Tuesday, September 12, 2023

WATOTO ZAIDI YA LAKI 4 KUPATA CHANJO YA POLIO MKOA WA SONGWE

Na. WAF - Songwe

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amebainisha kuwa zaidi ya watoto laki Nne wanatarajia kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio katika Mkoa wa Songwe. 

Waziri Ummy ameyasema hayo Septemba 11, 2023 wakati akianza ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ambapo ameanza kutembelea katika Hospitali ya Wilaya hiyo, Zahanati ya Mbala pamoja na Kituo cha Afya Mbuyuni kilichopo katika Wilaya hiyo.

“Baada ya kupatikana kwa mtoto Mmoja mwenye ugonjwa wa Polio tumeamua kutoa chanjo ya ugonjwa huo ambapo kwa Mkoa wa Songwe tunatarajia kuchanja watoto takribani Laki Nne ambao wana umri chini ya Miaka Nane”. Amesema Waziri Ummy 

Amesema, Mwaka 2015 Shirika la Afya Duniani (WHO) iliitangaza Tanzania kuwa ni nchi ambayo imetokomeza ugonjwa Polio, Mwaka huu 2023 Tanzania imepata Mtoto mwenye ugonjwa huo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkaoni Rukwa. 

“Baada ya Miaka 8 toka WHO iitangaze Tanzania kumalizika kwa ugonjwa wa Polio, Mwaka huu 2023 tumepata mtoto mmoja kutoka Mkoa wa Rukwa ambaye ana virusi vya ugonjwa wa Polio (aina ya Pili)”. Amesema Waziri Ummy 

Aidha, Waziri Ummy amesema kutokana na hatari iliyopo, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeamua kuendesha kampeni maalumu ya kutoa chanjo ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Polio. 

Amesisitiza kuwa, chanjo hiyo itatolewa katika Mikoa Sita iliyopo mipakani ambayo ni Mkoa wa Songwe, Kigoma, Rukwa, Katavi, Mbeya pamoja na Kagera. 

“Mikoa Sita itafikiwa na zoezi hili na lengo ni kuwafikia zaidi ya watoto Mil. 3.5 ambao wana umri chini ya Miaka Nane kwa sababu watoto wote waliozaliwa kuanzia Mwaka 2016 walipata chanjo ya Polio ya kukinga kirusi aina ya kwanza”. Amesema Waziri Ummy 

Pia, Waziri Ummy amesema zoezi hilo la utolewaji wa chanjo litaendeshwa kwenye vituo vya kutoa huduma za Afya, mashuleni, nyumba kwa nyumba, sehemu za ibada na vilabuni.

“Wakati wa zoezi hili tutawatumia watu Watatu Watatu katika kila timu ambao watapita kama ni mashambani, mashuleni au masokoni kwa ajili ya kuwapa watoto chanjo hiyo dhidi ya ugonjwa wa Polio ili tuwakinge watoto wetu na ugonjwa huo”. Amesema Waziri Ummy

KIBITI WAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO NYERERE SUPER CUP

Picha ya matukio ya Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani ikiwakirishwa na Ndugu Omary Punzi Katibu wa Taasisi hiyo wakikabidhi Tshirt na Mipira ya zawadi ya mashindano ya NYERERE SUPER CUP 2023 Kwa Mhe Kanali Joseph kolombo Mkuu wa wilaya ya Kibiti Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Tarehe 23.9.2023 na kutamatisha 12.10.2023 yakishirikisha Timu 12 Timu 6 kutoka Kibiti na Timu 6 kutoka Rufiji wadhamini wa mashindano ni NSSf,NBC BANK na  TANGANYIKA ORGANIC Kauli mbiu ya mashindano AMANI NA UMOJA VITAWALE MITANO TENA

Saturday, September 9, 2023

NYERERE SUPER CUP TIMU ZAKABIDHIWA VIFAA

Katika kuelekea kumbukizi ya Miaka 24 ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani ikiwakirishwa na Ndugu Omary Abdull Katibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Pwani Leo Tarehe 9.9.2023 imekabidhi Vifaa vya michezo ya mashindano ya NYERERE SUPER CUP Jezi seti Moja na Mpira Mmoja Kwa Kila Timu, Tshirt za maandalizi ya Ufunguzi, Zawadi za Mashindano na Mpira Kwa Chama Cha Mpira Rufiji Kwa Mkuu wa wilaya ya Rufiji Mhe Meja Edward Gowele ili akabidhi Kwa Timu sita hizo zitakazoshiriki kwa upande wa Rufiji 1. NGORONGO 2.UTETE,3.MGOMBA, 4.MUHORO 5.UMWE na 6.MKONGO yatakayoshirikisha Wilaya Mbili KIBITI na RUFIJI yatanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 23.9.2023 na kutamatika 12.10.2023 Wadhamini wa mashindano hayo NBC bank, NSSF, TANGANYIKA ORGANIC na UNGA AFYA LISHE kauli mbiu ya Mashindano UMOJA NA AMANI VITAWALE MITANO TENA

MTANZANIA ALICE GYUNDA AOMBA APIGIWE KURA MRS/MISS AFRICA UK 2023

MSHIRIKI wa shindano la Miss/Mrs Africa UK 2023 kutoka Tanania Alice Gyunda amesema kuwa endapo atafanikiwa kushinda taji hilo atajenga studio kwenye baadhi ya shule a msingi a Jijini Dar es Salaam ili kuzalisha vipaji vingi vya waimbaji waweze kuitangaa nchi kupitia muziki.

Aidha alisema kuwa ndoto yake nyingine ni kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu hususani wanawake na watoto ili waweze kupata haki zao za msingi ili nao waweze kufikia malengo waliojiwekea katika maisha yao.

Gyunda ambaye ni mwalimu na mwimbaji akizungumza kwa njia ya simu kutokea nchini Uingereza anakoishi alisema kuwa endapo Watanania watampigia kura kwa wingi atakuwa na uwezo wa kushinda kwani hadi sasa bado yuko kwenye nafasi nzuri ya kufanya vema.

“Namewaomba Watanzania wanipigie kura ili nishinde ambapo vigezo ni kuonyesha utashi jinsi unavyo ongea na watu na namna unavyofanya mambo yako uwe mtu mwenye ushawishi na nikiwa mshindi nitakuwa balozi wa Kiswahili duniani na malengo yangu kuacha alama kwenye jamii kwa kusaidia watu wasiojiweza huko nyumbani japo niko mbali,”alisema Gyunda.

Alisema kuwa endapo atashinda atahakikisha anajenga studio kwenye baadhi ya shule za Msingi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wanafunzi ambao wana vipaji lakini hawana uwezo wa kurekodi itakuwa bure bure au kama kutakuwa na malipo yatakuwa ni madogo sana kwani muziki Tanzania uko chini sana licha ya kuwa na vipaji vingi kwani wengi hawawezi kurekodi kutokana na gharama kuwa kubwa.

“Nia ni kuinua muziki ambapo tutawekea kwa wanafunzi na vijana ambao wana vipaji vikubwa lakini kutokana na mazingira magumu ya uwezo wanashindwa kutimiza ndoto zao na wakipatikana vijana wenye vipaji wataenda kwenye matamasha ya American Good Talent au UK Good Talent ambapo vijana wa nchi za Uganda na Kenya huwa wanakwenda kwenye matamasha hayo ambapo atashirikiana na serikali ili nao washiriki wakirudi wawe chachu kwa wengine,”alisema Gyunda.

Aliongeza kuwa aliingia kwenye shindano hilo baada ya kuona tangazo na walipewa maswali 10 kuchujwa ambapo walikuwa 30 wakachujwa tena wakabaki 20 wakachujwa na kubaki 15 na baadaye mchujo mwingine ulifanyika na kubaki 13 ambapo wanatoka nchi za Afrika na Asia na kuwaomba Watanania wampigie kura ambapo hadi wakati anaongea alikuwa ameshapigiwa kura 1,800 kupitia https://africaukpageants.co.uk/poll/mrs-miss-africa-finalist-2023/

Friday, September 8, 2023

WAFANYABIASHARA WATAKA UBORESHWAJI WA HUDUMA SOKONI HAPO

WAFANYABIASHARA wa soko la Uhindini Wilaya ya Chunya wameomba uboreshwaji wa huduma  zikiwemo za miundombinu ya barabara maji na umeme ili waweze kutoa huduma kwa ubora kwa wateja wao.

Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara wa wilaya hiyo wakati wa mkutano wa wafanyabiashara ulioongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Hamis Livembe September 7 wenye lengo la kupokea changamoto kero na maoni ya biashara ili kupatiwa ufumbuzi.

Mmoja wa wafanyabiashara wilayani hapo Qeen Mwasakela  amesema kuwa changamoto ya umeme ina takribani miaka 10 tangu soko hilo kuanzishwa na kuiomba serikali kutatua kero hiyo.

Naye katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Ismail Masoud amewataka wafanyabiashara kueleza changamoto kwa mamlaka husika bila ya kuogopa ili zipatiwe ufumbuzi.

Katika hatua nyingine Masoud amewataka  wafanyabiashara hao kutoungana na baadhi ya maofisa wa mamlaka mbalimbali ambao wanahujumu mipango ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasan ya ukusanyaji wa mapato.

Amesema kuwa wasikubali kudanganywa kuwa watapunguziwa au kufutiwa kodi kwa kutakiwa kutoa rushwa ambapo mamlaka zinazohusika zikifuatilia hujikuta akiwa na deni kubwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Hamis  Livembe amesema kuwa ukosefu wa huduma bora za msingi za kibiashara zinasababisha kushuka kwa biashara na ulipaji kodi kutofanyika vizuri na  atahakikisha changamoto hizo zinafikishwa kwenye mamlaka husika ili kupatiwa ufumbuzi.

WATAKA HATUA ZAIDI KUONGEZA MATUMIZI YA GESI

IMEELEZWA kuwa matumizi ya nishati ya gesi kwa ajili ya kupikia ni asilimia moja tu huku matumizi ya kuni na mkaa ikiwa ni asilimia 98.9 hapa nchini huku ikihitajika hatua za makusudi za kuzuia matumizi hayo ya miti ili kupunguza athari kubwa za kimazingira.

Aidha serikali imeombwa kuweka bei ya juu ya
upatikanaji wa vibali vya ukataji wa miti ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuhamasisha matumizi ya gesi majumbani.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na ofisa Mahusiano wa kampuni ya Taifa Gesi Ambwene Mwakalinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliotembelea eneo la ujazaji wa gesi ya (LPG) kwenye ghala lililopo Kigamboni.

Mwakalinga amesema kuwa matumizi ya kuni na mkaa ni makubwa sana hivyo kuna haja ya serikali kuweka jitihada za makusudi za kukabiliana na hali hiyo ili kusitokee mabadiliko ya Tabianchi ambayo yanasababisha athari ikiwemo ukosefu wa mvua na uharibifu wa mazingira.

Naye meneja wa ghala hilo la Kigamboni Juma Masese amesema kuwa Taifa Gesi ndiyo kampuni ya hifadhi kubwa ya gesi hapa nchini ambayo inamilikiwa na mzawa ambapo kwa sasa inahifadhi ujazo wa metriki tani 7,400 ambapo inatarajia kuwa kampuni ya kwanza Afrika kwa kuwa na hifadhi kubwa ya nishati hiyo ambayo huletwa na meli kutoka nchi zinazozalisha gesi duniani.

Kwa upande wake ofisa usalama wa kampuni hiyo Albert Bungayela amesema kuwa wanatoa elimu kwa mawakala ili nao watoe elimu kwa watumiaji kuwa makini katika matumizi ili kuepuka madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya gesi.