Na John Gagarini, Kibaha
BAADHI ya wadau wa watoto wilayani Kibaha mkoani Pwani
wameiomba serikali kuyafutia usajili mabanda ya video ambayo yamekuwa chanzo kikuu
cha watoto wadogo kufanyiwa vitendo vya ubakaji.
Mabanda hayo yamekuwa yakitumiwa na baadhi ya watu wazima
ambao wanawafanyia watoto hao vitendo hivyo baada ya kuwarubuni kuwaingiza
kwenye mabanda hayo kisha kuwapakata na kuwaingilia watoto hao ikiwa ni pamoja
na kinyume cha maumbile.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na mratibu wa shirika lisilo la
kiserikali la (KICODET) Dk Rose Mkonyi wakati wa mafunzo ya kupinga vitendo vya
ukatili kwa watoto kwa wadau mbalimbali kwenye kata ya Kibaha wilayani
humo alisema moja ya vyanzo vya ongezeko
la vitendo vya ubakaji watoto ni mabanda hayo.
“Vitendo vya ubakaji watoto ambapo ni moja ya ukatili vimekithiri
na kuongezeka wilayani Kibaha na moja ya sababu ni mabanda hayo ambayo
yanaonyesha video chafu za ngono bila ya kujali umri,” alisema Dk Mkonyi.
Dk Mkonyi alisema kuwa mabanda hayo yamejaa kwenye mitaa na
vijiji hayajali umri licha ya sheria kutaka watoto wenye umri chini ya miaka 18
kutoingia lakini wamiliki wamekuwa wakiwaruhusu watoto hao ambao ni wanafunzi kuingia
pia kufunguliwa muda wa kazi ambapo wanafunzi hao wamekuwa wakiishia humo na
kuacha kwenda shule.
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Faustina Kayombo ambaye
ni ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha alisema kuwa tatizo
kubwa ni usiri unaofanywa na umaskini imekuwa ni chanzo kikuu cha kuendela kwa
vitendo hivyo.
Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni mwenyekiti
wa mafunzo hayo Alkhas Katopola alisema kuwa mafunzo hayo yamtawafanya waweze
kujua namna ya kukabilina na vitendo hivyo ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na
kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria.
Katopolo alisema kuwa baadhi ya matukio hayo yamekuwa
yakiendelea kutokana na wanafamilia kuficha kuogopa mahusiano mabaya au
kurubunia kwa kupewa fedha ili wasitoe taarifa za vitendo hivyo.
Mradi huo ni wa miaka miwili ambapo mafunzo hayo
yamefadhiliwa na Plan International, UNICEF, Save the Children na Jumuiya ya
Ulaya na serikali kwa kushirikiana na shirika hilo la KICODET.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment