Picha ya matukio ya Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani ikiwakirishwa na Ndugu Omary Punzi Katibu wa Taasisi hiyo wakikabidhi Tshirt na Mipira ya zawadi ya mashindano ya NYERERE SUPER CUP 2023 Kwa Mhe Kanali Joseph kolombo Mkuu wa wilaya ya Kibiti Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Tarehe 23.9.2023 na kutamatisha 12.10.2023 yakishirikisha Timu 12 Timu 6 kutoka Kibiti na Timu 6 kutoka Rufiji wadhamini wa mashindano ni NSSf,NBC BANK na TANGANYIKA ORGANIC Kauli mbiu ya mashindano AMANI NA UMOJA VITAWALE MITANO TENA
Tuesday, September 12, 2023
Saturday, September 9, 2023
NYERERE SUPER CUP TIMU ZAKABIDHIWA VIFAA
MTANZANIA ALICE GYUNDA AOMBA APIGIWE KURA MRS/MISS AFRICA UK 2023
MSHIRIKI wa shindano la Miss/Mrs Africa UK 2023 kutoka Tanania Alice Gyunda amesema kuwa endapo atafanikiwa kushinda taji hilo atajenga studio kwenye baadhi ya shule a msingi a Jijini Dar es Salaam ili kuzalisha vipaji vingi vya waimbaji waweze kuitangaa nchi kupitia muziki.
Aidha alisema kuwa ndoto yake nyingine ni kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu hususani wanawake na watoto ili waweze kupata haki zao za msingi ili nao waweze kufikia malengo waliojiwekea katika maisha yao.
Gyunda ambaye ni mwalimu na mwimbaji akizungumza kwa njia ya simu kutokea nchini Uingereza anakoishi alisema kuwa endapo Watanania watampigia kura kwa wingi atakuwa na uwezo wa kushinda kwani hadi sasa bado yuko kwenye nafasi nzuri ya kufanya vema.
“Namewaomba Watanzania wanipigie kura ili nishinde ambapo vigezo ni kuonyesha utashi jinsi unavyo ongea na watu na namna unavyofanya mambo yako uwe mtu mwenye ushawishi na nikiwa mshindi nitakuwa balozi wa Kiswahili duniani na malengo yangu kuacha alama kwenye jamii kwa kusaidia watu wasiojiweza huko nyumbani japo niko mbali,”alisema Gyunda.
Alisema kuwa endapo atashinda atahakikisha anajenga studio kwenye baadhi ya shule za Msingi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wanafunzi ambao wana vipaji lakini hawana uwezo wa kurekodi itakuwa bure bure au kama kutakuwa na malipo yatakuwa ni madogo sana kwani muziki Tanzania uko chini sana licha ya kuwa na vipaji vingi kwani wengi hawawezi kurekodi kutokana na gharama kuwa kubwa.
“Nia ni kuinua muziki ambapo tutawekea kwa wanafunzi na vijana ambao wana vipaji vikubwa lakini kutokana na mazingira magumu ya uwezo wanashindwa kutimiza ndoto zao na wakipatikana vijana wenye vipaji wataenda kwenye matamasha ya American Good Talent au UK Good Talent ambapo vijana wa nchi za Uganda na Kenya huwa wanakwenda kwenye matamasha hayo ambapo atashirikiana na serikali ili nao washiriki wakirudi wawe chachu kwa wengine,”alisema Gyunda.
Aliongeza kuwa aliingia kwenye shindano hilo baada ya kuona tangazo na walipewa maswali 10 kuchujwa ambapo walikuwa 30 wakachujwa tena wakabaki 20 wakachujwa na kubaki 15 na baadaye mchujo mwingine ulifanyika na kubaki 13 ambapo wanatoka nchi za Afrika na Asia na kuwaomba Watanania wampigie kura ambapo hadi wakati anaongea alikuwa ameshapigiwa kura 1,800 kupitia https://africaukpageants.co. uk/poll/mrs-miss-africa- finalist-2023/

Friday, September 8, 2023
WAFANYABIASHARA WATAKA UBORESHWAJI WA HUDUMA SOKONI HAPO
WAFANYABIASHARA wa soko la Uhindini Wilaya ya Chunya wameomba uboreshwaji wa huduma zikiwemo za miundombinu ya barabara maji na umeme ili waweze kutoa huduma kwa ubora kwa wateja wao.
Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara wa wilaya hiyo wakati wa mkutano wa wafanyabiashara ulioongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Hamis Livembe September 7 wenye lengo la kupokea changamoto kero na maoni ya biashara ili kupatiwa ufumbuzi.
Mmoja wa wafanyabiashara wilayani hapo Qeen Mwasakela amesema kuwa changamoto ya umeme ina takribani miaka 10 tangu soko hilo kuanzishwa na kuiomba serikali kutatua kero hiyo.
Naye katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Ismail Masoud amewataka wafanyabiashara kueleza changamoto kwa mamlaka husika bila ya kuogopa ili zipatiwe ufumbuzi.
Katika hatua nyingine Masoud amewataka wafanyabiashara hao kutoungana na baadhi ya maofisa wa mamlaka mbalimbali ambao wanahujumu mipango ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasan ya ukusanyaji wa mapato.
Amesema kuwa wasikubali kudanganywa kuwa watapunguziwa au kufutiwa kodi kwa kutakiwa kutoa rushwa ambapo mamlaka zinazohusika zikifuatilia hujikuta akiwa na deni kubwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Hamis Livembe amesema kuwa ukosefu wa huduma bora za msingi za kibiashara zinasababisha kushuka kwa biashara na ulipaji kodi kutofanyika vizuri na atahakikisha changamoto hizo zinafikishwa kwenye mamlaka husika ili kupatiwa ufumbuzi.
WATAKA HATUA ZAIDI KUONGEZA MATUMIZI YA GESI
IMEELEZWA kuwa matumizi ya nishati ya gesi kwa ajili ya kupikia ni asilimia moja tu huku matumizi ya kuni na mkaa ikiwa ni asilimia 98.9 hapa nchini huku ikihitajika hatua za makusudi za kuzuia matumizi hayo ya miti ili kupunguza athari kubwa za kimazingira.
Aidha serikali imeombwa kuweka bei ya juu ya
upatikanaji wa vibali vya ukataji wa miti ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuhamasisha matumizi ya gesi majumbani.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na ofisa Mahusiano wa kampuni ya Taifa Gesi Ambwene Mwakalinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliotembelea eneo la ujazaji wa gesi ya (LPG) kwenye ghala lililopo Kigamboni.
Mwakalinga amesema kuwa matumizi ya kuni na mkaa ni makubwa sana hivyo kuna haja ya serikali kuweka jitihada za makusudi za kukabiliana na hali hiyo ili kusitokee mabadiliko ya Tabianchi ambayo yanasababisha athari ikiwemo ukosefu wa mvua na uharibifu wa mazingira.
Naye meneja wa ghala hilo la Kigamboni Juma Masese amesema kuwa Taifa Gesi ndiyo kampuni ya hifadhi kubwa ya gesi hapa nchini ambayo inamilikiwa na mzawa ambapo kwa sasa inahifadhi ujazo wa metriki tani 7,400 ambapo inatarajia kuwa kampuni ya kwanza Afrika kwa kuwa na hifadhi kubwa ya nishati hiyo ambayo huletwa na meli kutoka nchi zinazozalisha gesi duniani.
Kwa upande wake ofisa usalama wa kampuni hiyo Albert Bungayela amesema kuwa wanatoa elimu kwa mawakala ili nao watoe elimu kwa watumiaji kuwa makini katika matumizi ili kuepuka madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya gesi.
Thursday, September 7, 2023
JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA TANZANIA WACHARUKA MKOANI MBEYA
WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya waiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Mbeya kufanya marekebisho ya baadhi ya mifumo na Sheria za Kodi zinachochea rushwa .
Hayo yamesemwa na wafanyabiashara wa mkoani hapo wakati wa kupokea kero, maoni na changamoto za wafanyabiashara katika mkutano uliofanyika eneo la soko jipya la Mwanjelwa chini ya Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Hamis Livembe.
Wamesema kuwa TRA mkoani hapo imekuwa ikitumia mifumo hiyo kama chanzo cha mapato binafsi na si kuwasaidia kukuza biashara za wafanyabiashara hao.
Aidha wameitaka serikali kutambua kuwa uchumi wa Watanzania wengi unajengwa kupitia biashara hivyo wanaiomba serikali ipunguze ututiri wa kodi .
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya wafanyabiashara Tanzania Hamis Livembe amesema kuwa moja ya sababu ya kufanya ziara mkoani hapo ni kukusanya changamoto , kero na maoni ili kuyatafutia ufumbuzi kwa mamlaka husika.
Livembe amesema kuwa zipo changamoto zinazowakumba wafanyabiashara hivyo kama kiongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara atahakikisha kero zote zimetafutiwa ufumbuzi.
Naye katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Abdall Salim amesema kuwa wafanyabiashara wote Tanzania wanatakiwa kuungana kwa pamoja ili kukomboa biashara zao hivyo wanapaswa kujisajili na Jumuiya hiyo.
Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania ni Taasisi inayosimamiwa na wafanyabiashara wenyewe wenye lengo la kuhakikisha wanatatua changamoto za kibiashara.
Subscribe to:
Posts (Atom)