Na John
Gagarini, Kibaha
WAKAZI wa
Mtaa wa Machinjioni Loliondoa au Sagulasagula waliobomolewa nyumba zao na
Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani kwa tuhuma za kujenga nyumba kwenye
eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa soko wamekanusha kuapaka kinyesi na kuvunja
vioo vya ofisi ya kata ya Maili Moja.
Akizungumza na
waandishi wa habari moja ya wahanga wa tukio la bomoa bomoa hiyo iliyofanyika
Juni 16 na 17 mwaka huu ambapo watu hao walifanya uharibifu huu siku moja baada
ya bomobomoa hiyo huku jumla ya nyumba 18 zilibomolewa, Said Tekelo amesema
kuwa wao hawahusiki na tukio hilo na wamesikitishwa na kitendo hicho.
Tekelo amesema
kuwa kitendo hicho kimefanywa na watu ambao walikuwa na malengo yao na hawaungi
mkono watu waliofanya uharibifu huo kwani ni tukio ambalo ni kinyume cha sheria
na hakistahili kuunga mkono.
Amesema kuwa
wao kama wahanga wa bomobomoa hiyo hawawezi kufanya hivyo kwa sababu bado wako
katika kutafuta haki yao waliyoipoteza baada ya nyumba zao kubomolewa pasipo
kupewa fidia yoyote hivyo wasingeweza kufanya uharibifu.
Aidha amesema
kuwa vi vema vyombo vya kisheria vikafanya yake ili kubaini wale waliofanya
hivyo na kuwachukulia hatua kazi za kisheria kwani hao ni wahalifu kama
wahalifu wengine na hawahusiani na waliobomolewa nyumba zao.
Amebainisha kuwa
suala lao liko mahakamani tangu zoezi la kubomolewa nyumba zao lilipofanyika na
hawaungi mkono watu waliofanya hivyo na wanawalaani vikali watu hao ambao
wamejificha kwenye mwamvuli wa uhalifu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment