Tuesday, January 15, 2013

KOMBE LA NG'OMBE

Na John Gagarini, Kibaha

TIMU ya soka ya Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani imeifunga timu ya Mbwate kwa magoli 2-1 mchezo wa ligi ya Mbwate Cup kwenye uwanja wa Mwendapole.

Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kuvutia uliovuta mashabiki wengi iliwachukua Mbwate dakika 29 kuandika bao kupitia kwa Mbulu Juma.

Maili Moja walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kwa Keneth Lufunga dakika ya 40 ambapo timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo mabadiliko hayo ambayo yaliisaidia zaidi Maili Moja ambao walifanikiwa kupata bao la ushindi dakika ya 89 kupitia kwa Lufunga kwa mara nyingine.

Kutokana na matokeo hayo Maili Moja imefanikiwa kufuzu hatua ya nane bor kutoka kundi, huku kundi B Parasuparasu wakifuzu, kundi C Lisborn nayo imefuzu hatua hiyo.

Jumla ya Makundi manne yanamenyana katika michuano hiyo ambapo kila kundi litatoa timu mbili kwenda hatua ya robo fainali na  Msindi wa kwanza atajinyakulia ngombe mnyama huku mshindi wa pili akipata mbuzi mnyama na mshindi wa tatu akijinyakulia mpira mmoja.

Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo Mshindo Kitike lengo la michuano hiyo ni kukuza vipaji vya vijana ndani ya wilaya hiyo na mashindano hayo yameandaliwa na mdau wa michezo Bakar Mbepo.

       

No comments:

Post a Comment