Na
John Gagarini, Kibaha
WATU
watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamekamatwa wakiwa na silaha aina ya
Short Gun yenye namba 07019302 ikiwa na risasi nane.
Hayo
yamesemwa na kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alipoongea na
waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Mohamed Kalipa (20) dereva wa Bajaji mkazi wa Mbagala
Rangi Tatu, Salum Shekivui (20) mkazi wa Buza na Seuli Lucas (18) makazi wa
Mbagala Rangi Tatu Jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 20 mwaka huu majira ya saa
2:30 huko Mlandizi wilaya ya Kibaha.
“Mbali
ya silaha pia walikutwa na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 6,611,800,
vocha mbalimbali za simu zenye thamani ya shilingi milioni 2,185,500 na simu za
mkononi sita za aina mbalimbali ambazo thamani yake bado hazijafahamika,”
alisema Kamanda Matei.
Aaidha
alisema kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walifanya tukio la unyanganyi wa
kutumia silaha huko Kijiji cha Mbwewe wilaya ya Bagamoyo kwenye duka la Twaha
Mbuta siku ya Oktoba 19 saa 1:30 usiku na kupora kiasi cha shilingi milioni
30,000,000.
“Baada ya kukamatwa walimtaja mtuhumiwa
mwenzao ambaye walikuwa wakishirikiana
naye Samwel Joseph mkazi wa Kongowe Kibaha ambapo baada ya upekuzi walimkuta na
risasi sita za Short Gun ambazo alikuwa akizimiliki bila ya kibali hata hivyo
mtuhumiwa huyo alitoroka,” alisema Kamanda Matei.
Katika tukio lingine watu wawili
walikamatwa kwa tuhuma za wizi wa ngombe 61 wenye thamani ya shilingi milioni
27,450 ,000 mali ya Keke Furaha (37) kwa kutumia silaha aina ya sime.
Alibainisha kuwa tukio hilo limetokea
Oktoba Mosi mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi huko Lulenge kata ya Ubena
wilayani Bagamoyo ambapo watuhumiwa ni Sadala Lupoto (25) mkazi wa Kimamba
Kilosa na Luseky Sogoyo (25) na juhudi za kuwatafuta ngombe wengine 39
zinaendelea.
Katika tukio lingine watu wawili
wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya gobore bila ya
kibali huku wengine 11 walikamatwa
kwenye matukio ya kukutwa na bangi gunia mbili na kete 250 pamoja na lizla
zipatazo 100.
Mwisho.
 |
No comments:
Post a Comment