Thursday, May 15, 2014

WACHEZAJI WAMIMINIKA RUVU SHOOTING KUOMBA USAJILI



Na John Gagarini, Kibaha
JUMLA ya wachezaji 251 wamejitokeza kufanya majaribio kwenye kikosi cha Ruvu Shooting ya Wilayani Kibaha mkoani Pwani ili kusajiliwa na timu hiyo waweze kupata nafasi kwenye timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Voda Com.
Akizungumza na wachezaji hao kwenye uwanja wa Ruvu Kocha Mkuu Tom Olaba alisema kuwa lengo la kutangaza nafasi hiyo ya kuwaita  wachezaji ni kuwapatia fursa chipukizi wenye uwezo wa kusakata soka ili waweze kutoa mchango wao kwenye kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi Kuu ya msimu ujao.
Olaba alisema kuwa wamewaita  wachezaji hao kufanya majaribio ili wataofanikiwa majaribio hayo waweze kupata nafasi ya kukitumikia kikosi chetu ya Ruvu Shooting tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao unaotaraji kuanza kutimua vumbi mwezi wa 8 mwaka huu, hivyo wanapaswa kuonesha uwezo na watakaofaulu watapata nafasi bila ya upendeleo.
“Mazoezi haya yataendelea kwa wiki mbili ambayo yatakuwa yanachezwa kwa mtindo wa bonanza ikiwa na lengo la kuwapatia nafasi nzuri zaidi wachezaji kuonesha uwezo wao wa kucheza soka na hatimye wapatikane wachezaji wenye vipaji,” alisema Olaba.
Naye Mkuu wa Kikosi cha Ruvu kilichopo kikosi hicho Luteni Kanali Charles Mbuge alisema kuwa uongozi huo bado unaendelea kuwataka vijana zaidi wajitokeze kwani lengo ni kuhakikisha wanapata wachezaji wenye uwezo watakaosajiliwa kwa
ajili ya Ligi Kuu na wale wenye chini ya umri wa miaka 20.

"Lengo kubwa ni kuhakikisha tunapata wachezaji ambao wataisaidia timu ili iweze kufanya vyema kwenye ligi ijayo pamoja na kuwaandaa vijana wengine watakaoitumikia timu miaka ya baadaye kwenyeligi zijazo," alisema Luteni Mbuge.
Kanali Mbuge.

Aidha Luteni Mbunge alitoa shukrani kwa jopo la makocha mbali ya Olaba na msaidizi wake Seleman Mtungwe ambao wamejipanga vizuri katika kuhakikisha zoezi hilo linakwenda kama lilivyopangwa na hatimaye kupatikana kwa wachezaji bora zaidi watakaoongezea ushindani katika kikosi hicho kwenye kinyang'anyiro kijacho.

MWISHO

No comments:

Post a Comment