Na John Gagarini,
Bagamoyo
HUKU uchaguzi wa
Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ukiwa umefanyika juzi na matokeo
yakiendelea kutoka wananchi 514 wa Kijiji cha Mwetemo Jimbo la Chalinze wilayani
Bagamoyo wameshindwa kupiga kura kutokana na uhaba wa karatasi za kupigia kura.
Uchaguzi huo
ulishindwa kufanyika kutokana na karatasi za kupigia kura kuwa chache hivyo
watu wengine kushindwa kupiga kura ambapo watafanya uchaguzi huo Desemba 19.
Akizungumza na
waandishi wa habari waliotembelea kitongoji hicho kuangalia zoezi hilo la
upigaji kura wa kuchagua viongozi akiwemo mwenyekiti na wajumbe watano
msimamizi msaidizi wa uchaguzi Thomas Madega alisema kuwa wamekubaliana
uchaguzi huo kufanyika siku hiyo.
“Karatasi za kupigia
kura kwanza zilichelewa kwani zilifika kituoni saa 10 kasoro jioni na pia zilikuwa
chache hivyo watu wachache walipiga kura na wengine walishindwa kupiga kabisa,”
alisema Madega.
Madega alisema kuwa
walikaa na viongozi wa vyama vyote na kukubaliana kusogezwa mbele zoezi la
upigaji kura.
“Tumekubaliana na
vyama vyote kusogeza uchaguzi huo hadi Ijumaa na wamekubali tumewaambia
wawatangazie wafuasi wao juu ya hili,” alisema Madega.
Juu ya kuahirisha kwa
muda mrefu tofauti na maeneo mengine ambayo yalikuwa na matatizo na uchaguzi
kufanyika jana alisema kuwa wametoa muda mrefu ili waandaliwe vifaa vya upigaji
kura kwa uhakika.
Kwa upande wake mbunge
wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa muda huo ni mrefu sana kwani
maeneo mengine yalifanya uchaguzi kesho yake.
“Nadhani suala la siku
ya kupiga kura lirudishwe nyuma kwani Ijumaa ni mbali sana hivyo kuna haja ya wahusika
kuliangalia hilo ili wasipishane na wengine,” alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alishauri zoezi
la namna ya kupiga kura washirikishwe zaidi wananchi kwani wale wanaowachagua
ni viongozi wao hivyo wao ndiyo wenye nafasi kubwa ya kushauri na si viongozi
wa vyama vya siasa.
Baadhi ya vijiji na
vitongoji ambavyo vilifanya uchaguzi wao jana Jumatatu badala ya Jumapili ni
Kijiji cha Changarikwa, Vitongoji vya Kwamkula, Mkambala A na B, Kwaluguru A na
B, Pugwe, Migola na Kwadivumo kwenye kata ya Mbwewe.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Ibrahim Matovu alipoulizwa juu ya baadhi ya
maeneo kushindwa kupiga kura alisema kuwa bado hajapata takwimu sahihi ndiyo
anafuatilia kujua changamoto hizo.
Uchuguzi mdogo
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi ulibaini zoezi la upigaji kura ulikumbwa
na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa vifaa vya upigaji kura kama vile
upungufu wa karatasi, picha za wagombea kuwekwa kwenye nembo ya chama
kisichohusika na kukosekana kwa fomu za
wagombea wa nafasi ya ujumbe.
Picha no 3942 msimamizi msaidizi wa kituo cha kupigia kura Kitongoji cha Mkwajuni kwenye Kijiji cha Miono wilaya ya Bagamoyo Faustina Oforo akisubiria wapiga kura wa uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa. |
Picha no 3940
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kitongoji cha Msikitini kwenye Kijiji cha Mbwewe
wilaya ya Bagamoyo Said Mlinde kulia akiongea na Mbunge wa Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete kushoto alipotembela kituo hicho kushuhudia zoezi la upigaji kura.
No comments:
Post a Comment