Na John Gagarini, Kibaha
MLINZI Bakari Mape (70) mkazi wa Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani
ameuwawa kwa kunyongwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walimwua mlinzi
huyo kwa kumvunja shingo kisha kuiba kwenye duka ambalo mlinzi huyo alikuwa
akililinda.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna
Mwandamizi Msaidizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei
14 mwaka huu majira ya saa 8 usiku eneo la sokoni Mlandizi wilayani hapa.
Kamanda Matei alisema kuwa watu hao baada ya kumwua marehemu ambaye alikuwa
akilinda duka la Conrad Masawe (53) mkazi wa Mtongani Mlandizi, waliiba kiasi
cha shilingi milioni 5.2.
"Walipomwua walingoa bati kisha kuingia ndani na kuiba fedha hizo na
kutoweka kusikofahamika huku wakimwacha marehemu hapo," alisema Kamanda
Matei.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Omary
Rajabu kuhusiana na suala hilo.
"Mwili wa marehemu ulikabidhiw andugu kwa ajili ya mazishi baada ya
uchunguzi wa daktari na tutawasaka watu walihusika na tukio hilo ili mkondo wa
sheria uweze kuchukua hatua kwani kitendo hicho ni ukatili ndani ya
jamii," alisema Kamanda Matei.
Aidha aliwataka wafanyabiashara waajiri watu weny umri wa kati ili waweze
kukabiliana na matukio kama hayo na kuacha kuajiri watu wenye umri mkubwa sana
kwani ni vigumu kukabiliana na matukio kama hayo.
mwisho.
No comments:
Post a Comment