Na Mwandishi Wetu Dodoma
KATIBU Mtendaji Mkuu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Beng'i Issa amewataka wananchi kuacha kukopa fedha bila malengo badala yake watumie mikopo kama fursa kujiletea maendeleo.
Issa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita.
Amesema kupitia Baraza la Uwezeshaji kiuchumi wameunda njia mbalimbali ambazo zitawasaidia wananch kunufaika na Baraza hilo la kuwezesha wananchi kiuchumi ikiwemo mifuko ya mikopo ya jamii ambayo kwa sasa kuna jumla ya mifuko 72 ili kuwanufaisha wanchi wote walio katika mifuko hiyo ya jamii.
"Hadi sasa imewezesha kuwapatia ya zaidi ya shilingi bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini na inasimamia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika mikoa yote 26 na Halmashauri zote nchini.
Aidha amesema kuwa Watanzania zaidi ya 83,000 wamepata ajira za kimkakati na Baraza huandaa makongamano kwa ajili ya maonesho kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment