Monday, May 26, 2014

MATUKIO PWANI

 Na John Gagarini, Kibaha

WATU wawili wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana huko eneo la Bwawani kata ya Ubena Tarafa ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 25 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni katika barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Kamanda Matei alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari T 752 ADE aina ya Toyota Landcruiser likiendeshwa na Anthony Paul (47) raia wa Uingereza ambaye ni mkazi wa Rock Garden mkoani Morogoro akitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro aligongana uso kwa uso na gari namba T 404 CSN aina Forester lililokuwa likiendeshwa na Hizza Semkubo na kusababisha vifo hivyo.

Aliwataja waliokufa kuwa  dereva Semkubo na abiria aitwaye Odino Haule (45) na majeruhi wanne amao ni Happy Michael (21), Jamila Jaffary (21) ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam.

Aidha aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Joseph Mapunda (30) mkazi wa Iringa ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Kamanda Matei alisema kuwa dereva Paul na majeruhi wengine wawili walikimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu, Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba T 404 CSN kuyapita magari mengine bila ya kuchukua tahadhari na miili ya maerehemu imehifadhiwa katika hospitali Teule ya Tumbi.

Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha

WATU 10 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu wakiwemo wanawake watatu waliopatikana na bangi kilogramu 2 ikiwa kwenye mfuko wa plastiki maarufu kama Rambo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kamanda wa polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei amesema kuwa watuhumniwa hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu 19 majira ya saa 09:00 alasiri huko Mkuranga Kata/Tarafa ya Mkuranga Wilaya ya Mkuranga.

Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na  askari waliokuwa doria,  watuhumiwa hao ni Ummy  Mkwachu (32) mkazi wa Mbagala Charambe, Amina Said (23), mkazi wa Mbagala Kiburugwa na Sarah Daud (19), mkazi wa Mbagala Charambe wakiwa na Bhangi yenye uzito wa kg 2 ikiwa imefungwa kwenye mfuko wa nailoni (Rambo), wakisafirisha katika gari lenye namba za usajili T117 BKN aina ya Toyota Hiace wakitokea Dar es Salaam kwenda Kisiju wilayani Rufiji.

Kamanda Matei alisema kuwa kwenye tukio lingine Salum Rashid (43) mkazi wa Ubena Zomozi anashikiliwa kwa tuhuma ya kupatikana na silaha aina ya Gobore bila ya Kibali.

Alibainisha kuwa tukio hilo lilitokea Mei 23 mwaka huu majira ya saa 05:41 asubuhi huko Kijiji cha Ubena kata ya Ubena Tarafa ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo, ambapo askari wakiwa doria walimkamata mtuhumiwa huku sila hiyo ikiwa na risasi moja.

 Katika tukio lingine watu watatu wanshikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kupatikana na Madawa ya kulevya aina ya Mirungi bunda 33 wakiwa ndani ya Basi la kampuni ya Tawfiq lenye namba za usajili T 248 KBT likitoka Tanga Kwenda Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Mei 24mwaka huu majira ya saa 08:15 mchana huko kijiji cha Msoga kata/Tarafa ya Msoga Wilaya ya Bagamoyo.

Watuhumiwa hao walikamatwa na askari waliokuwa doria, ambapo waliwakamata walimkamata Hafidh Siraji, ( 22), mkazi wa Tanga, akiwa na Mirungi bunda 33 sawa na kg 33 ndani ya gari lenye namba za usajili T 248 KBT aina ya Isuzu Bus.

Katika hatua nyingen jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuvua samaki kwa njia haramu ya nyavu ambazo zimepigwa marufuku na serikali.

Alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 25 mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi huko maeneo ya Bondeni Pwani Kata ya Kilindoni Tarafa ya kusini Wilaya ya mafia

Alifafanua kuwa askari wakiwa doria waliwakamata Ussi Juma, (50), mkazi wa Msufini, Ahmad Saleh,(22), mkazi wa Msufini na Ahmad Bakari,(27), mkazi wa Kichangachui wakivua samaki kwa kutumia nyavu haramu.

MWISHO.

Wednesday, May 21, 2014

MKOA WA PWANI WAINGIA MIKATABA NA WAKUU WA WILAYA

Na John Gagarini, Kibaha
MKOA wa Pwani umeingia umeingia mkataba na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na wenyeviti wa halmashauri juu ya utekelezaji wa mpango wa kupunguza vifo vya mama wajawazito watoto wachanga na wale wenye umri chini ya miaka mitano.
Pia mkoa umeingia na viongozi hao kwenye mkataba kwa ajili ya makusanyo ya mapato ambayo waliyapitisha kuwa wana uwezo wa kuyakusanya  kwenye halmashauri za wilaya saba za mkoa huo katika kipindi cha bajeti ya mwaka 2014-2015.
Tukio hilo la kihistoria la kusaini mikataba hiyo ya kazi kwa viongozi hao ndani ya mkoa wa Pwani lilifanyika juzi mjini Kibaha na lilisimamiwa na mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na mwanasheria  wa mkoa Mohamed Magati ambapo viongozi hao endapo watashindwa kufikia malengo yaliyowekwa itawabidi kujieleza.
Wakuu wa wilaya ambao waliingia mikataba hiyo na wilaya zao ni pamoja na Mercy Silla wilaya ya Mkuranga, Fatuma Kimariyo Kisarawe, Nurdin Babu Rufiji, Sauda Mtondoo wilaya ya Mafia, Ahmed Kipozi wilaya ya Bagamoyo  na Halima Kihemba wilaya ya Kibaha.
Akizungumza na watendaji hao kuhusiana na mikata hiyo walioingia na mkoa Mahiza alisema kuwa mikataba hiyo itasaidia uwajibikaji kwa watendaji hao ambao wanawatumikia wananchi katika kuwaletea maendeleo.
“Mikataba hii ni changamoto kwa watendaji wetu hawa na endapo watashindwa kutekeleza majukumu yao kama mkataba unavyoonyesha itabidi wajieleze kwani hata mimi nishaingia mikataba na mamlaka za juu hivyo kila mtu lazima atimize wajibu wake,” alisema Mahiza.
Mahiza alisema kuwa kwa upande wa vifo vya mama wajawazito, watoto wa changa na wale wenye umri chini ya miaka mitano ni tatizo kubwa hivyo mkataba huo utasaidia kupunguza vifo hivyo visivyo vya lazima.
“Kwa upande wa makusanyo kila halmashauri ilileta makadirio yake ya kukusanya mapato kwenye bajeti ya mwaka 2014- 2015 hivyo ni lazima watimize kusudio lao na hakuna sababu ya kusema wameshindwa kuyafikia malengo hayo ya ukusanyaji wa mapato,” alisema Mahiza.
Halmashauri hizo kila moja imejiwekea kiwango chake cha kukusanya kutegemeana na vyanzo vyake vya mapato ambapo Bagamoyo watakusanya bilioni2.6, Kibaha Mjini, bilioni 4.2, Kibaha Vijijini bilioni 2.6, Kisarawe bilioni 3.8, Mafia bilioni 1, Mkuranga bilioni 2.1 na Rufiji bilioni 2.7 ambapo jumla ya makusanyo hayo kwa wilaya zote za mkoa huo itakuwa ni bilioni 8.7
Naye mganga mkuu wa mkoa wa Singida ambaye alishinda tuzo ya Rais ya kupunguza vifo vya makundi hayo Dk Doroth Gwajima alisema kuwa vifo vingi vinatokana na uzembe wa baadhi ya watumishi wasio na maadili ya kazi.
 Dk Gwajima aliwataka wahudumu wa afya kwenye mkoa huo wa Pwani kumtanguliza Mungu wakati wa utendaji wao wa kazi pia kuzingatia maadili ya kazi zao kwani baadhi ya vifo vinatokana na uzembe na si mapenzi ya Mungu. 
Mwisho.

MAHIZA APINGA MFUKO WA WENYEVITI WA HALMASHAURI

Na John Gagarini, Kibaha
MKUU wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza amezuia bajeti ya fedha iliyokuwa inatengwa kwa ajili ya wenyeviti wa halmashauri za wilaya badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
Fedha hizo ambazo zimekuwa zikitengwa kwenye bajeti za kila mwaka za halmashauri bado hazijaonyeshwa kuwa zinatengwa kwa kanuni gani tofauti na fedha nyingine ndani ya halmashauri.
Akizungumza na wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri, maofisa mipango na waweka hazina wa halmashauri za mkoa huo Mahiza alisema kuwa fedha hizo ni nyingi kwani baadhi ya wenyeviti wamekuwa wakitengewa hadi milioni 11 kw akila bajeti.
Mahiza alifikia kutoa agizo hilo baada ya baadhi ya halmashauri kusema kuwa zimetenga fedha hizo kwa ajili ya wenyeviti wa halmashauri kwa ajili ya matumizi ambayo hayakuwekwa bayana.
“Natoa agizo kuwa mfuko huo wa fedha kwa ajili ya mwenyekiti uondolewe hadi mtakapotoa mwongozo wa mfuko kwani mifuko yote ikiwemo ile ya Jimbo ya Mbunge ipo kisheria na inatambulika je huu umewekwa kwa kufuata sheria ipi,” alisema Mahiza.
Alisema kuwa hana nia mbaya juu ya kuzuia mfuko huo lakini anachotaka ni mwongozo ambao unaelekeza kuwepo kwa fedha hizo ambapo wakurugenzi walishindwa kuonyesha ni sheria gani wanayoitumia kutenga fedha hizo.
“Hadi sasa hakuna anayejua fedha hizi zinatengwa kwa kufuata utaratibu au mwongozo upi hivyo naomba ofisa wa serikali za Mitaa anipatie mwongozo ili mfuko uo uendelee na kama hakuna mwongozo wowote basi fedha ziende kwenye miradi ya maendeleo,” alisema Mahiza.
Aidha alisema hata wakuu wa wilaya hawana fedha kama hizo ambapo wao fedha zao hazizidi zaidi ya milioni tano jambo ambalo liliwashitua watu wengi waliposikia kuhusu mfuko huo wa wenyeviti wa halmashauri.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
ILI kuleta ufanisi wa utendaji kazi kwa wauguzi mkoa wa Pwani utawapatia kiasi cha shilingi 1,000 kwa muuguzi atakayezailisha mama wajawazito kwa usalama.
Pia vituo vya afya na zahanati zinatakiwa kufanya kazi kwa saa 24 ili kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu kwa muda wote tofauti na ili sasa ambapo wahudumu wa afya wanafunga muda wa kazi saa 9:30.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza wakati wa kikao cha kazi ambacho kiliambatana na uingiwaji wa mikataba baina ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo juu ya utendaji kazi kwenye sekta ya afya na makusanyo kwenye bajeti ya mwaka 2014- 2015.
Mahiza alisema kuwa mpango wa kuwapa fedha wauguzi wanaowazalisha mama wajawazito salama ni kuwapa hamasa ili waweze kufanya vizuri katika kuwahudumia akinamama hao.
“Kwa kuwa tayari tumeshaingia mkataba na wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya miaka mitano lazima tuwape motisha watendaji wa sekta ya afya ili wafanye kazi kwa moyo,” alisema Mahiza.
Aidha Mahiza alisema kuwa kuanzia sasa vituo vya afya na zahanati vifanye kazi kwa saa 24 ili kuweza kufikia malengo ya kupunguza vifo hivyo pamoja na utoaji huduma kwa muda wote kwani ugonjwa hauna saa.

WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KULIMA BANGI HEKARI 2

 Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia wakazi wawili wa Kijiji
cha Mwetemo wilaya ya Bagamoyo mkoani humo kwa tuhuma za kulima shamba
la bangi hekari mbili kwenye shamba la mahindi.

Watuhumiwa hao walibainika baada ya askari wa jeshi hilo kufanya doria
ya kusaka makosa mbalimbali wilyani humo ili kukamata wahalifu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana mjini Kibaha kamanda wa
polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi (SACP)
Ulrich Matei alisema kuwa msako huo ni wa kawaida.

Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 19 mwaka huu
majira ya saa 9 alasiri huko kijiji cha Mwetemo- Kiwangwa Tarafa ya
Msata wilayani humo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Musa Zahoro (20) na Asher Mbuya (29)
ambapo watuhumiwa hao watafikishw amahakamani mara upelelezi
utakapokamilika.

Kwenye tukio lingine Jeshi hilo linamshikilia Omary Sultan (32)
mkulima wa mkazi wa Kijiji cha Kauzeni wilaya ya Kisarawe kwa tuhuma
za kupatikana na pombe ya Moshi lita 12 na mtambo wa kutengenezea
pombe hiyo.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 19 majira ya saa 6:00 Kijijini
hapo na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara uchunguzi wa
tukio hilo utakapokamilika.

Mwisho.

MFUKO WA MWENYEKITI WAKATALIWA

Na John Gagarini, Kibaha
MKOA wa Pwani umeingia umeingia mkataba na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na wenyeviti wa halmashauri juu ya utekelezaji wa mpango wa kupunguza vifo vya mama wajawazito watoto wachanga na wale wenye umri chini ya miaka mitano.
Pia mkoa umeingia na viongozi hao kwenye mkataba kwa ajili ya makusanyo ya mapato ambayo waliyapitisha kuwa wana uwezo wa kuyakusanya  kwenye halmashauri za wilaya saba za mkoa huo katika kipindi cha bajeti ya mwaka 2014-2015.
Tukio hilo la kihistoria la kusaini mikataba hiyo ya kazi kwa viongozi hao ndani ya mkoa wa Pwani lilifanyika juzi mjini Kibaha na lilisimamiwa na mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na mwanasheria  wa mkoa Mohamed Magati ambapo viongozi hao endapo watashindwa kufikia malengo yaliyowekwa itawabidi kujieleza.
Wakuu wa wilaya ambao waliingia mikataba hiyo na wilaya zao ni pamoja na Mercy Silla wilaya ya Mkuranga, Fatuma Kimariyo Kisarawe, Nurdin Babu Rufiji, Sauda Mtondoo wilaya ya Mafia, Ahmed Kipozi wilaya ya Bagamoyo  na Halima Kihemba wilaya ya Kibaha.
Akizungumza na watendaji hao kuhusiana na mikata hiyo walioingia na mkoa Mahiza alisema kuwa mikataba hiyo itasaidia uwajibikaji kwa watendaji hao ambao wanawatumikia wananchi katika kuwaletea maendeleo.
“Mikataba hii ni changamoto kwa watendaji wetu hawa na endapo watashindwa kutekeleza majukumu yao kama mkataba unavyoonyesha itabidi wajieleze kwani hata mimi nishaingia mikataba na mamlaka za juu hivyo kila mtu lazima atimize wajibu wake,” alisema Mahiza.
Mahiza alisema kuwa kwa upande wa vifo vya mama wajawazito, watoto wa changa na wale wenye umri chini ya miaka mitano ni tatizo kubwa hivyo mkataba huo utasaidia kupunguza vifo hivyo visivyo vya lazima.
“Kwa upande wa makusanyo kila halmashauri ilileta makadirio yake ya kukusanya mapato kwenye bajeti ya mwaka 2014- 2015 hivyo ni lazima watimize kusudio lao na hakuna sababu ya kusema wameshindwa kuyafikia malengo hayo ya ukusanyaji wa mapato,” alisema Mahiza.
Halmashauri hizo kila moja imejiwekea kiwango chake cha kukusanya kutegemeana na vyanzo vyake vya mapato ambapo Bagamoyo watakusanya bilioni2.6, Kibaha Mjini, bilioni 4.2, Kibaha Vijijini bilioni 2.6, Kisarawe bilioni 3.8, Mafia bilioni 1, Mkuranga bilioni 2.1 na Rufiji bilioni 2.7 ambapo jumla ya makusanyo hayo kwa wilaya zote za mkoa huo itakuwa ni bilioni 8.7
Naye mganga mkuu wa mkoa wa Singida ambaye alishinda tuzo ya Rais ya kupunguza vifo vya makundi hayo Dk Doroth Gwajima alisema kuwa vifo vingi vinatokana na uzembe wa baadhi ya watumishi wasio na maadili ya kazi.
 Dk Gwajima aliwataka wahudumu wa afya kwenye mkoa huo wa Pwani kumtanguliza Mungu wakati wa utendaji wao wa kazi pia kuzingatia maadili ya kazi zao kwani baadhi ya vifo vinatokana na uzembe na si mapenzi ya Mungu. 
Mwisho.

Thursday, May 15, 2014

WACHEZAJI WAMIMINIKA RUVU SHOOTING KUOMBA USAJILI

Na John Gagarini, Kibaha
JUMLA ya wachezaji 251 wamejitokeza kufanya majaribio kwenye kikosi cha Ruvu Shooting ya Wilayani Kibaha mkoani Pwani ili kusajiliwa na timu hiyo waweze kupata nafasi kwenye timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Voda Com.
Akizungumza na wachezaji hao kwenye uwanja wa Ruvu Kocha Mkuu Tom Olaba alisema kuwa lengo la kutangaza nafasi hiyo ya kuwaita  wachezaji ni kuwapatia fursa chipukizi wenye uwezo wa kusakata soka ili waweze kutoa mchango wao kwenye kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi Kuu ya msimu ujao.
Olaba alisema kuwa wamewaita  wachezaji hao kufanya majaribio ili wataofanikiwa majaribio hayo waweze kupata nafasi ya kukitumikia kikosi chetu ya Ruvu Shooting tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao unaotaraji kuanza kutimua vumbi mwezi wa 8 mwaka huu, hivyo wanapaswa kuonesha uwezo na watakaofaulu watapata nafasi bila ya upendeleo.
“Mazoezi haya yataendelea kwa wiki mbili ambayo yatakuwa yanachezwa kwa mtindo wa bonanza ikiwa na lengo la kuwapatia nafasi nzuri zaidi wachezaji kuonesha uwezo wao wa kucheza soka na hatimye wapatikane wachezaji wenye vipaji,” alisema Olaba.
Naye Mkuu wa Kikosi cha Ruvu kilichopo kikosi hicho Luteni Kanali Charles Mbuge alisema kuwa uongozi huo bado unaendelea kuwataka vijana zaidi wajitokeze kwani lengo ni kuhakikisha wanapata wachezaji wenye uwezo watakaosajiliwa kwa
ajili ya Ligi Kuu na wale wenye chini ya umri wa miaka 20.

"Lengo kubwa ni kuhakikisha tunapata wachezaji ambao wataisaidia timu ili iweze kufanya vyema kwenye ligi ijayo pamoja na kuwaandaa vijana wengine watakaoitumikia timu miaka ya baadaye kwenyeligi zijazo," alisema Luteni Mbuge.
Kanali Mbuge.

Aidha Luteni Mbunge alitoa shukrani kwa jopo la makocha mbali ya Olaba na msaidizi wake Seleman Mtungwe ambao wamejipanga vizuri katika kuhakikisha zoezi hilo linakwenda kama lilivyopangwa na hatimaye kupatikana kwa wachezaji bora zaidi watakaoongezea ushindani katika kikosi hicho kwenye kinyang'anyiro kijacho.

MWISHO

MLINZI ANYONGWA

Na John Gagarini, Kibaha
MLINZI Bakari Mape (70) mkazi wa Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani ameuwawa kwa kunyongwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walimwua mlinzi huyo kwa kumvunja shingo kisha kuiba kwenye duka ambalo mlinzi huyo alikuwa akililinda.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu majira ya saa 8 usiku eneo la sokoni Mlandizi wilayani hapa.
Kamanda Matei alisema kuwa watu hao baada ya kumwua marehemu ambaye alikuwa akilinda duka la Conrad Masawe (53) mkazi wa Mtongani Mlandizi, waliiba kiasi cha shilingi milioni 5.2.
"Walipomwua walingoa bati kisha kuingia ndani na kuiba fedha hizo na kutoweka kusikofahamika huku wakimwacha marehemu hapo," alisema Kamanda Matei.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Omary Rajabu kuhusiana na suala hilo.
"Mwili wa marehemu ulikabidhiw andugu kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktari na tutawasaka watu walihusika na tukio hilo ili mkondo wa sheria uweze kuchukua hatua kwani kitendo hicho ni ukatili ndani ya jamii," alisema Kamanda Matei.
Aidha aliwataka wafanyabiashara waajiri watu weny umri wa kati ili waweze kukabiliana na matukio kama hayo na kuacha kuajiri watu wenye umri mkubwa sana kwani ni vigumu kukabiliana na matukio kama hayo.
mwisho.