Na John Gagarini, Kibaha
HATIMAYE wanafunzi wa sekondari ya Kata ya Maili Moja
wilayani Kibaha mkoani Pwani waliokamatwa na mgambo wa kata kwa tuhuma za
kutoingia madarasani na kuishia vichakani na kukutwa na kondomu wameadhibi kwa
kuchapwa viboko.
Wanafunzi hao walipata adhabu hiyo jana baada ya
baraza la kata kuwakuta na hatia ya kujihusisha na vitendo kinyume na taratibu
za shule.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza la kata Bw Amadeus
Ngombale alisema kuwa wanafunzi hao walikiri kujihusisha na vitendo hivyo
kinyume cha maadili ikiwa ni pamoja na kukutwa na kondomu na simu.
“Baada ya kukiri baraza lilitoa adhabu ya viboko
kutegemea na kosa la mhusika ambapo adhabu hizo za viboko walichapwa na wazazi
wao ambao nao walitwa kwenye baraza hilo,” alisema Bw Ngombale.
Bw Ngombale alisema kuwa wao kama baraza walishatoa
adhabu yao na wanatakiwa Jumatatu Januari 28 wanatakiwa kwenda shuleni na
wazazi wao ili wapewe taratibu nyingine za shule.
“Bodi ya shule ndiyo itakayoamua hatma ya wanafunzi
hao kama watapewa adhabu nyingine au kuwasamehe hilo litaamuliwa na bodi ya
shule kwa lengo la kurejesha nidhamu kwa wanafunzi hao,” alisema Bw Ngombale.
Wanafunzi hao waliomba msamaha na kukiri kuwa
hawatarudia tena kwani walifanya vitendo hivyo kwa kuiga tu mambo ya ujana.
Wanafunzi hao walikamakamatwa juzi na mgambo wa kata
hiyo kwani walikuwa hawaingii madarasani na kuishia njiani huku wengine wakiwa
vichakani na kukutwa na kondomu kwenye mifuko yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment