Na John
Gagarini, Bagamoyo
MKUU wa
wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Bw Ahmed Kipozi ametaka apewe majina ya ofisa
aliyetoa viwanja kwenye hifadhi ya Misitu ya Mikoko wilayani humo.
Akizungumza
na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya mara baada ya zira
kutembelea misitu ya hifadhi ya Uzigua na Mikoko iliyoandaliwa na Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bagamoyo na kusema uharibifu uliofanyika
alisema kuwa misitu hiyo imeharibiwa kwa kiasi kikubwa.
Bw Kipozi
alisema kuwa inashangaza kuona maofisa hao kugawa viwanja kwenye hifadhi ya
misitu badala ya kutoa viwanja kwenye maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya
viwanja.
“Siwezi
kukubaliana na watu ambao hawawajibiki ipasavyo kwani inashangaza kuona kuwa
watu wanatoa maeneo ambayo ni hifadhi kwani misitu ni muhimu kwa viumbe hai
hivyo nataka niwajue waliofanya hivi ili hatua ziweze kuchukuliwa,” alisema Bw
Kipozi.
Aidha alisema
kuwa watu waliopewa viwanja kwenye maeneo hayo ya hifadhi ya mikoko wamekata
miti hiyo ambapo baadhi walikata ili kuona madhari ya bahari na wengine
walianzisha miradi ya samaki.
“Wameharibu
hifadhi hii kwa kiasi kikubwa kwani kila mtu anaelewa umuhimu wa misitu kwani
kukata miti kuna athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mvua kuharibu
mazalio ya samaki na kubadili uoto wa asili hivyo lazima wahusika wawajibike,”
alisema Bw Kipozi.
Kwa upande
wake meneja wa wilaya ya Bagamoyo Bw Charles Mwamfute alisema kuwa hifadhi za
misitu hiyo zimeharibiwa na watu kwa ajili ya kukata miti, kuchoma mkaa na
wafugaji kuingia kwenye misitu hiyo.
“Sisi wakala
mpya ambao umeanzishw akwa ajili ya kulinda misitu ya asili kila wailaya hivyo
hatua ya kjwanza ni kuangalia eneo ambalo limeathirika na uharibifu ambapo tutawachukulia
hatua za kisheria wale waliongia kwenye hifadhi za misitu,” alisema Bw
Mwamfute.
Bw Mwamfute
alisema kuwa Misitu ya Uzigua zaidi ya nusu ya misitu hiyo imeharibiwa ambayo
ni hekta 24,436 kwenye msitu wa Uzigua huku ile ya mikoko hekta 70 zimeharibiwa
kati ya hekta zaidi ya 5,000.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment