MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge leo Aprili 26, 2023 amezindua Daraja la Mipeko iliyopo Barabara ya Mwanambaya lenye thamani ya shilinigi milion 214.
Kunenge akisalimia wananchi wa Mipeko amepongeza Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Maendeleo ambayo yanamgusa mwanachi wa kawaida.
Ameeleza kuwa Rais alipofanya ziara Mkoani Pwani alisema nia yake ya kuhakisha Mkoa unapata Miundombinu ya yote muhimu ya Afya, Elimu, Maji, Nishati, Barabara.
Aidha amesema kuwa mkoa huo una Mtandao wa Barabara wa km 6629 zinazohudumiwa na TANROADS na TARURA.
Ameongeza kuwa bajeti ya kutekeleza shughuli za Barabara kwa mwaka 2021/22 ilikuwa ni bilion75.5 na kwa mwaka 2022/23 imeongezwa kufikia bilion 81.
Amewataka Wananchi wa eneo hilo kulinda Daraja hilo na kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mkuranga kupanga Mji wa Mkuranga kwa kuwa Mji huo unakuwa kwa kasi.
Kunenge ameeleza Serikali inafanyia kazi maombi ya Wananchi hao ya kujengewa Kituo cha Afya, kupelekewa Umeme na ujenzi wa Daraja.
No comments:
Post a Comment