Shirika la AMEND Tanzania ambalo linajihusisha na masuala ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usalama barabarani limeweza kutoa elimu na mafunzo kwa maafisa wasafirishaji wa vituo tofauti katika jiji la Dodoma.
Shirika hilo ambalo lipo chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania limeweza kutoa elimu na mafunzo kwa maafisa wasafirishaji maarufu kwa jina la bodaboda kwa malengo ya kudhibiti wigo ajali barabarani pamoja na kuwapa mafunzo mbali mbali pamoja na utumiaji wa alama za barabarani ambazo zimekuwa zikipuuzwa na maafisa wasafirishaji hao.
Nuhu Toyi ambaye ni balozi wa mafunzo na afisa msafirishaji kutoka kituo cha UDOM jijini Dodoma amesema alibaatika kupata mafunzo ambayo yametolewa na shirika la AMEND Tanzania na kupitia mafunzo hayo yameweza kumsaidia kuendesha chombo chake kwa kujihamini bila kusababisha ajali.
“Pongezi za dhati ziende kwa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania hususan kitengo cha afya kinachofadhiliwa na miss Vivian kwa kutambua umuhimu wa kundi hili la vijana wa bodaboda wengi ni vijana ambao tupo kati ya umri wa miaka 25. Kazi hii wengi tumekuwa tukiifanya kwa mazoea na hatuna elimu kwaio wengi tumekuwa ni wahanga wa kusababisha au kusababishiwa ajari kwasababu ya kukosa elimu barabarani lakini Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania umeona itakuwa ni vyema kama vijana hawa ambao ni taifa la kesho na nguvu kazi ya taifa wasiweze kudhuulika na ajali” alisema Toyi.
Kwa upande wake afisa usafirishaji, Laurenti Mayowa amesema alikuwa haelewi alama za barabarani lakini kupitia mafunzo hayo wamepokea kutoka shirika la AMEND Tanzania kwani limekuja kitofauti katika kutoa mafunzo yao kwani wamefundishwa kwa nadharia pamoja na vitendo.
“Tulipata mafunzo mazuri sana kwenye swala la uendeshaji wa pikipiki lakini pia tumeweza kufundishwa namna ya kutumia barabara lakini pia namba ya kutumi vyombo vyetu, kwa kweli mafunzo yalikuwa mazuri nimejifunza mambo mengi na mazuri na kabla ya mafunzo nilikuwa sielewi kwamba barabarani nilikuwa naendesha hovyo hovyo tu na baada ya mafunzo nashukuru mpaka sasaivi nime elewa na tulikuwa wengi sana tukifundishwa awamu kwa awamu nafikiri bodaboda takriban 230 au 250 kwa Dodoma hapa na sasahivi wame elimika”, alisema Mayowa.
Alisema alama za barabarani ilikuwa ni changamoto kwa madereva wengi , walikuwa wanaziona lakini wanashindwa kuzitumia kama ipasavyo na walidhani ni michoro tu lakini baada ya mafunzo waliweza kuelewa aina za michoro na alama zinazotumiwa barabarani.
“Tulifundishwa kuna alama za onyo, alama za amri, kuna alama za maelekezo kwaio hayo yote tumefundishwa lakini pia nimefundishwa alama nyengine ambazo nilikuwa sizielewi vizuri kama alama za michoro juu ya sakafu ya barabara hizo nazo nilikuwa sizielewi nilikuwa naona tu michoro na sielewi maana yake lakini baada ya elimu nimevielewa vizuri” alisema Mayowa
Aidha alisisitiza kwa maafisa usafirishaji kubadilika na kuwa na mahudhurio mazuri ya mafunzo yanayotolewa na shirika la AMEND Tanzania kwasababu yanafundishwa kwa vitendo pamoja na kutii sheria za barabarani.
“Tumefundishwa dereva kujihami kwaio wale ambao hawajapata mafunzo hawezi kuelewa na kutii sheria akiwa yupo barabarani na anaweza kusababisha ajali kwasababu anakuwa hana uelewa wowote na vigumu kujilinda anapotumia chombo chake”,Mayowa.
Naye afisa usafirishaji kutoka kituo cha Ndasha,Bw. Ally Rashid Ally alisema kuwa bodaboda ni ajira kama zilivyo ajira nyengine na imeteka soko kubwa la ajira kwa vijana kwenye upataji wa kipato na awali haikupewa thamani kama zilivyo biashara nyengine.
Amesema wamekuwa na madereva usafirishaji wengi lakini baadhi yao kwenye kundi hilo hawana elimu ya kutosha ya barabarani na kutambua alama zilizomo.
Aidha Bw. Ally amesema elimu iliyotewa ni msaada mkubwa kwa maafisa usafirishaji mkoani Dodoma kwani wengi wao wamekuwa na nidhamu iwapo wanatumia vyombo vyao barabarani na changamoto za ajali na vifo vimeweza kuepukika kutokana na maarifa waliopokea kutoka kwa wakufunzi kupitia shirika la AMEND Tanzania.
No comments:
Post a Comment