Na John Gagarini,
Kibaha
JESHI la Polisi mkoani
Pwani linawashikilia watu wawili wakazi wa mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kupatikana
na magunia 12 ya Bangi.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kamanda wa Polisi mkoani humo
Ulrich Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na askari waliokuwa doria.
Kamanda Matei alisema
kuwa tukio hilo lilitokea huko Desemba 2 mwaka huu majira ya 4.40 usiku kwenye
pori la Vikawe kata Pangani wilaya ya Kibaha.
Aliwataja watuhumiwa
hao kuwa ni Sabas Petro (25) na Emily Magomba (21) ambao walikamatwa na askari
waliokuwa doria.
“Watuhumiwa walikutwa
wakishusha magunia hayo kwenye pori hilo kwa lengo la kuyaficha kutoka kwenye
gari namba T 773 ELB,” alisema Kamanda Matei.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment