Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia wahamiaji haramu watano
wa nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kuingia nchini bila ya kibali.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani humo Ulrich Matei
alisema kuwa raia hao walikamatwa wakati wa msako wa kukamata wahamiaji haramu.
Kamanda Matei alisema kuwa wahamiaji haramu hao walikamatwa
Januari 23 mwaka huu huko Kitongoji cha Kibosha Kijiji cha Mapinga wilayani
Bagamoyo.
“Wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa wanasafirishwa
kwenye gari namba T 371 BTL aina ya Noah,” alisema Kamanda Matei.
Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshw ana Bw Evarist
Mbilinyi (25) dereva wa Mwananyamala Jijini Dar es Salaam akisaidiwa na Omary
Karim (28) fundi magari mkazi wa Magomeni Makuti wakielekea Ethiopia kupitia
Bagamoyo.
Aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Itemegen Wolde (20)
mwanafunzi, Beyene Dutano (25), Aduel Ashebo (24) na Detene Bore (25) kutoka
nchini Ethiopia na Abdirsa Abdilim (20) ambaye ni raia wa nchi ya Somali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment