Na John
Gagarini
CHAMA cha
soka mkoa wa Kilimanajaro (KRFA) kitafanya usaili kwa wadau walijitokeza kujaza
nafasi za uongozi Januari 14 mwaka huu.
Akizungumza kwa
njia ya simu msemaji wa chama hicho Yusufu Mazimu alisema kuwa uchaguzi wa
kujaza nafasi hizo uitafanyika Januari 26.
Mazimu alisema
kuwa hadi sasa ni wadau sita waliojitokeza kujaza nafasi hizo ambazo zilibaki
wazi kutokana na wagombea kutokuwa na sifa kwenye uchaguzi wa chama hicho
uliofanyika Septemba 29 mwaka jana.
“Kwa muda
uliobaki tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze ili kuwania nafasi hizo ili
kukifanya chama kuwa na uongozi uliokamilika kwani kwa sasa uongozi bado
haujakamilika,” alisema Mazimu.
Alizitaja
nafasi hizo zilizobaki wazi kuwa ni pamoja na makamu mwenyekiti, katibu
msaidizi, mjumbe kwenda TFF, mwakilishi wa soka la wanawake na wajumbe wawili
wa kamati ya utendaji.
“Gharama ya
fomu kwa nafasi za juu ni shilingi 100,000 huku nafasi za ujumbe zikitolewa kwa
shilingi 50,000 ambapo tunawaomba wadau wajitokeze kabla ya muda wa usaili
kwisha,” alisema Mazimu.
Mwisho.
Na John
Gagarini
TIMU za soka
za Polisi na Magadini zinatarajiwa kuchuana kwenye ligi daraja la Tatu mkoa wa
Kilimanajaro Jumamosi Januari 12 mwaka
huu.
Kwa Mujibu wa
Msemaji wa Chama Cha soka Mkoa wa Kilimanjaro KRFA Yusufu Mazimu alisema kuwa
mchezo huo utapigwa kwenye kituo cha VETA.
Mazimu alisema
kuwa siku ya Jumapili Januari 13 kutakuwa na mchezo baina ya timu za Panone na
Kitayosce kwenye kituo hicho.
Katika kituo
cha Holili utapigwa mchezo baina ya Mwanga Asilia na Machava huku Jumapili
ikiwa ni kati ya Kurugenzi na Bodaboda.
Kwenye michezo
iliyopita Machava imeicharaza Bodaboda kwa magoli 2-1.
Mchezo huo
ulipigwa kwenye uwanja wa Holili magoli ya washindi yalifungwa na Adam Soba
dakika ya 29 na Issa Kipese dakika ya 80 na la Bodaboda lilifungwa na Paul
Wliam dakika ya 17.
Kwenye kituo
cha Himo Kilimanajaro iliifunga Vijana kwa magoli 2-1 wafungaji wakiwa ni Omary
Juma dakika ya 24 na Ramadhan Gumbo dakika ya 36 la vijana lilifungwa na Abdala Husein dakika
ya 75.
Timu ya
Polisi Hai iliifunga KIA kwa mabao 4-0 mchezo uliopigwa kituo cha VETA Soweto
na Forest walishindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu ya 0-0.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment