuegesha magari katika maeneo hayo
Katika hatua nyingine amesema kuwa wanatarajia kubomoa Hospitali hiyo na kujenga kubwa zaidi kwaajili ya kuboresha utoaji wa huduma bora za Afya na kuendana na wakati.
Mbali na hayo Hospitali hiyo,katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 imeidhinishiwa na Serikali jumla ya Shilingi Bilioni170.6 ili kutekeleza vipaumbele vyake.









