Na John Gagarini, Kibaha
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani
Pwani kimeonyesha kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa,
Vitongoji na Vijiji ambapo kwenye matokeo ya awali kimeonekana kushinda maeneo
mengi.
Katika Jimbo la Mafia CCM ilishinda
vitongoji 96 kati ya 136
sawa na asilimia 70 Chama Cha Wananchi CUF asilimia 40 sawa na asilimia
29,katika vijiji CCM
ilishinda vijiji 19 kati ya 23 sawa na asilimia 82.6 CUF vijiji 4 sawa na
asilimia 17.3.
Katika Jimbo la Kibaha Mjini kati ya mitaa iliyopo 73 ,CCM imeshinda
mitaa 62 sawa na asilimia 84.9, huku wapinzani wao Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) wakishinda kwenye mitaa 10 sawa na asimilia 13.7.
Katika Jimbo Kibaha Vijijini
kwenye Vijini 32 CCM ilishinda mitaa 31 , ambapo kwenye mitaa 10 ilishinda bila
kupingwa sawa na asimilia 96.9 ,upinzani ilishinda kijiji kimoja sawa na
asimilia 13.1, kati ya vitongoji 106 CCM ilishinda vitongoji 98 sawa na
asilimia 92.5,upinzani vitongoji 4 sawa na asilimia 3.8.
Katika Wilaya ya Bagamoyo vijiji vilivyopo ni 75 CCM ilishinda
vijiji 67 sawa na asilimia 90.5 na vijiji 8 havijafanya uchaguzi, kati ya vitongoji 610 CCM ilishinda 540 sawa na
asilimia 88.5 na vitongoji 45 havijafanya uchaguzi ambapo wapinzani walishinda vitongoji sawa na asilimia 4.1.
Wilaya ya Bagamoyo haijafanya uchaguzi katika vijiji 8 na
vitongoji 45 kutokana na uhaba wa vifaa ikiwemo katasi husika za viti maalum na
kuchanga majina ya wananchi na nembo za vyama vya siasa.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo
Ibrahim Matovu alithibitisha kutokea kwa mabadiliko ya uchaguzi katika maeneo
hayo ambapo alisema uchaguzi huo baadhi ya maeneo ulifanyika jana na kwingine
utafanyika leo desemba 16.
Mwisho
No comments:
Post a Comment