Na John Gagarini
WATU watatu wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kugongana na pikipiki.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei
alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya mchana eneo la Msata-
Kihangaiko wilayani Bagamoyo.
Kamanda Matei alisema kuwa watu hao waliofariki wawili
waliokuwa wamepakia pikipiki na dereva wa basi la Jay.
“Chanzo cha ajali hiyo
ni mwendo wa kasi wa basi la Jay lenye namba za usajili T 732 AFP lililokuwa
likitoka Morogoro kwenda mkoani Tanga na kugongana ambapo watu wote walifia
papo hapo,” alisema Kamanda Matei.
Aliwataja waliokufa kuwa ni Bw Sindi Kombo (48) mkazi wa
Tanga ambaye ni dereva wa basi, Bw Mangulu Idd (48) fundi bomba na Bi Sharifa
Omary (42).
Aidha alisema kuwa maiti wamehifadhiwa zahanati ya Msata huku
majeruhi wakiwa wamepelekwa hospitali ya Chalinze na Lugoba ambapo wangine
watahamishiwa hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment