Na John
Gagarini, Kibaha
MKUU wa Mkoa
wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka wakuu wapya wa wilaya wlioteuliwa na
Rais Dk John Magufuli mkoani humo kuinua pato la wananchi wa mkoa huo kutoka
milioni 1.2 kwa mwaka hadi milioni 3 kwa mwaka.
Aliyasema hayo
jana mjini Kibaha wakati akiwaapisha wakuu hao wa wilaya wapya na kusema kuwa
pato la mwananchi wa mkoa wa Pwani liko chini sana licha ya kuwa na fursa
mbalimbali za kipato.
Ndikilo alisema
kuwa kutoakana na pato hilo la wananchi kuwa dogo kiasi hicho hata mchango wa
mkoa kwa Pato la Taifa ni dogo sana la asilimia 1.8 jambo ambalo linapaswa
kuwekewa mkakati wa kupandisha pato hilo ili liwe na mchango mkubwa kwa
mwananchi na Taifa kwa ujumla.
“Nawapongezeni
kwa kuchaguliwa kwenye nafasi hizi na mkoa tayari umeandaa mpango kazi wake kwa
ajili ya kuinua pato la mwananchi hivyo mnapaswa kuweka vipaumbele ambavyo
vitasaidia kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya unayoongoza,” alisema Ndikilo.
Alisema kuwa
hakuna sababu ya mkoa kuendelea kuwa na pato dogo huku kukiwa na vyanzo vingi
vya mapato ikiwa ni pamoja na rasilimali mbalimbali kama vile uvuvi, kilimo,
korosho, maliasili ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama na madini mbalimbali.
“Mfano ni
majumba mengi yanayojengwa Dar es Salaam kokoto na mawe yanatoka mkoa wa Pwani
hivyo hakuna sababu ya kuwa maskini tuna zao la korosho ambapo kwa msimu
uliopita wakulima waliuza korosho zenye tahamani ya shilingi bilioni 18,”
alisema Ndikilo.
Aliwataka wahakikisha
wanawajibika na kutowalea watumishi ambao ni kikwazo na wenye urasimu wa
kuwahudumia wananchi ambao hufika ngazi ya mkoa kulalamika ili hali ngazi za
chini kuna watendaji ambao wangeweza kutatua matatizo hayo.
“Changamoto
ni nyingi ikiwa ni pamoja na suala la ulinzi na usalama, wahamiaji haramu,
matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi nisingependa mambo haya yatokee tena
hakikisheni mnatimiza wajibu wenu na kuwaondolea kero wananchi,” alisema
Ndikilo.
Kwa upande
wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid
Mwanga alisema kuwa moja ya changamoto ambazo atakabiliana nazo ni pamoja
na wahamiaji haramu kw akudhibiti bandari 19 ambazo zimekuwa ni njia ya
wahamiaji hao haramu.
Naye Asumpter
Mshama alisema kuwa moja ya mambo atayapaa kipaumbele ni kuhakikisha fedha kwa
makundi ya vijana na akinamama asilimia 10 zinatoka ili wananchi waweze kujenga
uchumi wao na ule wa Taifa.
Wakuu wapya
walioapishwa jana ni pamoja na Shaibu Nunduma wilaya ya Mafia, Filberto Sanga
Mkuranga, Gulamu Kifu wilaya ya Kibiti, Asumpter Mshama wilaya ya Kibaha, Juma
Njwayo wilaya ya Rufiji na Majid Mwanga wilaya ya Bagamoyo huku Happyness
William hakuweza kuapishwa kutokana na dharura.
Mwisho.
Mkuu mpya wa wilaya Rufiji Juma
Njwayo kulia akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo
wakati wakiapishwa wakuu wa wilaya za mkoa huo kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu
wa mkoa huo.
|
No comments:
Post a Comment