Na John
Gagarini, Kibaha
WATU wawili wamefariki dunia na wengine wanne
wamejeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana huko eneo la
Bwawani kata ya Ubena Tarafa ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Pwani
Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo
lilitokea Mei 25 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni katika barabara kuu ya Dar
es Salaam – Morogoro.
Kamanda Matei alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha
gari T 752 ADE aina ya Toyota Landcruiser likiendeshwa na Anthony Paul (47)
raia wa Uingereza ambaye ni mkazi wa Rock Garden mkoani Morogoro akitokea Dar
es Salaam kwenda Morogoro aligongana uso kwa uso na gari namba T 404 CSN aina
Forester lililokuwa likiendeshwa na Hizza Semkubo na kusababisha vifo hivyo.
Aliwataja waliokufa kuwa dereva Semkubo na
abiria aitwaye Odino Haule (45) na majeruhi wanne amao ni Happy Michael (21),
Jamila Jaffary (21) ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar
es Salaam.
Aidha aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Joseph
Mapunda (30) mkazi wa Iringa ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili Dar es Salaam kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Kamanda Matei alisema kuwa dereva Paul na majeruhi
wengine wawili walikimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu, Chanzo
cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba T 404 CSN kuyapita magari
mengine bila ya kuchukua tahadhari na miili ya maerehemu imehifadhiwa katika
hospitali Teule ya Tumbi.
Na John Gagarini, Kibaha
WATU 10 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani
Pwani kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu wakiwemo wanawake watatu waliopatikana
na bangi kilogramu 2 ikiwa kwenye mfuko wa plastiki maarufu kama Rambo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
mjini Kibaha kamanda wa polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP)
Ulrich Matei amesema kuwa watuhumniwa hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu 19
majira ya saa 09:00 alasiri huko Mkuranga Kata/Tarafa ya Mkuranga Wilaya ya
Mkuranga.
Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa na askari waliokuwa doria, watuhumiwa hao ni Ummy Mkwachu (32) mkazi wa Mbagala Charambe, Amina
Said (23), mkazi wa Mbagala Kiburugwa na Sarah Daud (19), mkazi wa Mbagala
Charambe wakiwa na Bhangi yenye uzito wa kg 2 ikiwa imefungwa kwenye mfuko wa
nailoni (Rambo), wakisafirisha katika gari lenye namba za usajili T117 BKN aina
ya Toyota Hiace wakitokea Dar es Salaam kwenda Kisiju wilayani Rufiji.
Kamanda Matei alisema kuwa kwenye tukio lingine Salum
Rashid (43) mkazi wa Ubena Zomozi anashikiliwa kwa tuhuma ya kupatikana na
silaha aina ya Gobore bila ya Kibali.
Alibainisha kuwa tukio hilo lilitokea Mei 23 mwaka
huu majira ya saa 05:41 asubuhi huko Kijiji cha Ubena kata ya Ubena Tarafa ya
Chalinze Wilaya ya Bagamoyo, ambapo askari wakiwa doria walimkamata mtuhumiwa
huku sila hiyo ikiwa na risasi moja.
Katika tukio lingine watu watatu wanshikiliwa na
jeshi hilo kwa tuhuma za kupatikana na Madawa ya kulevya aina ya Mirungi bunda
33 wakiwa ndani ya Basi la kampuni ya Tawfiq lenye namba za usajili T 248 KBT
likitoka Tanga Kwenda Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Mei 24mwaka huu majira ya saa 08:15 mchana huko kijiji
cha Msoga kata/Tarafa ya Msoga Wilaya ya Bagamoyo.
Watuhumiwa hao walikamatwa na askari waliokuwa doria,
ambapo waliwakamata walimkamata Hafidh Siraji, ( 22), mkazi wa Tanga, akiwa na
Mirungi bunda 33 sawa na kg 33 ndani ya gari lenye namba za usajili T 248 KBT
aina ya Isuzu Bus.
Katika hatua nyingen jeshi hilo linawashikilia watu
watatu kwa tuhuma za kuvua samaki kwa njia haramu ya nyavu ambazo zimepigwa
marufuku na serikali.
Alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 25 mwaka huu
majira ya saa 1:30 asubuhi huko maeneo ya Bondeni Pwani Kata ya Kilindoni Tarafa
ya kusini Wilaya ya mafia
Alifafanua kuwa askari wakiwa doria waliwakamata
Ussi Juma, (50), mkazi wa Msufini, Ahmad Saleh,(22), mkazi wa Msufini na Ahmad
Bakari,(27), mkazi wa Kichangachui wakivua samaki kwa kutumia nyavu haramu.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment