Tuesday, April 18, 2023

TANZANIA KUBORESHA MAWASILIANO

 


SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu bora ya mawasiliano yenye kutumia Teknolojia ya kisasa ambayo italeta tija na ufanisi katika kuongeza uzalishaji na ujenzi wa uchumi na kuimarisha usalama na ulinzi wa Taifa.

Hayo yamesemwa Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye katika hafla ya utiaji saini kati ya TTCL na HUAWEI kuhusu upanuzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 23  uliyofanyika Jijini Dodoma.

Nape amesema zaidi ya  shilingi  bilion 37 zitangharimu ujenzi wa kilometa 1,520 ambazo zitaunganisha Wilaya 23 katika upanuzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano kati ya shirika la mawasiliano Tanzania na kampuni ya HUAWEI International.

Amesema kuwa mradi huu unaenda kuleta mageuzi makubwa yakiwemo kukuza matumizi ya tehama Wilaya kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato pamoja na kuleta fursa kwa wananchi kiuchumi.



Awali kwa upande wake Mkurugezi mkuu wa TCCL  mhandisi Peter Ulanga 

Amesema mradi huu utatoa fursa nzuri kwa wizara , Taasisi za umma na Taasisi binafsi kufikisha huduma Zao kwa wateja na watumiaji wao kwa haraka na wakati kwa kuwa mkongo wa Taifa utakuwa na uwezo mkubwa wa kubeba taarifa za kutuma kwa haraka.

No comments:

Post a Comment