Thursday, May 25, 2023

SHULE ZA SEKONDARI TUMBI NA MWANALUGALI ZAPOKEA MILIONI 300

SHULE ya Sekondari ya Tumbi imepokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule.

Aidha Shule ya Sekondari ya Mwanalugali imepokea kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula.

6,052 WATAMBULIWA MTAA WA LUMUMBA WALIOVAMIA SHAMBA LA MITAMBA

MTAA wa Lumumba Halmashauri ya Mji Kibaha utambuzi wa wananchi waliovamia eneo imefanyika na kukamilika na jumla ya wananchi 6,052 wametambuliwa.

Hayo yalisemwa na Hamis Shomari ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira na diwani wa Kata ya Kongowe aliyasema hayo kwenye kikao cha kawaida kipindi cha robo tatu Januari-Machi cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha.

Alisema kazi ya utambuzi wa wananchi waliovamia eneo imefanyika na kukamilika na kazi ua uandaaji michoro nane yenye jumla ya viwanja 7,264 imekamilika.

"Maandalizi ya upimaji katika mtaa wa Lumumba yamekamilika na kazi ya upimaji wa viwanja na matarajio ni kupima viwanja 7,264 ambapo itakamilika ndani ya miezi miwili,"alisema Shomari.


HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAFANYA UTAMBUZI WA WALIOVAMIA ENEO MTAA WA MKOMBOZI

HALMASHAURI ya Mji Kibaha imefanya utambuzi wa wananchi waliovamia maeneo kwenye Mtaa wa Mkombozi ambapo 4,509 wametambuliwa.

Hayo yalisemwa na Hamis Shomari ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira na diwani wa Kata ya Kongowe aliyasema hayo kwenye kikao cha kawaida kipindi cha robo tatu Januari-Machi cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha.

Shomari alisema kuwa watu hao wametambuliwa ili kupimiwa viwanja 6,250 kwenye michoro 22 ambayo imeandaliwa na kuidhinishwa. 

"Kazi ya upimaji wa viwanja 6,300 imefanyika na kuwasilishwa kwa ajili ya uidhinishwaji wa ramani kwa mpima ardhi wa mkoa na jumla ya viwanja 3,950 vimeidhinishwa,"alisema Shomari.

Alisema kuwa uuzaji wa viwanja katika mtaa umeanza Machi 24 ambapo wananchi walijulishwa kwa njia ya matangazo na mkutano wa hadhara ambapo hadi Aprili jumla ya ankara ya viwanja 168 vyenye thamani ya shilingi milioni 129.2 zimetolewa.

HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAKUSANYA MABILIONI

HALMASHAURI ya Mji Kibaha imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.5 sawa na asilimia 78 ya makisio ya mwaka 2022/2023 ikiwa ni mapato ya ndani ambapo ilikadiria kukusanya shilingi bilioni 4.5.

Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina Wilson wakati wa kikao cha baraza la madiwani kwa kipindi cha robo tatu Januari hadi Machi.

Wilson alisema kuwa makusanyo hayo ni kuanzia Julai 2022 hadi Machi 2023 ambapo kwa upande wa vyanzo fungwa makisio ilikuwa ni shilingi milioni 506.7.

"Na kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2022 mpaka Machi 2023 kiasi cha shilingi milioni 587.8 kimekusanywa sawa na asilimia 116 ya makisio ya mwaka,"alisema Wilson.


HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAKUSANYA MABILIONI



HALMASHAURI ya Mji Kibaha imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 3.5 sawa na asilimia 78 ya makisio ya mwaka 2022/2023 ikiwa ni mapato ya ndani ambapo ilikadiria kukusanya shilingi bilioni 4.5.

Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina Wilson wakati wa kikao cha baraza la madiwani kwa kipindi cha robo tatu Januari hadi Machi.

Wilson alisema kuwa makusanyo hayo ni kuanzia Julai 2022 hadi Machi 2023 ambapo kwa upande wa vyanzo fungwa makisio ilikuwa ni shilingi milioni 506.7.

"Na kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2022 mpaka Machi 2023 kiasi cha shilingi milioni 587.8 kimekusanywa sawa na asilimia 116 ya makisio ya mwaka,"alisema Wilson.

Saturday, May 20, 2023

VYAMA VYA USHIRIKA KUUNGANISHWA NA WADAU


Na Wellu Mtaki, Dodoma

JUKWAA la maendeleo ya vyama vya ushirika  mkoa wa Dodoma limepanga kuwaunganisha vyama vya ushirika na wadau mbalimbali wakiwemo mabenki ili kuwawezesha kifedha pamoja na kuimalika kimtaji  viweze kupata maendeleo.

Hayo ameyasema  Jijini Dodoma Kaimu Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Dodoma Octavia Bidyanguze wakati wa uzinduzi wa jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Dodoma 2023.

Bidyanguze amesema mkoa wa Dodoma una vyama vya ushirika 124 vikiwemo 57 vyama vya kifedha, 49 vyama vya  kilimo na masoko na vyama vinginevyo 18 hivyo kutokana na idadi hii jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika linakwenda kuwajengea uwezo kwa maana ya kutoa elimu kwa vyama hivyo.

Amesema kuwa mpaka sasa vyama hivyo vimeweza kununua hisa zenye thamani ya 146.3 ili kuwa na uwezo  wa kusaidiana kwa wale wasio na uwezo wa kifedha.

Kwa upande wake Meneja wa UDOM SACCOS LTD Erasmus Tandike amesema kuwa Moja ya mikakati walio nayo ni kujitangaza na kuhakikisha ushirika huu unaazia ngazi ya chini ili kufikia wakazi wote wa Dodoma pamoja na  kuhakikisha kila vyama vinanufaika na vinafikia malengo.

Naye Mjumbe wa bodi ya PCCB SACOOS pia ni   Mratibu wa kongamano la Central Women Connect  Rashida Mfaume amewataka wanawake kukimbilia fursa ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kijamii kama ambayo yeye  amenufaika na ushirika huu kwa maana ya kuweza  kuwekeza pamoja na kupata nafasi ya kukopa .

Ikumbukwe kuwa moja ya lengo la jukwaa hili ni kutoa fursa vyama vya ushirika, kuwakutanisha na kubadilishana uzoefu, kuelimishana na kuweza kujifunza mambo mbalimbali ya vyama vya ushirika.




Thursday, May 18, 2023

WIZARA VIWANDA NA BIASHARA KUANDAA MWONGOZO KWA WAFANYABIASHARA

MKURUGENZI wa uwezeshaji wananchi kiuchumi na maendeleo ya sekta binafsi ya TAMISEMI Conrad Milinga amesema kuwa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji inaandaa mwongozo wa kuwawezesha wafanyabishara wajasiliamari kutambua kuwa wanapohitaji kuanzisha biashara sehemu ya kuanzia na kuishia.

Milingi ameyasema hayo Jijini Dodoma, katika kikao cha kuthibitisha rasimu ya muongozo wa wataalamu wa biashara na mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kilichofanyika katika ukumbi wa bodi ya wakandarasi.

Aidha amesema kuhusiana na taarifa za mwenendo wa bei za vyakula nchini wanahitaji kuzipata kuanzia kwao lakini zisitofautiane na zile zinazotolewa na wizara, hivyo waweke mfumo wa taarifa watakazo kuwa wanazipata kutoka kwao.

Kwa upande wake katibu tawala masidizi wa viwanda, biashara na uwekezaji mkoa wa Kigoma Deogratias Sangu, amesema kabla ya kuanzishwa kwa idara hiyo wizara ilikuwa ikifanya, kuunda, kupendekeza pamoja na kuanzisha sera ambapo utekelezaji wa chini haukuwa thabiti kwasababu haukuwa na wasimamizi, hivyo kupitia idara hiyo wasimamizi wana mwendelezo wa majukumu yaliyopangwa yatatimizwa.

Naye katibu tawala msaidizi viwanda, bishara na uwekezaji mkoa wa Morogoro Beatrice Njawa amesema kwakuwa wamepitishwa kwenye mpango wa kuboresha mazingira ya kufanyia bishara anaamini wanaenda kusimamia na kuondoa vikwazo vyote vya kibishara na uwekezaji katika mamlaka za serikali za mitaa na mikoani ili kuweza kutangaza uwekezaji unaopatikana katika maeneo hayo.

Njawa ameongeza kuwa wakiweza kuboresha eneo hilo hasa uwekezaji na ujenzi wa viwanda maana yake wanaenda kuzipa nguvu mamlaka za serikali za mitaa na wataongeza mapato na wanaenda kuimalisha mahusiano kati ya mikoa, halmashauri pamoja na sekta binafsi zilizopo katika maeneo yao.