Na John Gagarini, ChalinzeMGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amekanusha kumtuma mgombea wa Chama Cha (SAU) Shaban Maulid kugombea Udiwani Kata ya Talawanda.Akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika kwenye Vijiji vya Kisanga, Vundumu na Talawanda kwenye kata hiyo alisema kuwa yeye hajamtuma mtu huyo wala hajawahi kukutana naye.Ridhiwani alisema kuwa yeye hawezi kumtuma mtu kwenda kugombea na kama ni kumtaka mtu basi angependekeza kutoka chama chake na si chama kingine kwani hakuna ushirikiano na vyama vingine.“Huyo mtu kwanza na mshangaa kwani sijawahi kumuona wala sijawahi kukutana naye wala sijawahi kumtuma mtu namshangaa unajua wagombea wengine hawana sera hivyo wanatumia majina ya watu kujipatia umaarufu,” alisema Ridhiwani.Alisema kuwa huo ni uzushi na wananchi hawapaswi kumsikiliza mtu huyo kwani chama chake hakina uhusiano na CCM wala na yeye na hajawahi hata kukutana naye.“Achaneni na maneno ya kutuvuruga kwani kwa sasa sisi tunafanya kampeni ili kuhakikisha chama cehtu kinashinda kwenye nafasi zote ikiwemo Urais, Ubunge na Udiwani hivyo wasituvurge wakati huu wa kampeni kama hawana sera wakae pembeni,” alisema Ridhiwani.Kwa upande wake meneja wa kampeni Jimbo la Chalinze Alhaj Amir Mkangata alisema kuwa anamshangaa mgombea huyo kwani hakuna muungano baina ya CCM na SAU kama ilivyo kwa muungano wa vyama vya upinzani vinavyounda UKAWA.Alhaj Mkangata alisema kuwa wagombea kama hao hawana uwezo hivyo wanatafuta njia ya kujipenedekeza ili kuonyesha kuwa wametumwa kugombea.“CCM haijaungana na chama kingine sasa mgombea huyo anavyojitapa kuwa ametumwa na CCM atuambie umoja huo unaitwaje atuambie hapa na tunamshangaa aache kabisa kutengeneza maneno ya uongo,” alisema Mkangata.Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Talawanda Said Zikatimu alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha kuwa changamoto zilizopo kwenye kata hiyo zikiwemo za Afya, Elimu na Maji.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeWAKULIMA na Wafugaji kwenye Kijiji cha Lulenge Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wametakiwa kuheshimiana ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza na kusababisha vurugu zinazopelekea kuvunja amani baina ya wananchi.Hayo yalisemwa na mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Lulenge kata ya Ubena.Ridhiwani alisema kuwa tatizo kubwa la migogoro linatokana na pande mbili hizo kutoheshimu mipaka yao kwani kuna baadhi ya maeneo yametengwa kwa jamii hizo mbili.“Mnaweza kuepusha migogoro kwa kuheshimiana na kuheshimu mipaka iliyopo kwani kila mmoja akimweshimu mwenzake migogoro haitakuwepo na watu wataishi kwa Amani na upendo,” alisema Ridhiwani.Alisema kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha inaondoa migogoro ikiwa ni pamoja na kutenga maoeneo kwa ajili ya mipango ya matumizi bora ya ardhi wakulima na wafugaji kwa baadhi ya maeneo huku mengine yakiwa yanaandaliwa kufanywa hivyo.“Nyie ni ndugu hakuna sababu ya kugombana na kuingia kwenye migogoro isiyokuwa ya lazima kwani mtashindwa kufanya shughuli za maendeleo kutokana na migogoro hiyo,” alisema Ridhiwani.Naye mgombea udiwani kupitia chama hicho Nicholaus Myuwa alisema kuwa atatumia taaluma yake ya kuwa Mwanasheria kuikabili migogoro hiyo kwa kuziweka pamoja jamii hizo.Myuwa alisema kuwa endapo atachaguliwa kuwa diwani watahakikisha changamoto za maji, zahanati na barabara zinatatuliwa kwa kuwashirikisha wananchi.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeWANANCHI wa Jimbo la Chalinze wametakiwa kutowachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwani wengi wao ni viongozi wa msimu ambao wanajitokeza nyakati za uchaguzi.Hayo yalisemwa na meneja wa kampeni wa Jimbo hilo Alhaj Amir Mkangata wakati wa mikutano ya kampeni ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete kwenye kata ya Miono.Alhaj Mkangata alisema kuwa chama chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo wananchi ni CCM na vyama vingine viongozi wao hawana uwezo hivyo ni vema wakaendelea kukiamini chama.“Msiwachague wapinzani kwani wengi wao wanajitokeza wakati wa uchaguzi lakini uchaguzi ukishaisha hawaonekani hivyo mkiwachagua hamtawapata kwani wengine hawajulikani hata wanapoishi lakini wa CCM wanafahamika na wanatambulika,” alisema Alhaj Mkangata.Alisema kuwa CCM imechagua wagombea wenye uwezo na wanasifa za kuongoza lakini wagombea wa upinzani hawana uwezo wa kuongoza hivyo hakuna sababu ya kuwachagua.“CCM imefanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo hivyo hakuna sababu ya kuchagua chama kingine kutawala hivyo msihadaike na wapinzani ambao wanaongopa kuwa wataleta maendeleo msikubali kudanganyika,” alisema Alhaj Mkangata.Aidha alisema kuwa kwa mwaka huu chama kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi wa kishindo ili kiweze kuongoza na kuleta maendeleo kwa wananchi.Aliwataka wananchi kuichagua CCM kwani ina uwezo wa kuongoza na wagombea walioingia kwenye kinyanganyiro cha ugombea kwenye ngazi mbalimbali wana uwezo kwani wamechaguliwa kwa uwezo wao.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeKIJIJI cha Lulenge kata ya Ubena Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo kinatarajia kuanza ujenzi wa zahanati Desemba mwaka huu ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwenyekiti wa Kijiji hicho Lucas Sultan alisema kuwa ujenzi huo utaanza baada ya kukamilika michango ya kila kaya.Sultan alisema kuwa walikubaliana kwenye mkutano wa Kijiji kila kaya itoe kiasi cha shilingi 20,000 kwa ajili ya kujenga zahanati kwa ajili ya kuwapatia huduma ya afya.“Tayari tuna eneo la ukubwa wa hekari tano kwa ajili ya kufanya ujenzi huo kwani ndani ya miezi michache ijayo tutakuwa tumekamilisha michango hiyo ili kuanza ujenzi,” alisema Sultan.Alisema kuwa kwa kaya itakayoshindwa kutoa mchango huo atapaswa kufanya shughuli za kijamii kama sehemu ya mchango wake ili kila mtu atoe jasho lake kwenye kijiji.Alisema kuwa kwa sasa wanapata huduma ya afya kwenye zahanati binafsi ambako ni mbali kwani usafiri uliopo ni wa pikipiki ambapo gharama yake ni shilingi 8,000 kwenda na kurudi.“Gharama za kwenda kupata matibabu ni kubwa sana hivyo ndiyo maana tuliona kuwa kuna haja ya kweza kuanzisha ujenzi wa zahanati ili kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Sultan.Aidha alisema kuwa changamoto nyingine ni kwamba sehemu kubwa ya kijiji iko kwenye hifadhi ya Wami Mbiki hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.“Suala la Kijiji kuwa kwenye hifadhi linafanyiwa kazi na tunaamini tutapata majibu mazuri na tunaamini mipaka itatengenezwa na tutaishi kwa utaratibu mzuri,” alisema Sultan.Alisema kuwa Kijiji hicho kina jumla ya wakazi wapatao 2,700 huku kukiwa na mifugo mbalimbali ngombe wakiwa 17,000, mbuzi 4,000 na mbuzi 2,000 ambapo wakazi wake ni wakulima na wafugaji.Mwisho.Na John Gagarini, ChalinzeMGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amesema kuwa endapo atafanikiwa kuwa mbunge atahakikisha anasimamia upelekwaji wa fedha pensheni za wazee kwa wakati.Aliyasema hayo katika kijiji cha Tukamisasa kata ya Ubena na kusema kuwa wazee wanapaswa kuheshimiwa na kupewa stahiki zao kwani wamefanya kazi kubwa ya kuifanya nchi ifikie hapa ilipo.Ridhiwani alisema kuwa kwa kuwa sera ya chama inaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2016 wazee watakuwa wanapata pensheni zao kwa ajili ya kuwasaidia katika maisha yao.“Wazee wetu wamefanya kazi kubwa hivyo kuna haja ya kuhakikisha wanapata stahiki zao kwani walifanya kazi kubwa kuikomboa nchi na kuifanya iwe kama ilivyo sasa moja ya vitu nitakavyovisimamia ni kuhakikisha fedha zao zinakuja kwa wakati,” alisema Ridhiwani.Alisema kuwa wazee wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wakipata pensheni zao zitawasaidia kuweza kujikimu na kumudu mambo madogomadogo tofauti na ilivyo sasa.“Wazee wakilipwa pensheni zao zitawasaidia kumudu maisha yao kwani walikuwa wakiishi kwenye hali ngumu kutokana na kukosa fedha hata za kununua vitu vidogovidogo ambavyo vingewasaidia kumudu maisha,” alisema Ridhiwani.Aidha wazee wamehudumia nchi ya Tanzania na kutumia nguvu zao na jasho lao hivyo ni haki yao sasa kupata pensheni ambayo itawafanya wajisaidie kwenye maisha yao.“Mbali ya kusimamia malipo hayo pia nitahakikisha wanapata huduma mbalimbali ambao ni fursa kwao ikiwa ni pamoja na matibabu pamoja na mikopo ambayo itawasaidia kwenye ujasiriamali,” alisema Ridhiwani.Mwisho.
Sunday, October 18, 2015
HABARI MOTO MOTO ZA KAMPENI ZA UCHAGUZI UCHAGUZI JIMBO LA CHALINZE
Wednesday, October 14, 2015
RIDHIWANI AMWAGIA SIFA DK MAGUFULI
Na John Gagarini, Chalinze
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk John
Magufuli amepongezwa kwa kuuachia mkoa wa Pwani hususani wilaya ya Bagamoyo
miradi mikubwa ambayo itakapokamilika itasaidia kuinua kipato cha wakazi wa
mkoa huo.
Miradi hiyo ambayo inatoka kwenye Wizara Ujenzi na
Miundombinu aliyokuwa akioongoza Dk Magufuli kabla ya kuteuliwa na chama chake
kuwa mgombea Urais kwenye kinyanganyiro kitakachofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa na mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze
kupitia chama hicho Ridhiwani Kikwete, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye Kijiji cha Miono wilayani Bagamoyo na kusema kuwa mgombea huyo kila mkoa
ameupatia miradi ambayo itachochea maendeleo.
Ridhiwani alisema kuwa Dk Magufuli ni kiongozi ambaye
anastahili kuongoza nchi hii kwani wakati akiwa waziri alihakikisha kila mkoa
unatumia rasilimali zake viuzuri ili kujiletea maendeleo hali ambayo
imesababisha nchi kupiga hatua.
“Sisi wakazi wa wilaya ya Bagamoyo tunamshukuru kwani ametuachia
miradi mikubwa ikiwa ni pamoja na ule wa Barabara ya Afrika Mashariki
itakayoanzia Bagamoyo, Makuruge, Saadani hadi mkoa wa Tanga hadi Mombasa nchini
Kenya,” alisema Ridhiwani.
Alisema kuwa mradi mwingine ni ule wa Bandari ambayo itakuwa
ni kubwa ambao utaanza wakati wowote kuanzia sasa kwani mipango tayari
imekamilika huku mradi wa barabara tatu zitakazoanzia Jijini Dar es Salaam hadi
mkoani Morogoro pia mzaini wa kisasa uliopo Vigwaza ambao tayari unafanya kazi.
“Mradi mwingine ni ule wa upanuzi wa Daraja la Mto Wami ili
kupunguza ajali zinazotokea kwenye daraja hilo ambapo kwa sasa magari hayawezi
kupishana, hakika miradi hii ni mikubwa na itafungua fursa za maendeleo kwa
kukuza uchumi wao kutumia fursa zilizopo na zitakazokuwepo kwenye miradi hiyo,”
alisema Ridhiwani.
Aidha alisema Dk Magufuli ni kiongozi ambaye hana kashfa
yoyote na ameonyesha kuwa anafaa kuliongoza Taifa la Tanzania kutokana na
uchapa kazi wake pamoja na uadilifu aliokuwa nao ukilinganisha na viongozi
wengine wanaowania nafasi hiyo.
Aliwataka watanzania kumchagua kwa kumpiga kura nyingi za
kishindo ili awe Rais wa awamu ya tano na anaamini kuwa uwezo wa kuongoza nchi
anao akiwa chini ya CCM ambao kwa wakati huu imechagua viongozi wenye sifa na
wanaopendwa na wananchi.
Mwisho.
| Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akizindua huku akiwa amekaa kwenye kigoda tawi la vijana wa Boda boda kwenye Kijiji cha Pongwemnazi |
| Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akizindua tawi kwa kupandisha bendera kwenye moja ya matawi wakati wa kampeni kuwania kiti hicho. |
| Mgombea Udiwani kata ya Kimange kwa tiketi ya CCM Husein Hadingoka akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kikwazu wakati wa mkutano wa kampeni |
| Mama Mwenye ulemavu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akiwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea wa CCM Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji cha Pongwemnazi kata ya Kimange. |
| Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye kijiji cha pongwekiona kata kimange wilayani bagamoyo |
| wananchi wa kijiji cha pongwekiona wakiwa wanamsikiliza mgombea ubunge jimbo la chalinze ridhiwani kikwete hayupo pichani wakati wa mkutano wa kampeni |
| Mwigizaji aitwaye Puto akitoa burudani kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Pongwemnazi kata ya Kimange wilayani Bagamoyo |
| Mwimbaji Sam wa Ukweli akiimba na moja ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni wa CCM kwenye kijiji cha Pongwemnazi |
| Wagombea Ridhiwani Kikwete kushoto akicheza na mgombea Udiwani kata ya Kimange Hussein Hadingoka wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye kijiji cha Pongwekiona |
| Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akimkabidhi moja ya wanachama wapya kwenye Kijiji cha Pongwekiona |
Friday, October 9, 2015
DK MAGUFULI AFUNIKA BAGAMOYO
| Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakimskiliza mgomea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM John Magufuli kwenye uwanja wa shule ya msingi Majengo Bagamyo. |
| Mkuu wa mkoa wa Tanga mwenye miwani Mwantumu Mahiza akielekeza jambo wakati wa kumsubiri mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk John Magufuli kwenye kijiji cha Mbwewe wilayani Bagamoyo |
| Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango |
| Mgombe urais wa CCM Dk John Magufuli kulia akitete jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ambaye pia ni mgombe Ubunge Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa |
| Aliyekuwa mgombea Ubunge kura za maoni wa CCM Jimbo la Bagamoyo Abdul Sharif kulia akiwa amepozi kushoto ni Dk zainab Gama katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Pwani |
| Abdala Bulembo mjumbe wa kampeni wa CCM Taifa akionyesha mfano wa fomu ya kupigia kura |
| Mgombea Urais wa CCM Dk John Mgafuli akiongea na wananchi wa Bagamoyo waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Majengo |
| Wananchi wakiinua mikono juu kumuunga mkono mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk John Magufuli |
| Wananchi wakimshangilia mgombea Urais Dk John Magufuli |
| Mgombea Urasi Dk John Magufuli kushoto akimnadi mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika bagamoyo |
| Dk John Magafuli kulia mgombea Urais CCM akimtambulisha mgombea Ubunge Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa |
| Baadhi ya madiwani wa wilaya ya Bagamoyo |
| Mgombea Ubunge kupitia Umoja wa Wanawake UWT mkoa wa Pwani Subira Mgalu kulia akitambulishw ana mgombea Urais CCM Dk John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Bagamoyo. |
Wednesday, October 7, 2015
WAOMBA KUONDOLEWA 100,000 KWA AJILI YA GARI LA WAGONJWA
Na John Gagarini, Chalinze
WAKAZI wa Kijiji cha Kwaruhombo Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo
wametoa kilio chao kwa kuomba viongozi watakaochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu
kuwaondolea changamoto ya kutozwa kiasi cha shilingi 100,000 kwa ajili ya
mafuta ya kuweka kwenye gari la wagonjwa wanaopata rufaa toka kwenye kituo cha
afya cha Kwaruhombo.
Akizungumza Kijijini hapo mara baada ya mkutano wa kampeni wa
mgombea ubunge jimbo hilo Ridhiwani Kikwete, Ally Rashid alisema kuwa hali hiyo
inawapa wakati mgumu kutokana na hali halisi ya kipato chao kidogo.
Rashid alisema kuwa changamoto hiyo ni kubwa kwani wao kupata
fedha hizo mzigo mkubwa ikizingatiwa maisha ya Kijijini ni magumu na hawana
vyanzo vikubwa vya mapato zaidi ya kilimo ambacho nacho kimekuwa si cha uhakika
kutokana na mvua kutokuwa za uhakika.
“Tunaomba viongozi watakaochaguliwa wahakikishe wanashughulikia
kero hii kwani kwa sasa ni muda mrefu na tumekuwa tukilalamika lakini hakuna
hatua zinazochukuliwa pia tunaomba Halmashauri itenge bajeti kwa ajili ya
mafuta ya gari hilo la wagonjwa,” alisema Rashid.
Naye mgombea Udiwani wa kata ya Kwaruhombo ramadhan mahamba
alisema kuwa kero hiyo ni kubwa kwa wanakijiji na kumwomba mgombea huyo wa
ubunge kuhakikisha nawasemea huko halmashauri ili gari hilo liwe na bajeti ya
mafuta.
Mahamba alisema kuwa mbali ya kero hiyo ya wananchi kutakiwa
kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuwekea mafuta ya kuwasafirisha
wagonjwa wanapopata rufaa kwenda hospitali kubwa pia kuna tatizo la upungufu wa
wahuduma wa afya.
Kwa upande wake Ridhiwani Kikwete alisema kuwa kero hiyo
ameisikia na mara atakapochaguliwa atahakikisha anashinikiza kutenga fedha za
mafuta kwa ajili ya vituo vya afya ili kuwaondolea mzigo wananchi.
Ridhiwani alisema kuwa utaratibu umewekwa na Halmashauri wa
bajeti ya mafuta ya magari hayo hivyo akichaguliwa hiyo ni moja ya vitu
atakavyovifuatilia kwa karibu ili kuhakikisha mafuta yanapatikana kwenye gari
hilo.
Mwisho.
NA John Gagarini, Chalinze
KIJIJI ch Kwaruhombo Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo
kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji hali inayowafanya wakazi wake
kuchota maji ya visima vya kienyeji ambavyo viko chini ya ardhi huku vingine
vikiwa na urefu wa futi 12.
Mbali ya visima hivyo kuwa na urefu mkubwa ambapo huwabidi
wachotaji wengi wao wakiwa ni wakinamama kushuka kwa kutumia ngazi pia kumekuwa
na foleni kubw ahali ambayo inawafanya wakeshe wakisubiri maji ambayo yamekauka
kutokana na hali ya kiangazi.
Moja ya wanakijiji aliyejitambulisha kwa jina la Hadija
Yusufu alisema kuwa maji ni changamoto kubwa kwao kwani wamekuwa wakitumia muda
mrefu wa kusubiria maji hasa kipindi hichi cha kiangazi pia ni hatari kwa
maisha yao kutokana na urefu wa visima hivyo.
“Tunaiomba serikali kutusaidia kupatikana maji ili
kutuondolea adha hii kwani tumeletewa maji ambapo kuna vioski kwa ajili ya
kuchota maji lakini havitoi maji hatujui kuna tatizo gani linalosababisha maji
yasitoke hivyo tumebaki tunategemea maji ya visima hivyo vya kienyeji ambavyo
navyo ni hatari kweteu,” alisema Yusufu.
Kwa upande wake mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM Ramadhan
Mahamba alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anafuatilia suala hilo
ili maji yaweze kupatikana kwa kutatua changamoto iliyopo ili maji yapatikane
na kuwaondolea kero wananchi.
Naye mgombe ubunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema
kuwa tatizo la ukosefu wa maji ni kutokana na miundombinu iliyowekwa kuwa ya
zamani hivyo kushindwa kuhimili kasi ya maji na kupasuka.
Ridhiwani alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha
miundombinu mipya ambayo ni mabomba inapatikana ili kuondoa kero hiyo
inayowanyima usingizi wananchi hao ambao hicho ni kilio chao kikubwa.
Mwisho.
Tuesday, October 6, 2015
DIWANIA AHIDI KUNUA GARI LA WAGONJWA
Na John Gagarini, Chalinze
MGOMBEA Udiwani kata ya Vigwaza Jimbo la Chalinze kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Muhsin Bharwan amesema kuwa endapo atafanikiwa
kuchaguliwa atanunua gari la kubeba wagonjwandani ya kipindi cha miezi sita kwa
ajili ya kuwapeleka wagonjwa wanaopata rufaa kwenda hospitali kubwa.
Aliyasema hayo kwenya mkutano wa kampeni ya kumnadi mgombea
Ubunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji cha Buyuni kwenye kata
hiyo na kusema kuwa gari hilo litatumika kwenye vijiji vya kata hiyo ya Vigwaza.
Bharwan alisema kuwa kutokana na kata hiyo kutokuwa na gari
la wagonjwa wakazi hao wamekuwa wakipata
taabu kuwapeleka wagonjwa wao wanaopata rufaa kwenda kwenye hospitali kubwa
kama vile Tumbi au Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Endapo nitafanikiwa kuchaguliwa kwenye nafasi hii ya Udiwani
ndani ya miezi sita nitahakikisha nimenunua gari la kubeba wagonjwa, tutamwomba
mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupata msamaha wa kodi toka
serikalini ili kufanikisha kupatikana gari hilo,” alisema Bharwan.
Alisema kuwa kwa kushirikiana na Wanakijiji hao atahakikisha
ujenzi wa zahanati unakamilika ili waanze kupata huduma za afya kijijini hapo
badala ya kupata huduma hiyo mbali kwani kwa sasa hakuna huduma hiyo kutokana
na kukosa zahanati.
“Sera inasema kila Kijiji lazima kiwe na zahanati na kata
inakuwa na kituo cha afya hivyo tutahakikisha tunatimiza hilo ili kusogeza
huduma za afya kwa wananchi,” alisema Bharwan.
Kwa upande wake Ridhiwani Kikwete alisema kuwa moja ya
vipaumbele vyake ni pmaoja na upatikanaji wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wahudumu wa afya wanapatikana.
Ridhiwani alisema kuwa pia upatikanaji wa madawa, vifaatiba,
pamoja na ujenzi wa nyumba za wahudumu wa afya ili waishi kwenye vituo vyao vya
kazi kwa lengo la kutoa huduma kwa urahisi.
Naye mkazi wa Kijiji hicho Pamilasi Sambana alisema kuwa
huduma hizo za kiafya zikipatikana itawasaidia kukabiliana na matatizo
yanayotokana na umbali wa upatikanaji wa huduma hizo.
Sambana alisema kuwa huduma za afya ni moja ya vilio vya
wananchi na mara anapotokea mgonjwa inakuwa ni taabu sana hivyo wanawaomba
wagombea hao kutimiza ahadi zao ili kuwapunguzia adha ya kupata huduma hizo.
Mwisho.
Na John Gagarini, Chalinze
UTUNGWAJI wa sheria ndogondogo kwenye Kijiji cha Malivundo
kata ya Pera kwenye Jimbo la Chalinze kumesaidia kupunguza migogoro baina ya
wakulima na wafugaji ambayo ilikuwa imekithiri katika Kijiji hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari moja ya wanakamati ya
maridhiano baina ya wakulima na wafugaji ya Kijiji hicho Charles Antony alisema
kuwa tangu kuundwa kamati hiyo miezi minne iliyopita migogoro imepungua kwa
kiasi kikubwa.
Antony alisema kuwa mkutano wa Kijiji ulipitisha sheria ya
kumtoza mfugaji gunia nane za mahindi kwa hekari moja endapo ataingiza mifugo kwenye shamba la
mkulima ambalo lina mazao na kwa shamba ambalo limeandaliwa halina mazao
atatozwa kiasi cha shilingi 50,000 kwa hekari moja na 40,000 kwa shamba ambalo limevunwa mazao.
“Sheria hii iliridhiwa na wakulima na wafugaji licha ya kuwa
tatizo kubwa lipo kwa wafugaji ambao wamekuwa wakilisha mifugo kwenye mashamba
ya wakulima hali ambayo ilikuwa inasababisha migogoro ya mara kwa mara lakini
toka sheria hii imepitishwa na Kijiji matatizo hayo yamepungua,” alisema
Antony.
Alisema kuwa endapo mlalamikiwa anakataa kutekeleza agizo la
kamati suala hilo linapelekwa ngazi ya kata ambako nao husisitiza mlalamikiwa
kulipa faini hiyo mara baada ya kamati kupita kwenye eneo ambalo limefanyiwa
uharibifu.
“Kamati hii inaundwa na watu 10 wakulima watano na wafugaji
watano ambao huangalia ukubwa wa tatizo kisha hutoa maamuzi juu ya uharibifu
uliofanywa lakini pia pande mbili zinazohusika nazo huruhusiwa kukaa na
kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo,” alisema Antony.
Ashura Ramadhan alisema kuwa kwa sasa angalau mazao yao
yanaweza kukua bila ya tatizo lolote tofauti na ilivyokuwa awali ilikuwa ni
ugomvi mkubwa kati ya wakulima na wafugaji lakini kwa sasa angalau amani
inapatikana kutokana na sheria hizo.
Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Pera kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM)Lekope Laini alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anatumia
taaluma yake ya sheria kukabili migogoro ya wakulima na wafugaji pia kuwaunganisha
ili waishi kama ndugu.
Naye mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani
Kikwete alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha mpango wa matumizi bora
ya ardhi unawekewa mkazo ili kuwe na maeneo ya wakulima na wafugaji kupunguza
migogoro hiyo.
Mwisho.
Na John Gagarini, Chalinze
WAKINAMAMA wa Jamii ya wafugaji kwenye Kijiji cha Wafugaji
cha Chamakweza wameiomba serikali kuwapatia matenki makubw aya kuhifadhia
maziwa pamoja na soko la uhakika la kuuza maziwa yao.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge Jimbo
la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete Anastazia
Masaka alisema kuwa maziwa wanayozalisha ni mengi lakini hawana sehemu ya
kuhifadhia pamoja na soko la uhakika.
Masaka alisema kuwa wanaiomba serikali kuwapatia matenki hayo
ili waweze kuhifadhi maziwa yao ili yasiweze kuharibika wakati yakisubiri
kusafirishwa au kuwasubiri wanunuzi wa maziwa hayo ambayo yanapatikana kwa
wingi kwenye kijiji chao ambacho ni cha wafugaji.
“Maziwa ni mengi lakini tunataabika na soko pamoja na sehemu
ya kuhifadhia hivyo tunaiomba serikali kupitia mgombea Ubunge kutusaidia kupata
matenki ya kuhifadhia pamoja na soko la uhakika kwani soko likiwa kubwa vijana
wetu watapata ajira kupitia maziwa,” alisema Masaka.
Alisema kuwa wakipata ufumbuzi wa masuala hayo basi itakuwa
ni ufumbuzi wa changamoto wa namna ya kuhifadhi pamoja na soko la kuuza bidha
hiyo ambayo inapendwa na watu kutokana na umuhimu wake kiafya.
Kwa upande wake Ridhiwani Kikwete alisema kuwa endapo
atafanikiwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo atahakikisha soko pamoja na matenki
hayo vinapatikana ili kuwaondolea adha ya kuhifadhi maziwa yao pamoja na soko.
Ridhiwani alisema kuwa kwa kupitia umoja wao wa wauzaji
maziwa atahakikisha anawaletea wanunuzi wa maziwa pia wanawezeshwa kuptia fedha
ambazo zitatolewa kwa kila Kijiji kiasi cha shilingi milioni 50.
Naye mgombea Udiwani Lekope Laini alisema kuwa endapo
atachaguliwa atahakikisha anakabiliana na changamoto za akinamama wa kifugaji
ili nao waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya
kufanya shughuli zao.
Mwisho.
Na John Gagarini, Bagamoyo
KATIKA kuhakikisha kurahisisha utendaji kazi hasa katika kipindi hichi cha uchaguzi CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani kimetoa pikipiki 12 kwa makatibu kata kwenye Jimbo la Bagamoyo ili kuwaondolea tatizo la usafiri wakati wakutimiza majukumu yao.
Akikabidhi pikipiki hizo mwenyekiti wa CCM wilayani hapo Maskuzi alisema walikuwa wakikabiliwa na changamoto
ya ukosefu wa usafiri kwa makatibu hao hivyo kushindwa kutekeleza kikamilifu
shughuli za chama.
Maskuzi alisema kuwa lengo lingine ni kuwawezesha makatibu kata hao
kuweza kusimamia majukumu yao kikamilifu pamoja na uhai wa chama na kurahisisha
shughuli hasa katika kipindi hichi cha uchaguzi.
“Utoaji wa pikipiki hizi zenye thamani ya shilingi milioni 24 kwa makatibu wa kata ni muendelezo ambapo awali kwenye awamu ya kwanza tulitoa
pikipiki 15 katika Jimbo la Chalinze na sasa kumalizia na jimbo la Bagamoyo,”
alisema Maskuzi.
Alisema kuwa kwasasa anaamini watendaji hao watafanya kazi zao pasipo
usumbufu kwani tatizo kubwa lilikuwa ni ukosefu wa usafiri wa uhakika
wakutembelea maeneo mbalimbali ya kazi.
“Pikipiki hizi tunazitoa sio kwa shughuli nyingine ila ni kwa ajili ya
kutekeleza shughuli za kichama kwa kutembelea matawi,kusimamia uhai wa chama na
kutekeleza majukumu yatakayotakiwa kufuatilia wakati huu wa kuelekea kwenye
uchaguzi mkuu”alisema Masukuzi.
Kata zilizopatiwa pikipiki hizo ni pamoja na Mapinga, Kerege, Zinga, Kilomo,
Yombo, Dunda, Magomeni, Kisutu na Nianjema, Makurunge na Fukayosi na pikipiki
moja itakuwa kwa ajili ya mtendaji mkuu CCM wilayani hapo.
Kwa upande wake katibu wa CCM kata ya Kisutu Buruhani Setebe alisema
amepokea pikipiki na amekishukuru chama kwa kutambua changamoto yao hivyo
atahakikisha anaitunza pikipiki hiyo.
Naye katibu wa CCM kata ya Mapinga ,Muhdin Mipango alisema awali
walikuwa wakipata shida katika utendaji wa kazi zao ikiwa ni pamoja na
kutembelea kwa miguu ama kukodi pikipiki ili kwenda kutembelea matawi.
Mwisho.
Sunday, October 4, 2015
MCH MTIKILA AFARIKI AJALINI
Na John Gagarini, Chalinze
MWANASIASA Mkongwe hapa nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama ChaDemocratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila (62) amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Pwani Jafary Mohamed alisema kuwa tukio hilo lilitokea huko Msolwa Barabara Kuu ya Dar es Salaam Morogoro wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamanda Mohamed alisema kuwa ajali hiyo ilitokea saa 11:45 Alfajiri wakitokea mkoani Njombe wakiwa na gari aina ya Toyota Corola lenye namba za usajili T189 AGM lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye George Steven (31) maarufu Ponera mkazi wa Mbezi Jijini Dar es Salaam.
"Gari hilo likiwa na abiria watatuakiwemo marehemu mkazi wa Mikocheni B, lilikuwa kwenye mwendo wa kasi liliacha njia na kuserereka pembeni mwa barabara kasha kupinduka ambapo marehemu alirushwa nje ya gari na kupoteza maisha papo hapo,"alisema Kamanda Mohamed.
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na dereva wa gari hio, Mchungaji Patrick Mgaya (57) na Ally Mohamed (42) wote wakazi wa Jijini Dar es Salaam ambao wote walikimbizwa kweye hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi pamoja na kuhifadhi mwili wa marehemu.
"Chanzo caha ajali hiyo ni mwendo wa kasi wa dereva huyo ambao ulisababisha ashindwe kulimudu gari hilo na kuserereka pembeni ya barabara kasha kupinduka na kupelekea kifo hico cha kusikitisha cha mwanasiasa huyo," alisema Kamanda Mohamed.
Hata hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zilisemakuwa mara baada ya ajali hiyo wahanga hao hawakuweza kupata msaada kwani eneo hilo halina makazi ya watu.
mwisho.
Friday, October 2, 2015
ADHA YA MAJI KIJIJI CHA GONGO KATA YA MKANGE JIMBO LA CHALINZE WILAYA YA BAGAMOYO PWANI
Na John Gagarini, Mkange
WANANCHI wa Kijiji cha Gongo kata ya Mkange wilayani Bagamoyo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ambapo huweka foleni ya kuchota maji kwenye kisima kilichopo kijijini hapo baada ya wiki mbili.
Kutokana na usosefu huo wa maji wananchi hao wamekuwa wakinunua maji ya bomba ndoo ya lita 20 kati ya shilingi 1,000 na shilingi 1,500 maji ambayo huuzwa kwenye magari au pikipiki hivyo kuwafanya wajikute hawapati maendeleo kutokana na gharama kubwa kuzitumia kununulia maji.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete, kwenye kata ya Mkange mwananchi wa Kijiji hicho Hungilo Nyoka alisema kuwa maji yamewafanya washindwe kupata maendeleo.
Nyoka alisema kila kaya inatakiwa ichote madumu manne ili angalau kila mmoja apate baada ya hapo maji hukatika ambapo inatakiwa mtu asubirie tena na mzunguko huo hufanya foleni ya mtu mmoja kufikiwa tena baada ya wiki mbili kwani hapa kuna wananchi 1,690.
Alisema changamoto kubwa kwao ni maji ambayo yamekuwa yakiwafanya washindwe kufanya shughuli za maendeleo ipasavyo kwani hata wakipata fedha kutokana na shughuli zao fedha zote huishia kununulia maji.
“Tunawaomba wahusika kutuangalia kwa jicho la huruma maji kwetu ni kikwazo cha kupata maendeleo kwani hata ukipata fedha kiasi gani zote zinaishia kwenye maji hivyo tunaomba tuchimbiwe kisima kwani kilichopo maji ni kidogo sana yanatoka kila baada ya saa moja yanakatika,” alisema Nyoka.
Aidha alisema kuwa maji wanayokunywa ni ya bomba lakini yanatoka vijiji jirani vya Matipwili ambako kuna umbali wa kilomita 11 na kijiji cha Mkange kilomita tisa na alisema kuwa chanzo cha maji ya kisima kutotoka ipasavyo ni kwamba waliochimba kisima hawakuchimba hadi kuuukuta mwamba ambapo chini ya mwamba ndiyo kuna maji mengi.
“Tunaomba wadau wa masula ya maendeleo kutusaidia kuweza kupata maji kwani tunashindwa hata kujiletea maendeleo kutokana ukosefu wa maji na wkati mwingine watoto hushindwa kwenda shule endapo maji yanakuwa ya shida kwani hawawezi kwenda wachafua kwani mimi kwa siku hutumia madumu matatu hadi matano kwa siku,” alisema Nyoka.
Kwa upande wake mgombea udiwani kupitia CCM Injinia Juma Mgweno alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa sana lakini atahakikisha maji yanapatikana kwa kuita wadau mbalimbali ili waweze kuwachimbia kisima.
Naye mgombea wa Ubunge kupitia CCM Ridhiwani Kikwete alisema kuwa visima viwili vilivypo kijiji hapo havitoi maji ambapo kimoja kinahitaji pampu ambayo imeharibika atahakikisha inapatikana mpya ili kuwaondolea kero wananchi wa kijiji hicho.
Ridhiwani alisema kuwa mbali ya kuhakikisha pampu mpya inapatikana pia kuna mradi mwingine wa mjai toka Matipwili na ule wa Wami Chalinze atahakikisha maji yanafika kwani mradi huo utavifikia vijiji na vitongoji ambavyo havikupata maji katika awamu mbili zilizopita vitafikiwa na awamu hii.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)