Wednesday, April 5, 2023

WATAKIWA KUPINGA UKATILI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKUU wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaasa wananchi wa Kata ya Chang'ombe kukubali kubadilika kupinga Ukatili kwa kushirikiana pamoja ili Mkoa wa Dodoma kuwa wa Mfano kwa maendeleo ya Taifa. 

Ameyasema hayo aliposhiriki katika Kongamano la Kupinga Ukatili Mkoa wa Dodoma lililoandaliwa na kamati ya kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na Msaada wa Kisheria, kupitia kikundi cha Wanawake na Samia na kusikiliza kero za wananchi wake katika Mtaa wa Mazengo Chang'ombe. 

Senyamule amesema kuwa Chang'ombe bila vitendo vya kikatili inawezekana na kutoa rai kwa wazazi na walezi wa Kata ya Chang'ombe kutoficha vitendo viovu vya watoto na vijana katika jamii inayowazunguka ili jitihada za pamoja za kutokomeza vitendo vya kikatili ziweze kufanikiwa.

Aidha, Mhe. Senyamule ameendelea kumshukuru Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuimarisha Mkoa wa Dodoma kwa miradi mikubwa ya kimkati ambayo ni fursa kwa vijana ambayo ni fursa kwao kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kwani wana sehemu ya kupeka nguvu kazi zao ili kujiepusha na tabia zisizo na Maadili.

"Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ningetamani kila Kata, Mtaa, Kaya na kila nyumbani isiwe na mhalifu wala mtu yeyote anaefanya ukatii na unyanyasaji wa kijinsia, lakini itawezekana kama sisi wananchi tutaamua kuungana na juhudi na dhamira nzurii za Serikali 

"Vijana mjipange kubadilika sisi kama Mkoa tunadhamira njema na kizazi cha nchi hii, ni wakati sahihi wakujiwekea sheria ambazo tutasimamia wenyewe zinazohusu Ukatili wa Kijinsia kwani inawezekana kubadilika kusiwe na vijana vibaka, wezi ili kupongeza wale wenye Maadili mazuri na kuwa mfano wa kuigwa "Amesema Senyamule. 

Naye Mwanakamati ya kupinga Ukatili Fatuma Madidi ametoa elimu juu ya Ukatili wa nafsi, watoto, vijana, wazee na Wanawake ili kuweza kutambua Madhara ya Ukatili kwa Ujumla na kuendelea kujihadhalisha .

Kwa Upande wake Diwani wa Chang'ombe Bw. Bakari Fundikira amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ujio wake katika kata yake na kuahidi kuendelea kutekeleza maelekezo yake.

No comments:

Post a Comment