BRAILO MEDIA

HABARI ZETU

Saturday, June 18, 2016

BOMOABOMOA YALIZA WENGI KIBAHA

Na John Gagarini, Kibaha
ZOEZI la bomoabomoa kwenye eneo ambalo Halmashauri ya Mji wa Kibaha linadai kuwa wananchi hao walijenga kinyume cha taratibu limewaacha wakazi 55 kwenye Mtaa wa Machinjioni, kata ya Mailmoja Kibaha mkoani Pwani wakiwa hawana mahali pa kuishi baada ya kutekeleza zoezi hilo.

Wakazi hao wakizungumzia bomoa bomoa hiyo akiwemo Said Tekelo, Sauda Lameck na Ally Saidi walisema bomoa bomoa hiyo imewaathiri kwa kiasi kikubwa kwani hawana pa kuishi,kuhifadhiwa kwa majirani na jamaa na wengine kuamua kwenda kuishi kwenye nyumba za kupanga .

Walisema kuwa kitendo walichofanyiwa ni kimewaumiza kutokana na kuwarudisha nyuma kimaendeleo huku wengine waliovunjiwa nyumba zao wamejikuta wakiibiwa baadhi ya vitu vyao na watu wasio wema.
“Tulipewa taarifa ya tukio hilo ilishatolewa mapema ambapo tulienda mahakamani kukata rufaa lakini tunashangaa kuona greda limeletwa na kuanza kubomoa nyumba zetu kabla ya shauri la mwisho,” Walisema.

Kwa upande wake ofisa habari wa halmashauri ya Mji wa Kibaha,Innocent Byarugaba alisema zoezi la bomoa boma limefanyika kwa siku mbili kuanzia june 15 na june 16.

Byarugaba alisema zoezi limefanyika kwa kufuata taratibu kwani kuanzia tarehe 31 may wakazi hao wote walipewa hati za kuwataka wabomoe wenyewe na kila mmoja katika nyuma zote 55 alipatiwa hati hiyo kwa jina lake.

Byarugaba alisema baada ya siku 16 walivunja nyumba hizo ambapo kisheria unapompa mtu hati ya kuvunja nyumba yake mwenyewe na badala yake kumvunjia kisheria ya mipango miji kifungu 74 kifungu kidogo cha 4,na sheria ya serikali za mitaa kifungu cha 139 kifungu kidogo cha 3 anatakiwa kulipia hizo gharama.

Alisema eneo hilo lilimilikishwa watau watano ambapo mwaka 2009 walitakiwa kuondoka na kulipwa fidia zao na kuanzia hapo watu wengine wasio waaminifu waliwauzia wengine kinyume na tararibu.
Eneo hilo lilipimwa kihalali kama  eneo la viwanda na watu watano walimilikishwa ambapo mwaka 2006 miliki ya viwanja hivyo ilifutwa kwa tangazo la serikali ili kupisha uendelezaji wa kitovu cha Mji na ujenzi wa soko .

Mwisho.



Posted by BRAILO MEDIA at 2:12 PM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Translate

Followers

Blog Archive

  • ►  2025 (74)
    • ►  June (7)
    • ►  May (12)
    • ►  April (11)
    • ►  March (19)
    • ►  February (10)
    • ►  January (15)
  • ►  2024 (210)
    • ►  December (19)
    • ►  November (5)
    • ►  October (8)
    • ►  September (6)
    • ►  August (25)
    • ►  July (23)
    • ►  June (15)
    • ►  May (12)
    • ►  April (27)
    • ►  March (33)
    • ►  February (27)
    • ►  January (10)
  • ►  2023 (322)
    • ►  December (7)
    • ►  November (11)
    • ►  October (17)
    • ►  September (38)
    • ►  August (62)
    • ►  July (51)
    • ►  June (34)
    • ►  May (17)
    • ►  April (13)
    • ►  March (36)
    • ►  February (26)
    • ►  January (10)
  • ►  2022 (31)
    • ►  December (4)
    • ►  November (16)
    • ►  October (10)
    • ►  May (1)
  • ►  2019 (1)
    • ►  September (1)
  • ►  2017 (75)
    • ►  December (2)
    • ►  November (9)
    • ►  October (16)
    • ►  September (3)
    • ►  August (15)
    • ►  July (13)
    • ►  June (2)
    • ►  April (1)
    • ►  March (8)
    • ►  February (2)
    • ►  January (4)
  • ▼  2016 (162)
    • ►  December (9)
    • ►  October (2)
    • ►  September (4)
    • ►  August (14)
    • ►  July (17)
    • ▼  June (18)
      • WAKANUSHA KUPAKA KINYESI NA KUVUNJA OFISI YA KATA
      • ZEGERENI KUJENGA SHULE YA MSINGI
      • MILIKINI MAENEO KIHALALI KUEPUKA MIGOGORO YA ARDHI-RC
      • KITONGOJI CHA MWEMBEBARAZA KUPATA MAJI KARIBUNI
      • KITONGOJI CHA MWEMBEBARAZA KUPATA MAJI KARIBUNI
      • MWENYEKITI WA MTAA AWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOFANYA...
      • SIDO YATUMIA DOLA MILIONI 2
      • WAVUNJUA VIOO VYA MADIRISHA WAPAKA KINYESI OFISI Y...
      • BOMOABOMOA YALIZA WENGI KIBAHA
      • MIGOGORO YA NDOA ISIWANYIME HAKI ZA MSINGI WATOTO
      • WATATU WASHIKILIWA KWA MAUAJI YA DEREVA WA NOAH
      • RC ATAKA MKATABA WA UWEKEZAJI KUPITIWA UPYA
      • WATAKA TAARIFA KUHUSU ENEO LA UWEKEZAJI BAADA YA M...
      • WAWEKEZAJI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUDUM...
      • TCRA YATOA MAFUNZO KUHUSU KUFUTWA SIMU FEKI
      • JUMUIYA YA WAZAZI YASISITIZA UBORA WA ELIMU CHUO C...
      • WATAKA TAARIFA RASMI MRADI WA MIWA KUFUTWA
      • WAWEKEZAJI WADHIBITI USALAMA WA NCHI
    • ►  May (34)
    • ►  April (14)
    • ►  March (16)
    • ►  February (21)
    • ►  January (13)
  • ►  2015 (106)
    • ►  December (14)
    • ►  November (1)
    • ►  October (15)
    • ►  September (12)
    • ►  August (6)
    • ►  July (11)
    • ►  June (3)
    • ►  May (7)
    • ►  April (7)
    • ►  March (5)
    • ►  February (8)
    • ►  January (17)
  • ►  2014 (117)
    • ►  December (21)
    • ►  November (10)
    • ►  October (13)
    • ►  September (7)
    • ►  August (16)
    • ►  July (19)
    • ►  June (6)
    • ►  May (14)
    • ►  April (6)
    • ►  January (5)
  • ►  2013 (138)
    • ►  December (11)
    • ►  November (6)
    • ►  October (1)
    • ►  September (5)
    • ►  August (6)
    • ►  July (16)
    • ►  June (3)
    • ►  May (11)
    • ►  April (9)
    • ►  March (16)
    • ►  February (26)
    • ►  January (28)
  • ►  2012 (16)
    • ►  December (16)
Powered By Blogger

Pages

  • HABARI

About Me

BRAILO MEDIA
View my complete profile
GAGARINI. Picture Window theme. Powered by Blogger.