Hayo yamesemwa leo Mei, 26 2023 na Mhe David Silinde (Mb.) Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa makabidhiano ya ardhi iliyokuwa sehemu ya Ranchi ya Ruvu kwenda kwa Wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo na Kibaha ambapo pande zote zimeridhia.
Ameeleza uamuzi huo wa Serikali ni kuwawezesha Wananchi kupata Ardhi kwa ajili ya Shughuli za kilimo, Mifugo na shughuli zingine za kijamii.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Ranchi ya NARCO Ruvu ukishuhudiwa na Viongozi wa Wilaya,Tarafa, Kata, Vijiji na Viongozi wa Wakulima na Wafugaji na wawakilishi wa Wananchi kutoka Vijiji 10.
Akipongeza uamuzi huo Mhe Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani amewaagiza Viongozi wa Mkoa na Wilaya kutimiza wajibu wao wa kusimamia kupanga matumizi ya Ardhi hiyo na kuwataka Wananchi kuheshimu Sheria na kwamba wasivamie tena eneo hilo la Serikali.
No comments:
Post a Comment