JUKWAA la maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Dodoma limepanga kuwaunganisha vyama vya ushirika na wadau mbalimbali wakiwemo mabenki ili kuwawezesha kifedha pamoja na kuimalika kimtaji viweze kupata maendeleo.
Hayo ameyasema Jijini Dodoma Kaimu Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Dodoma Octavia Bidyanguze wakati wa uzinduzi wa jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Dodoma 2023.
Bidyanguze amesema mkoa wa Dodoma una vyama vya ushirika 124 vikiwemo 57 vyama vya kifedha, 49 vyama vya kilimo na masoko na vyama vinginevyo 18 hivyo kutokana na idadi hii jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika linakwenda kuwajengea uwezo kwa maana ya kutoa elimu kwa vyama hivyo.
Amesema kuwa mpaka sasa vyama hivyo vimeweza kununua hisa zenye thamani ya 146.3 ili kuwa na uwezo wa kusaidiana kwa wale wasio na uwezo wa kifedha.
Kwa upande wake Meneja wa UDOM SACCOS LTD Erasmus Tandike amesema kuwa Moja ya mikakati walio nayo ni kujitangaza na kuhakikisha ushirika huu unaazia ngazi ya chini ili kufikia wakazi wote wa Dodoma pamoja na kuhakikisha kila vyama vinanufaika na vinafikia malengo.
Naye Mjumbe wa bodi ya PCCB SACOOS pia ni Mratibu wa kongamano la Central Women Connect Rashida Mfaume amewataka wanawake kukimbilia fursa ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kijamii kama ambayo yeye amenufaika na ushirika huu kwa maana ya kuweza kuwekeza pamoja na kupata nafasi ya kukopa .
Ikumbukwe kuwa moja ya lengo la jukwaa hili ni kutoa fursa vyama vya ushirika, kuwakutanisha na kubadilishana uzoefu, kuelimishana na kuweza kujifunza mambo mbalimbali ya vyama vya ushirika.
No comments:
Post a Comment