Tuesday, March 3, 2026
KAMBI SAMIA ARDHI KLINIKI YAANZA PWANI
Sunday, March 1, 2026
PWANI YAANZA MAANDALIZI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
MKOA wa Pwani umeanza maandalizi ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo kilele cha maadhimisho kimkoa yatafanyika Machi 8, 2026 katika Uwanja wa Ujamaa, Kata ya Umwe, Tarafa ya Ikwiriri, Halmashauri ya Mji Rufiji.
Mratibu wa maadhimisho hayo, Roseline Kimaro, amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge.
Akizungumza kuhusu maandalizi, Kimaro amesema maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “Haki kwa Wanawake na Wasichana: Msingi wa Maendeleo Jumuishi Dira 2050,” ikisisitiza umuhimu wa usawa wa kijinsia na haki kama nguzo ya maendeleo endelevu.
Amesema lengo ni kutambua na kuenzi mchango wa wanawake katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, sambamba na kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Amebainisha kuwa kuanzia Machi 1 hadi 7 kutafanyika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo utoaji wa elimu kwa umma na kampeni za uhamasishaji kuhusu usawa wa kijinsia, kilele cha maadhimisho Machi 8.
Ameongeza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na kutoa wito kwa wananchi na wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi kushiriki na kuunga mkono jitihada za kulinda na kuimarisha haki za wanawake na wasichana.
Friday, February 27, 2026
TRA PWANI KUBADILI UTARATIBU UKUSANYAJI KODI BANDARI YA BAGAMOYO
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani kuanza utaratibu mpya ukusanyaji mapato Bandari ya Bagamoyo Machi Mosi mwaka huu.Akizungumza na wafanyabiashara wa mafuta ya kula kwenye Bandari hiyo Meneja wa TRA Mkoa huo Masawa Masawa alisema kuwa changamoto iliyopo ni malalamiko ya wafanyabiashara kulalamikia bei ya kodi ya mafuta yanayotoka Zanzibar.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga alisema kuwa wananchi wengi wanategemea biashara ya mafuta na kuna wadau wengi wanategemea shughuli zinazohusiana na biashara ya mafuta.
Naye Diwani wa Kata ya Dunda Amiry Mpwimbwi alisema kuwa eneo hilo la Bandari linatoa ajira zaidi ya 8,000 hivyo kutokana na shughuli kutofanyika kumesababisha serikali kukosa mapato.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Mafuta kwenye Bandari hiyo Shaban Hamsini alisema kuwa hali imeshakuwa mbaya kwani wanategemea shughuli hizo kuendeshea maisha yao.
Saturday, February 21, 2026
MATUMLA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KUTATUA CHANGAMOTO
MWENYEKITI wa Mtaa wa Mwendapole B Manispaa ya Kibaha Abubakar Matumla ameendelea na ziara ya kutafutia majawabu changamoto zinazowakabili wananchi wa Mtaa huo.
DIWANI TANGINI ATOA POLE MTOTO ALIYENUSURIKA KIFO KWA KUSOMBWA NA MAJI NA WALIOEZULIWA PAA ZA NYUMBA ZAO
Thursday, February 19, 2026
ATAKA MASLAHI KWA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI
MADIWANI MANISPAA YA KIBAHA WAPITISHA BAJETI YA 2026/2027 YA TSH BILIONI 68.7 KWA KISHINDO
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani wamepitisha kwa kishindo bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 yenye jumla ya Shilingi Bilioni 68.7 katika Baraza Maalum la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kibaha.
Akizungumza wakati wa kupitisha bajeti hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Mawazo Nicas, amesema bajeti hiyo ni chachu ya maendeleo kwa wananchi na imezingatia mahitaji halisi ya Halmashauri.
“Bajeti hii imepitia kamati zote, imejadiliwa na kuboreshwa. Ni wajibu wetu kuipitisha ili ikalete maendeleo kwa wananchi wetu,” amesema Dkt. Nicas.
Diwani wa Kata ya Kibaha, Omary Bula, amesema bajeti hiyo imeandaliwa kwa ushirikishwaji wa madiwani wote na kuwataka wajumbe kuipitisha kwa maslahi ya wananchi.
Awali akiwasilisha rasimu ya bajeti hiyo, Naibu Meya wa Manispaa ya Kibaha, Aziza Mruma, amesema Halmashauri imekisia kutumia kiasi hicho cha Shilingi Bilioni 68.7, ikiwa ni ongezeko la asilimia sita ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2025/2026.
Kwa mujibu wa Mruma, katika mchanganuo wa bajeti hiyo, mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Shilingi Bilioni 17.8, miradi ya maendeleo Shilingi Bilioni 8.7, huku asilimia 60 ya mapato ya ndani ikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo na asilimia 40 kwenye matumizi ya kawaida.
Aidha, Shilingi Bilioni 1.4 zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Katika mwaka huo wa fedha, Halmashauri inatarajia kujenga kituo kimoja cha afya na zahanati mbili, pamoja na kutekeleza miradi ya kimkakati yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.3. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa maegesho ya malori yenye thamani ya Shilingi Milioni 242.3, kituo cha kibiashara Mbonde, na ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyama chenye thamani ya Shilingi Milioni 524.7.
Baada ya majadiliano, madiwani kwa pamoja waliipitisha bajeti hiyo kwa kauli moja, wakiahidi kusimamia utekelezaji wake ili kuhakikisha inaleta tija na maendeleo kwa wananchi wa Manispaa ya Kibaha.







