Na John Gagarini, Kibaha
HOSPITALI ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani inakabiliwa na upungufu
mkubwa wa dawa baada ya kukosa dawa kuanzia Januari mwaka huu kutoka Bohari Kuu
ya Madawa (MSD) kutokana na kudaiwa deni la shilingi milioni 220.
Hayo yamesemwa na mganga mkuu mfawidhi wa Hospitali hiyo
Tumaini Byron wakati Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya
Bagamoyo kutembelea wagonjwa na kuwapa misaada mablimbali katiaka kusherehekea miaka
61 ya kuanzishwa Jumuiya hiyo.
Dk Byron amesema kuwa kutokana na deni hilo Hospitali hiyo
kwa sasa imeonekana haikopesheki kutokana na deni hilo hivyo kunywimwa dawa
hadi pale watakapolipa deni hilo la madawa.
Amesema wanakosa dawa kutokana na deni hilo kwani hata
wakiomba hawapati hivyo kuwapa wakati mgumu wao pamoja na wagonjwa ambao
hutakiwa kwenda kununua kwenye maduka ya madawa.
Aidha amesema kuwa wanashindwa kupewa au kukopeshwa vifaa
tiba pamoja na vipimo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vipimo vya wingi wa damu
mkojo na malaria.
Amebainisha kuwa changamoto nyingine ni upungufu wa watumishi
kwani kwa sasa wana watumishi 147 huku mahitaji yakiwa ni watumishi 250,
vitanda vilivyopo ni 24 tu ambapo walau vingepatika japo 100 pamoja na uchakavu
wa miundombinu ya umeme..
Kwa upande wake Mfamasia wa wilaya ya Bagamoyo Mohamed Makarai
amesema kuwa mbali ya deni hilo la dawa pia MSD kutokuwa na dawa hivyo kuwa ni
tatizo la nchi nzima kuanzia Oktoba na Novemba mwaka jana.
Makarai amesema kuwa serikali ilibadilisha mfumo wa kutoa
tenda kwa wazabuni kwa ajili ya kuwapelekea dawa ambapo kwa sasa utaratibu
umebadilika kwani hakutakuwa na kutoa tenda tena.
Amesema kuwa walikuwa wakichukua dawa kwa mali kauli na kutoa
fedha baadaye hata hivyo walitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 100 ambapo
moja ya changamoto ya kukosa fedha ni pamoja na kuwa na misamaa ikiwemo ya
watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wazee, wajawazito na wale wenye
magonjwa sugu hivyo serikali inapaswa kufidia pengo la makundi hayo ambayo
yanapewa dawa bure.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment