Na John Gagarini,
Kibaha
HUKU leo ikiwa ndiyo siku
ya kwanza ya mwaka mpya wa 2015 ikiwa imeanza fundi wa kuchomelea Michael Mpondo
(36) mkazi wa Machinjioni wilayani Kibaha mkoani Pwani ameamua kukatisha uhai
kwa kujinyonga.
Imeelezwa kuwa chanzo
cha fundi huyo kuamua kuchukua maamuzi hayo magumu ya kuamua kujiua kunatokana
na kuugua kwa muda mrefu.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi mjini Kibaha mwenyekiti wa mtaa wa Machinjioni Evarist
Kamugisha alisema kuwa marehemu alijinyonga jirani na nyumba laiyokuwa akiishi.
Akielezea kwa kina
tukio hilo Kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 30 mwaka huu
majaira ya saa 4:30 asubuhi baada ya mwili wake kukutwa ukininginia kwenye mti umbali
wa mita 60 na alipokuwa akiishi.
“Marehemu usiku wa majira
ya saa 2:30 kabla ya kifo chake alikula chakula na ndugu zake lakini aliondoka
na jitihada za kumtafuta zilifanyika bila ya mafanikio lakini asubuhi yake
ndipo watu walipouona mwili wake ukinginginia,” alisema Kamugisha.
Kamugisha alisema kuwa
marahemu alikuwa akiumwa ambapo baada ya chumba chake kupelkuliwa kulikutwa
dawa aina ya Panadoli pamoja na Amoxilini ambazo inasemekana alikuwa
akizitumia.
“Marehemu alijinyonga
kwa kutumia kamba ya nguo ya jeshi ambayo aliikata na kuwa kama kamba na
kujinyonga nayo na hakuacha ujumbe wowote juu ya kifo chake,” alisema
Kamugisha.
Kwa upande wake
kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alithibitisha kutokea tukio hilo na
kusema kuwa chanzo cha kifo hicho ni marehemu kuugua muda mrefu na kukata tamaa
ya maisha.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment