MKURUGENZI wa uwezeshaji wananchi kiuchumi na maendeleo ya sekta binafsi ya TAMISEMI Conrad Milinga amesema kuwa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji inaandaa mwongozo wa kuwawezesha wafanyabishara wajasiliamari kutambua kuwa wanapohitaji kuanzisha biashara sehemu ya kuanzia na kuishia.
Milingi ameyasema hayo Jijini Dodoma, katika kikao cha kuthibitisha rasimu ya muongozo wa wataalamu wa biashara na mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kilichofanyika katika ukumbi wa bodi ya wakandarasi.
Aidha amesema kuhusiana na taarifa za mwenendo wa bei za vyakula nchini wanahitaji kuzipata kuanzia kwao lakini zisitofautiane na zile zinazotolewa na wizara, hivyo waweke mfumo wa taarifa watakazo kuwa wanazipata kutoka kwao.
Kwa upande wake katibu tawala masidizi wa viwanda, biashara na uwekezaji mkoa wa Kigoma Deogratias Sangu, amesema kabla ya kuanzishwa kwa idara hiyo wizara ilikuwa ikifanya, kuunda, kupendekeza pamoja na kuanzisha sera ambapo utekelezaji wa chini haukuwa thabiti kwasababu haukuwa na wasimamizi, hivyo kupitia idara hiyo wasimamizi wana mwendelezo wa majukumu yaliyopangwa yatatimizwa.
Naye katibu tawala msaidizi viwanda, bishara na uwekezaji mkoa wa Morogoro Beatrice Njawa amesema kwakuwa wamepitishwa kwenye mpango wa kuboresha mazingira ya kufanyia bishara anaamini wanaenda kusimamia na kuondoa vikwazo vyote vya kibishara na uwekezaji katika mamlaka za serikali za mitaa na mikoani ili kuweza kutangaza uwekezaji unaopatikana katika maeneo hayo.
Njawa ameongeza kuwa wakiweza kuboresha eneo hilo hasa uwekezaji na ujenzi wa viwanda maana yake wanaenda kuzipa nguvu mamlaka za serikali za mitaa na wataongeza mapato na wanaenda kuimalisha mahusiano kati ya mikoa, halmashauri pamoja na sekta binafsi zilizopo katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment