Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani limewataka
wananchi kutumia vikundi vya ulinzi shirikishi ili kukabiliana na uhalifu
katika kipindi hichi cha sikukuu za X-Mass na mwaka mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake mjini Kibaha, kamanda wa Polisi mkoani hapa Ulrich Matei alisema
kuwa wamejipanga vyema kudhibiti vitendo viovu kwa kushirikiana na wananchi.
Matei alisema kuwa katika kukabiliana
na matukio ya uhalifu kipindi cha sikukuu kwa kutumia ulinzi shirikishi, ulinzi
jirani na mgambo.
“Tutashirikiana na wananchi katika ulinzi
ili washerehekee kwa amani na utulivu na tutakaowabaini wanaofanya matukio ya
uhalifu,” alisema Matei.
Alisema kuwa katika ulinzi jirani
wananchi wanatakiwa kuacha tabia ya kuondoka nyumbani bila ya kuacha mtu au
hata kama wanatoka wawajulishe majirani zao.
“Baadhi ya vitendo viovu vinavyofanyika
ni pamoja na uchomaji matairi ni kinyume cha sheria na hairuhusiwi kufanya
hivyo,” alisema Matei.
Aidha alisema kuwa wazazi wanapaswa
kutowaacha watoto wao kwenda kwenye maeneo ya starehe peke yao kwani ni hatari.
Aliwataka madereva kuhakikisha
wanaendesha magari wakiwa hawajalewa ili kuepukana na ajali pia watawapima
ulevi madereva hao kwani vifaa vya kupimia sasa wanavyo vya kutosha.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment