Monday, September 28, 2026

*MAKURUNGE JOGGING YAZINDULIWA RASMI KWA KISHINDO TAREHE 26/09/2026 VIONGOZI WA SERIKALI WASHIRIKI*






Kikundi cha Makurunge Jogging kilichopo kata ya Makurunge Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani kimezinduliwa rasmi kwa kishindo na Viongozi wa serikali mnamo tarehe 26/09/2026 ambayo pia ni siku ya juma mosi ya mwisho wa mwezi usafi hufanyika.

Miongoni mwa viongozi wa serikali Ndg Wensaka p Mnane Mwenyekiti kitongoji Mkwajuni, Ndg Semwana Mwenyekiti kitongoji Gezaulole, Mhe Hashim Chochoro Diwani kata ya Makurunge, Katibu Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Mkoa wa Pwani Salehe Miraji Mheta, Polisi kata Makurunge Inspecta Fussy, polisi mtaa mikoroshini Stshen Sargent Raya na viongozi wengine.

Katika hafla hiyo wana jogging pamoja na viongozi kwenye uzinduzi huo wameweza kufanya usafi katika maeneo, zahanati ya kata ya Makurunge, Ofisi ya kitongoji cha Gezaulole pamoja na Ofisi ya Mtendaji kata Makurunge na mara baada ya usafi viongozi wamekua na machache ya kusema. 

Akizungumza Diwani kata ya Makurunge Mhe Hashim chochoro alipongeza ubunifu wa Jogging hiyo yenye lengo la "kulinda usalama wa Mtoto" kwa kutoa elimu kwa jamii na kuhamasisha suala zima la usafi hususuni wakati huu kutokana taarifa zilizopo kuhusu Mvua za ELI NINO, pamoja na hayo Diwani aliahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa wana jogging.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti kitongoji cha Mkwajuni Ndg Wensaka P Mnane amewapongeza  Askari waliopo kata ya Makurunge Inspecta Fussy, na polisi mtaa mikoroshini Stsheni Sargent Raya pamoja na wana jogging wote kwa ushirikiano mkubwa waliouweka wenye lengo la kutengeneza makurunge iliyo bora.

Kwa kuhitimisha Uongozi wa Kikundi cha Makurunge jogging ukiongozwa na Mwenyekiti wa jogging Ndg Neemia, pamoja na Katibu wa Joging Ndg Dotto Maulid Uliwashukuru Viongozi wa serikali kwa kuwaunga mkono katika jitihada walizo zipambania na kuahidi kua Jogging Makurunge yenye lengo la "kulinda haki za mtoto" itaendelea kuwa imara na kushiriki shughuli zote za kijamii wakati wote.

JOGGING MAKURUNGE
"LINDA HAKI YA MTOTO"

No comments:

Post a Comment