Na John Gagarini, Kibaha
SERIKALI na Bodi ya Mikopo Nchini (TCU)
imeshauriwa kuviingiza kwenye mpango wa mikopo wanafunzi wanaosoma Vyuo vya Kati
kama ilivyo kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani Abdul Sharifu wakati mkutano wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo
vya Juu wa (CCM).
Sharifu alisema kuwa wanafunzi hao ni
sawa na wale wa vyuo vikuu na wengine wanatoka kwenye mazingira magumu na
wanahitaji mikopo ili waweze kupata elimu ya juu.
“Hali ya sasa ni ngumu na wazazi ni
wale wale wanahitaji kupunguziwa mzigo wa kulipa ada ambazo ni kubwa hivyo
tunaona kuwa kuna haja ya serikali kuviingiza na vyuo vya kati kwenye mpango wa
kutoa mikopo kwa wanafunzi,” alisema Sharifu.
Alisema kuwa kwa kuwa nchi imeamua
kuwekeza kwenye elimu kwa lengo la kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu bora
hadi kufikia elimu ya juu ambayo ndiyo inaweza kumsaidia mtoto.
“Kwa sasa elimu ya juu ndiyo
inayotakiwa tofauti na elimu ya kawaida ambayo si ya juu ambayo kwa sasa haina
nafasi ya muhitimu kupata ajira hivyo kulazimisha watu wapate elimu ya juu,”
alisema Sharifu.
Aidha alisema kuwa shirikisho hilo ni
mboni ya chama na linafanya kazi kubwa ya kukijenga chama kwani hapo ni tanuru
la kuandaa viongozi wa baadaye wa kukiongoza chama pamoja na nchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Kibaha Maulid Bundala ambaye
alimwakilisha mwenyekiti wa Mkoa Mwinshehe Mlao alikuwa mgeni rasmi kwenye
mkutano huo alisema kuwa Shirikisho la Vyuo Vikuu la CCM linafanya kazi kubwa ya
kukitetea chama.
Bundala alisema kuwa CCM imeleta
ukombozi ndani ya nchi na ni chama kikongwe hivyo kwa wanavyuo waliojiunga na
shirikisho hilo wako sehemu salama kwani mawazo yao yataleta manufaa kwa nchi.
Aidha alisema kuwa nchi kwa sasa ina
hitaji kuongozwa na wasomi hivyo wasomi hawa wataleta mabadiliko na chama kiko
tayari kubadilika na wao wananafasi ya kumshauri Rais na wao ndiyo
watakaoliinua taifa.
Naye naibu katibu mkuu wa shirikisho
hilo Siraji Madebe alisema kuwa shirikisho lao linakabilia na changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na wancahama wake wale wa vyuo vya kati
kutotambuliwa na Bodi ya Mikopo hivyo kutopata mikopo.
Madebe alisema kuwa licha ya
changamoto mbalimbali lakini watahakikisha wanaendeleza umoja wao ili
kufanikisha malengo ya kuanzishwa shirikisho hilo ambayo ni kuwaunganisha
wasomi walio vyuo kuwa na umoja wao ili kukipigania chama.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment