Wednesday, April 30, 2025
MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KIBAHA MJINI YATAKIWA KUSHIRIKIANA
Saturday, April 19, 2025
BALOZI MATINYI AAHIDI KUITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA
BALOZI wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, amesema kuwa atatumia uzoefu alioupata katika kazi yake ya uandishi wa habari kutafuta taarifa na kung'amua mbinu za kuvutia watalii wengi kama ilivyo katika nchi hiyo ambayo inavutiwa na kutembelewa na watalii wengi.
"Nitakapofika katika nchi hizo tisa katika eneo langu la uwakilishi nitahakikisha ninatafuta na kujua ni mbinu gani wanazotumia kuvutia watalii kwani watalii wengi duniani huenda kwenye nchi hizo", alisema Mhe. Balozi Matinyi.
Alisema pia kuwa kwa kutumia uzoefu wake katika uandishi wa habari - fani ambayo hujenga tabia ya udadisi na mbinu za kutafuta taarifa za uwekezaji na pia tabia kulikamilisha jukumu la kazi baada ya kulichukua.
Balozi Matinyi alisema hayo hivi karibuni katika mahojinao maalumu na kituo cha televisheni cha ZBC cha Zanzibar.
Alifafanua kwa kueleza kuwa diplomasia ya uchumi nchini ilianzishwa katika utawala wa awamu ya tatu ambapo ili kuujenga uchumi wetu baada ya kumaliza kuzisaidia nchi zingine za Afrika kupata uhuru.
"Hii ndiyo sababu viongozi wetu wakuu wanatusisitizia kwamba tunapokwenda nje ya nchi tukaifanyie kazi diplomasia ya uchumi," alidokeza Mhe. Balozi Matinyi.
"Nitakapofika katika nchi hizo tisa zilizoendelea kiuchumi, katika sekta ya uvuvi, kilimo katika viwanda vya mbolea na matrekta, utalii ambapo wanapokea watalii kati ya milioni 6 hadi 7 kwa mwaka wakitumia visiwa vingi na bahari kuvutia watalii, jukumu langu litakuwa kuhakikisha tunapata mbinu zao na Watanzania tunasonga mbele kiuchumi" alisema Mhe. Balozi Matinyi.
Aidha, akizungumzia namna atakakavyoiwakilisha Zanzibar, alisema kuwa tayari ameshapata maelezo mbalimbali kutoka taasisi za uwekezaji, kama za uchumi wa buluu na utalii na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kujua namna ya kuielezea Zanzibar.
"Tuna nchi tisa katika eneo ninalokwenda wenye tabia ya kutaka kufahamu vyakula vya watu wengine; hivyo, nitawaeleza kwamba Zanzibar kuna viungo vya kipekee vyenye ladha nzuri."
Mhe. Balozi Matinyi amezitaja nchi ambazo atakuwa mwakilishi mbali ya Sweden kuwa Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Lithuania na Ukrane.
Akijibu swali kuhusu mgogoro wa nchi za Ukraine na Russia, Mhe. Balozi Matinyi alisema kuwa Tanzania inasimamia amani na hivyo inataka nchi zinapokwaruzana zitafute suluhu kwa mazungumzo na si kupigana vita.
Thursday, April 17, 2025
UJENZI WA MRADI WA MAJI PANGANI KIBAHA WAANZA
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imemkabidhi mkandarasi eneo la mradi wa maji wa Pangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.9.
Thursday, April 3, 2025
UJENZI KIWANGO CHA LAMI BARABARA YA PICHA YA NDEGE-BOKOMNEMELA UNARIDHISHA-MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ISMAIL USSI
MWENGE wa Uhuru umeridhishwa na mradi wa ujenzi wa barabara ya Picha ya Ndege-Bomotimiza yenye urefu wa mita 550 kiwango cha lami wenye thamani ya shilingi milioni 760.
MWENGE WAZINDUA MRADI WA KISIMA CHA MAJI HOSPITALI YA TUMBI KUTOA LITA 10,000 KWA SAA
USSI ATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA MIKOPO ASILIMIA 10 YA HALMASHAURI WAJIKWAMUE KIUCHUMI
VIJANA kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoani Pwani wametakiwa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata fedha za mikopo asilimia 10 za mapato ya ndani ya Halmashauri ili wajikwamue kiuchumi.
KIONGOZI MBIO ZA MWENGE KITAIFA ISMAIL USSI APONGEZA UJENZI ZAHANATI KILIMAHEWA
