Thursday, September 24, 2026

KIWANDA CHA FORTUNE CHADHIBITI UTIRIRISHAJI MAJI MACHAFU HATARI KWA AFYA ZA WANANCHI

KIWANDA cha Fortune Paper kimedhibiti utiririkaji wa maji machafu na kufukia mabwawa yaliyokuwa yamechimbwa kuhifadhi maji ambayo yalikuwa hatari kwa afya za binadamu.

Kiwanda hicho kilichopo eneo la viwanda Zegereni Halmashauri ya Kibaha kilibainika mwanzoni mwa mwaka huu kuwa kinatiririsha maji ambayo yalikuwa ni hatari kiafya.

Akizungumza na uongozi wa kiwanda hicho baada ya kukitembelea Mstahiki Meya wa Halmashauri Kibaha Dk Nicas Mawazo amesema kuwa serikali inapenda kuona wawekezaji hawasumbuliwi lakini wanapaswa kulinda afya za wananchi.

Mawazo amesema kuwa kwa sasa maji yaliyokuwa yakizalishwa na kiwanda hicho yanatumika kwa matumizi mengine na hayatiririki tena hivyo kuondoa kero kwa wananchi wanaokizunguka kiwanda hichi.

"Nimefurahi kuona wametatua changamoto ya utiririshaji maji machafu kwani tunakoelekea kuna mvua za Elnino na endapo maji hayo yangeendelea kuwepo yangesambaa na kuketa athari za kiafya kwa wananchi lakini kwa kutotiririsha maji machafu hakutakuwa na madhara tena kwa wananchi,"amesema Mawazo.

Kwa upande wake Daudi Tito Mtaalamu wa mazingira wa kiwanda hicho amesema kuwa wametekeleza agizo la kuzuia maji kutiririka na kufukia mabwawa yaliyokuwa yabahifadhi maji hayo machafu pembeni mwa kiwanda hicho.

Tito amesema kuwa watahakikisha hali hiyo haitajirudia tena kwani tayari wameweka mifumo vizuri ili kudhibiti changamoto hiyo kutojirudia tena kiwandani kwao.

Awali mwenyekiti wa Mtaa wa Saeni kilichopo kiwanda hicho Edward Kitale amesema kuwa kulikuwa na mabwawa manne ambayo yalikuwa yanahifadhi maji hayo machafu kutoka kiwandani hapo.

Kitale amesema kuwa kwa sasa hali imekuwa ni nzuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo na kuleta kero kubwa kwa wananchi walioko jirani na kiwanda hicho.

MPANGO UJENZI WA MABWENI SHULE ZA SEKONDARI KUPELEKWA BARAZA LA MADIWANI

KUFUATIA ombi la Shule nyingi za Sekondari za kutwa kuomba kujengewa mabweni kwa ajili ya wanafunzi Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo amesema kuwa atapeleka pendekezo hilo kwenye Baraza la Madiwani ili kuweka mpango huo.

Mawazo ameyasema hayo kwenye Shule ya Sekondari ya kutwa ya Misugusugu wakati wa ziara yake kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu na barabara na viwanda ili kujua changamoto zilizopo kwenye sekta hizo.

Amesema kuwa ametembelea Shule nyingi za Sekondari lakini zote maombi yao makubwa ni kujengewa bweni kwa ajili ya wanafunzi wa Shule hizo.

"Nimekuja hapa Misugusugu na kabla kuja hapa nimetembelea Sekondari nyingi lakini zote hilo ni ombi lao kubwa kwa hiyo kuna haja ya kupeleka maombi haya kwenye Baraza la Madiwani ili liwe azimio,"amesema Mawazo

Aidha amesema kuwa kama hili ndilo hitaji na ni kipaumbele basi mpango uwekwe ili waanze ujenzi wa mabweni kwa Shule kujengewa mabweni kwa ajili ya wanafunzi.

"Kuna baadhi ya Shule kweli zina uhitaji wa mabweni kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo umbali hivyo kuna haja ya kujengwa mabweni mfano hapo jirani na Shule hiyo kuna sehemu ya kulaza malori hali ambayo ni hatari hasa kwa wanafunzi wa kike,"amesema Mawazo.

Naye Diwani wa Viti Maalum Sara Uledi amesema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari Misugusugu wanaishi na mzazi mmoja.

Uledi amesema kuwa wanafunzi wengine wanaishi mbali na Shule hivyo kuwa na changamoto ya umbali kutoka nyumbani hadi Shuleni na kurudi pi

Kwa upande wake Ofisa Elimu Sekondari Theresia Charles amesema kuwa kuna uhitaji wa mabweni kwa baadhi ya Shule kutokana na mazingira ya baadhi ya wanafunzi.

Charles amesema kuwa kuhusu umbali sheria inataka wanafunzi wasitembee umbali wa zaidi ya kilometa saba pia Shule ambazo zina mabweni zinafanya vizuri.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Misugusugu Mohamed Lacha amesema kuwa baadhi ya changamoto ni ukosefu wa mabweni na uzio wa Shule.

Lacha amesema kuwa pia wanahitaji huduma ya maji na umeme ambapo tayari wako kwenye hatua mbalimbali za kupata huduma hizo lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha.

mwisho.


Wednesday, September 23, 2026

HALMASHAURI YA MANISPAA KIBAHA KUBORESHA OFISI ZA WALIMU

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo amesema baada ya Serikali kuboresha miundombinu mbalimbali ya elimu wameanza mpango wa uboreshaji wa ofisi za walimu.

Mawazo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahafali ya tatu ya Shule ya Msingi Kanesa iliyopo Kongowe Kata ya Kongowe Wilayani Kibaha.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Dk Samia Suluhu Hassan imeboresha sekta ya elimu kwa kuweka mazingira mazuri ya usomaji na ufundishaji na miundombinu yakiwemo madarasa, maktaba, mabweni, maabara na miundombinu mingine sasa wameanza kuboresha ofisi za walimu.

"Kuanzia mwakani tutaanza kuboresha ujenzi wa ofisi za walimu ili ziwe za kisasa ambapo kwa sasa baadhi ya shule zina changamoto za ofisi hali inayosababisha wakati mwingine kutumia madarasa kama ofisi au kukaa nje,"amesema Mawazo.

Aidha amewataka walimu wakuu kurasimisha maeneo ya Shule ili yapimwe ili kupunguza migogoro ya ardhi itokanayo na uvamizi unaofanywa na watu wanaoishi jirani na maeneo ya shule.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kanesa Jordan Ngairo amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ni samani za ofisi za walimu ambapo wakati mwingine hutumia madawati ya wanafunzi.

Ngairo amesema kuwa kuhusu majengo hakuna changamoto pia wanahitaji wadau kuwasaidia kuweka uzio na hadi sasa wanatofali 415 kwa ajili hiyo hivyo wanawaomba wadau kujitokeza kuwasaidia kukabili changamoto hiyo.

Kwa upande wake mdau wa maendeleo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Africars Ltd Hafidh Amir amesema kuwa changamoto za samani watazifanyia kazi.

Amir amesema kuwa kuhusu suala la uzio watakaa na kuangalia namna gani watatatua changamoto hiyo kwa kushirikiana na Shule hiyo ili kuunga mkono jitihada za serikali.

Akisoma risala ya wahitimu kwa mgeni rasmi Anuary  Omary amesema kuwa Shule yao imejengwa kupitia mradi wa Boost na ni Shule Jumuishi ikiwa na wanafunzi wenye mahitaji maalum 12.

Omary amesema kuwa Shule hiyo ina kituo cha MEMKWA na changamoto ya uzio inasababisha hatari kwa usalama wa wanafunzi walimu na mali za Shule. Jumla ya wahitimu 129 walipewa vyeti.





Monday, September 21, 2026

PWANI YAWEKA MIKAKATI KUKABILI ELNINO.

MKOA wa Pwani unaendelea kuboresha na kutekeleza mpango wa kukabiliana na athari za Elnino kwa mwaka 2026/2027 kwa kuimarisha uratibu wa shughuli za maafa katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo wakati wa kikao cha mikakati ya uboreshaji na utekelezaji wa mpango wa kukabiliana na athari za Elnino.

Nyongo amesema kuwa mikakati hiyo ikiwemo kuhakikisha bajeti zilizopangwa kwa ajili ya shughulĂ­ za usimamnizi wa maafa zinatumika kwa wakati na kupewa kipaumbele kulingana na mahitaji na matukio yatakayotokea. 

"Makisio ya bajeti jumla ni Sh bilioni 32.6 kwa ajili ya kukabiliana na athari za maandalizi kabla na baada ya athari ya mvua za Elnino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni,"amesema Nyongo.



Wednesday, September 16, 2026

PWANI YATENGA MAENEO KUKABILI CHANGAMOTO ZA MVUA ZA ELNINO

MKUU wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo amesema Wilaya za Mkoa huo zimetenga maeneo kwa ajili ya wananchi watakaokumbwa na changamoto zitakazotokana na mvua za Elnino.

Aidha aliwataka wananchi waishio mabondeni waondoke na kuhamia kwenye maeneo ya miinuko ili kuepuka madhara wakati wa mvua hizo zitakazonyesha hivi karibuni.

Nyongo aliyasema hayo ofisini kwake Mjini Kibaha wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya tahadhari ya ujio wa mvua za Elnino zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni.

Alisema kuwa maeneo yaliyotengwa ni pamoja na shule na maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za kijamii hivyo wananchi wanapaswa kukaa sehemu zisizo hatarishi ili kupunguza madhara ya mvua hizo kwa wananchi kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

"Wananchi waishio mabondeni na sehemu hatarishi wanapaswa kuhama na kuishi sehemu salama wasisubiri hadi madhara yatokee,"alisema Nyongo.

Alibainisha kuwa suala la kutoa tahadhari kwa wananchi linapaswa kufanywa na watu wote wakiwemo viongozi wa dini na viongozi mbalimbali wa jamii.

"Tunapaswa kuwapa elimu wananchi ya kusafisha mazingira kwa kusafisha mitaro na njia za maji sehemu za biashara na kwenye makazi ili kuepusha maji kutuama bali yapate njia,"alisema Nyongo.

Pia aliwataka wananchi kuhifadhi chakula, madawa, tochi, madawa na vifaa mbalimbali kwani yawezekana kukawa na changamoto ya barabara katika kupata mahitaji.

Monday, September 14, 2026

WADAU WA ELIMU WAPONGEZWA UWEKEZAJI

UWEKEZAJI kwenye sekta ya elimu ni moja ya njia zinazoonyesha utayari wa kushirikiana kati ya serikali na sekta binafsi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Robert Shilingi wakati wa kuadhimisha miaka 25 ya Shule ya Msingi Kibaha Independent Pre and Primary School (KIPS).

Shilingi amesema kuwa Dira ya Maendeleo inataka ushirikiano na sekta binafsi kwenye masuala mbalimbali kiwemo kuinua sekta ya elimu ili kuweza kufikia malengo.

"Ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi umetajwa kuwa muhimu katika kuimarisha sekta ya elimu nchini hususani kwa kuongeza fursa za watoto kupata elimu pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia,"amesema Shilingi.

Amesema kuwa serikali inaunga mkono wadau wa elimu wakiwemo wa sekta binafsi kwani wanaisaidia serikali katika utoaji elimu ili kufikia mafanikio kwenye sekta hiyo.

"Katika kutimizi miaka 25 kupitia Makampuni ya Njuweni imewekeza katika Shule tatu za Msingi ambazo ni KIPS, KIPS Annex na KIPS Msangani pamoja na Njuweni Institute of Hotel Catering and Tourism Management na Shule tatu za Sekondari ambazo ni Vuchama Ugweno Islamic, Mangio na Pwani Sekondari,"amesema Shilingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makampuni ya Njuweni Alhaj Yusuf Mfinanga amesema kuwa anaishukuru serikali kwa kumpa ushirikiano katika uboreshaji wa elimu kwenye Shule hizo.

Mfinanga amesema kuwa Shule ya Sekondari ya Pwani inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mwaka 2027 hatua ambayo itaongeza fursa za elimu ya Sekondari kwa vijana wa Kibaha Pwani na maeneo mengine.

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi KIPS Salim Nkumbilwa amesema kuwa jumla ya wanafunzi 179 wamehitimu Darasa la Saba kutoka Shule tatu za KIPS, KIPS Annex na KIPS Msangani.

Sunday, September 13, 2026

NYIKA NA BABERIAN KUKIPIGA FAINALI MEETING POINT SUPER CUP 2026

TIMU za soka za Nyika na Baberian zinatarajiwa kuchuana kwenye hatua ya fainali ya kinyanganyiro cha Meeting Point Super Cup baada ya kushinda michezo yao ya hatua ya nusu fainali.

Nyika ilifanikiwa kuifunga Kiduli kwa mikwaju ya penati 4-3 kwenye nusu fainali ya kwanza na Baberian waliifunga Nyumbu kwa mabao 2-0 michezo yote ilifanyika uwanja wa Mwendapole Kibaha.

Mchezo huo wa hatua ya fainali utachezwa kwenye uwanja wa Mwendapole ambapo mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ndiyo utaanza kati ya Kiduli na Nyumbu.


NYIKA NA BABERIAN KUCHUANA FAINALI YA MEETING POINT SUPER CUP

MIAMBA ya soka Mkoa wa Pwani Nyika na Baberian zinatarajiwa kuchuana kwenye hatua ya fainali ya kinyanganyiro cha Meeting Point Super Cup baada ya kushinda michezo yao ya hatua ya nusu fainali.

Nyika ilifanikiwa kuifunga Kiduli kwa mikwaju ya penati 4-3 kwenye nusu fainali ya kwanza na Baberian waliifunga Nyumbu kwa mabao 2-0 michezo yote ilifanyika uwanja wa Mwendapole Kibaha.

Mchezo huo wa hatua ya fainali utachezwa kwenye uwanja wa Mwendapole ambapo mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ndiyo utaanza kati ya Kiduli na Nyumbu.

MUHEZA WALILIA RUTI YA DALADALA KWENDA MAILI MOJA

WAKAZI wa Mtaa wa Muheza Kata ya Maili Moja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wameomba kupatiwa ruti ya Daladala kutoka Maili Moja kwenda kwenye Mtaa huo na kupunguza gharama za pikipiki ambazo ni 4,000.

Aidha wamesema usafiri wao mkubwa ni pikipiki na hutumia kiasi cha shilingi 8,000 kwenda na kurudi kufuata mahitaji au kupata huduma za msingi za kila siku.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Maili Moja mwananchi Veronica Christopher alisema kuwa maombi yao ni kupatiwa ruti ili wawe na usafiri wa uhakika.

Christopher alisema kuwa suala la usafiri ni changamoto kubwa kwani hakuna usafiri wa uhakika zaidi ya pikipiki ambapo gharama zake ni kubwa sana na kipindi cha mvua gharama inaongezeka kwani barabara inaharibika sana kutokana na utelezi na tope jingi.

"Kwa sasa maisha ni magumu sana hebu fikiria ili uende kufuata mahitaji au huduma uwe na 8,000 au zaidi kwa kwenda na kurudi na kwenda huko ni lazima kwani ndiko huduma na mahitaji muhimu hupatikana hivyo tukipata ruti ya Daladala itatupunguzia gharama,"alisema Christopher.

Alisema kuwa Maili Moja ndiyo Mjini na kwa wale wanaofanya safari kwenda maeneo mbalimbali lazima wafike Maili Moja ambako ndiko wanakopata mahitaji lakini usafiri gharama ni kubwa sana za kwenda na kurudi.

Akijibu hoja hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo alisema kuwa mpango huo ni mzuri na leo atakutana na wenye viti wa Mitaa iliyoko kwenye Kata ya Maili Moja na LATRA ofisini kwake ili kupanga ruti hiyo.

Mawazo alisema kuwa hoja hiyo ni ya msingi kwani Serikali ina lengo la kuwapunguzia mzigo wananchi kwa kuwatatulia changamoto kama hizo ambazo ziko ndani ya uwezo wa serikali.

Naye Diwani wa Kata ya Maili Moja Ramadhan Lutambi alisema mpango wa kuboresha barabara kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA imetenga shilingi milioni 50 kwa kila Kata ambapo Mtaa huo wenye wakazi 12,000 na Mtaa wa Maili Moja wenye wakazi 4,000 watanufaika.

Lutambi alisema kuwa fedha hizo zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka 2026/2027 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara ikiwemo madaraja na makalavati.

Alisema kuwa baadhi ya maeneo mvua ikinyesha kwenye vivuko hakupitiki kutokana na maji kujaa ambapo kipaumbele kitawekwa kwenye maeneo ya Mkwanda Machokodo Makanyaga na Kwakamese kutawekwa Makalavati.

Saturday, September 12, 2026

NYIKA FC YAINGIA FAINALI MICHUANO MEETING POINT SUPER CUP

TIMU ya soka ya Nyika Fc imeifunga Kiduli Fc kwa penati 4-3 kwenye michuano ya Meeting Point Super Cup kwenye uwanja wa Mwendapole Kibaha. 

Timu hizo ziliingia kwenye hatua ya penati baada ya kufungana goli 1-1 hadi dakika 90 zilipotamatika kwenye mchezo huo.

Kutokana na matukio hayo Nyika imeingia hatua ya fainali ikisubiri mchezo kati ya Nyumbu na Baberian mchezo utakaopigwa kwenye uwanja huo huo wa Mwendapole.

DIWANI LUTAMBI AWATAKA WANANCHI KURASIMISHA ARDHI WAMILIKI KISHERIA

WANANCHI wa Mtaa wa Muheza Kata ya Maili Moja wametakiwa kuchangamkia fursa ya urasimishaji ardhi baada ya serikali kupunguza gharama kutoka 150,000 hadi 130,000.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa huo Diwani wa Kata ya hiyo Ramadhan Lutambi alisema kuwa hiyo ni fursa kwa wananchi kuelekea kupata umiliki wa ardhi kisheria.

Lutambi alisema kuwa kumiliki ardhi kisheria kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuepukana na migogoro ya ardhi ambaye imeleta changamoto kubwa kwa wananchi.

"Tunaishukuru Serikali kwa kupunguza gharama za urasimishaji ardhi hivyo kuwafanya wananchi kumiliki ardhi kisheria hivyo kuwa na umiliki halali na kupunguza migogoro,"alisema Lutambi.

Akizungumzia suala la changamoto ya maji alisema kuwa kuna mradi wa maji ambao kwa sasa uko kwenye utekelezaji ambapo mitaa yote itapitiwa ambapo kwenye mtaa huo watu zaidi ya 8,000 hawapati huduma hiyo.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo alisema kuwa mikopo ya asilimia 10 ipo kwa makundi wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Mawazo alisema kuwa fedha zimetengwa jambo kubwa ni walengwa kuunda vikundi ambavyo vitatimiza masharti ikiwa ni pamoja na usajili huku kwa watu wenye ulemavu hata kwa mtu mmoja anaruhusiwa.

Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John alisema kuwa mradi wa maji wa Pangani utaondoa changamoto ya maji kwenye mtaa huo hivyo wananchi wawe na subira.

John alisema kuwa Serikali imekuwa ikipambana kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto hiyo ambayo imekuwa kero kubwa lakini inakwenda kupatiwa suluhu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dk Rogers Shemwelekwa alisema kuwa mipango iliyopo ni ujenzi wa Shule ya Sekondari na Zahanati.

Shemwelekwa alisema kuwa kuhusu urasimishaji vifaa vimenunuliwa kwa ajili ya urasimishaji hivyo wananchi wajiandae na watazichukua changamoto zilizotolewa na wananchi ili wazipatie ufumbuzi.

Wednesday, September 9, 2026

ULEGA ATAKA MIUNDOMBINU ITOE HUDUMA KIPINDI CHA MVUA ZA ELNINO.

WAZIRI wa Ujenzi Abdala Ulega ametaka hatua za haraka kuchukuliwa ili miundombinu ya barabara iendelea kutoa huduma hata wakati wa mvua kubwa za Elnino zinazotarajiwa kuanza kunyesha hivi karibuni kote nchini.

Ulega ametoa maelekezo hayo akiwa mkoani Pwani katika ziara yake aliyoianza ya ukaguzi wa maandalizi ya kimiundombinu kufuatia maelekezo ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa watendaji wa Serikali kuhakikisha nchi inakingwa na athari za mvua zinazoweza kujitokeza wakati huo.

Amesema kuwa inapaswa kufanyika kwa ukaguzi wa barabara na madaraja kote nchini kama sehemu ya maandalizi dhidi ya mvua kubwa za Elnino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Aidha amesema kuwa ukaguzi huo ndiyo utakuwa msingi wa kufahamu ni wapi na wapi panahitaji kufanyiwa kazi ili mvua hizo zisiathiri mzunguko wa watu na biashara.

"Naagiza Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kuhakikisha barabara na madaraja yote nchini yanakaguliwa na hatua za haraka kuchukuliwa ili miundombinu hiyo iendelea kutoa huduma hata wakati wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini",amesema Ulega.

Amesisitiza kuwa pamoja na uwepo wa vifaa ³na mitambo utayari wa wataalam na watendaji ndio msingi wa kuhakikisha nchi inapita salama katika kipindi cha mvua hizo.

"Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na TANROADS kufanya tathmini ya kila wiki katika mikoa yote nchini ili kubaini maeneo yoyote yanayohitaji kuongezewa nguvu kwa wakati ili kuhakikisha huduma za dharura zinafika kila kona ya nchi,"amesema Ulega.

Aliingeza kuwa TANROADS mejipanga katika kanda mbalimbali na Mkoa wa Pwani ndiyo kitovu cha kanda zote kwa ajili maandalizi ya tahadhari ya mvua za Elnino.

Pia alikagua pia vifaa mbalimbali vitakavyotumika kufanya matengenezo ya dharura katika miundombinu ya barabara na madaraja nchini
kote.

Meneja wa TANROADS Mkoa waPwani Mhandisi Joel Mwambungu amesema kuwa wamejipanga kukabiliana na athari za mvua hizo kwa ununuzi na usambazaji wa vifaa vya dharura katika maeneo mbalimbali nchini.

Mwambungu amesema kuwa TANROADS tayari ina kalavati za chuma zenye jumla ya urefu wa mita 5,638 zitakazotumika katika maeneo ambayo barabara au madaraja yanaweza kupata athari kutokana na mvua hizo.

mwisho.

Tuesday, September 8, 2026

MEYA DK NICAS MAWAZO AKABIDHI PHOTOCOPY MACHINE KWA SEKONDARI YA MWAMBISI




MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo amekabidhi mashine ya kudurusu karatasi kwa Shule ya Sekondari Mwambisi na kusema kuwa itapunguza gharama za uandaaji mitihani.

Mawazo alikabidhi mashine kwa uongozi wa shule hiyo kwa kushuhudiwa na Ofisa elimu Sekondari, bodi za Shule za Sekondari za Manispaa, baadhi ya wazazi na wanafunzi wa Shule hiyo.

Amesema kuwa Serika inaendelea kuwaka mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu na kupunguza changamoto za Shule ndani ya Manispaa.

"Utoaji wa mashine hii ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa elimu kwani amejitahidi kujenga miundombinu ya elimu,"amesema Mawazo.

Aidha amesema kuwa miaka ya nyuma Shule zilijengwa na wananchi lakini kwa miaka ya sasa Serikali imejenga miundombinu mingi ya elimu hivyo wadau nao waunge mkono serikali.

"Kuhusu bweni wenyeviti wa bodi za Shule zielezee kwenye mipango yao juu ya mahitaji hayo na kama yapo tutaongea na wadau ili kushirikiana na serikali kuyajenga kama kuna mahitaji hayo,"amesema Mawazo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yahaya Mtonda amesema kuwa kuna haja ya kuipandisha hadhi Shule hiyo ili iwe na kidato cha tano.

Mtonda amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wanashindwa kwenda kusoma mbali pale wanapofaulu kutoka Shule za Msingi kwenye Manispaa ya Kibaha.

RC PWANI KUENDELEZA AGENDA YA UWEKEZAJI NA KUWAJENGA VIJANA KIUCHUMI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, amesema ataendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili kukuza uwekezaji na uchumi wa Mkoa wa Pwani, huku akisisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana kiuchumi.

Mhe. Nyongo amesema hayo leo, Septemba 8, 2026, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Abubakar Mussa Kunenge, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Amesema Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa maeneo muhimu kwa uwekezaji nchini na kwamba atashirikiana na viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa rafiki kwa wawekezaji.

“Mkoa huu ni wa uwekezaji. Nimezunguka maeneo mbalimbali kutafuta wawekezaji, kwa hiyo niwakaribishe kwa kuweka mazingira wezeshi,” amesema Mhe. Nyongo.

Aidha, Mhe. Nyongo ameomba ushirikiano wa jamii katika kuwajenga na kuwawezesha vijana kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yanayolenga kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla.

Amesema atashirikiana na viongozi wa Mkoa katika kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, mifugo, uchumi wa buluu pamoja na sekta nyingine za uzalishaji.

“Ninaamini utendaji wetu wa pamoja utatumika kikamilifu katika kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kutatua changamoto zao mbalimbali, pamoja na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mhe. Nyongo ameomba viongozi na wananchi kutumia sheria, kanuni na taratibu katika kutatua migogoro ya ardhi, akisisitiza umuhimu wa kutumia busara na haki ili kupata suluhisho la kudumu.

Ameahidi kulisimamia kwa karibu suala hilo kwa lengo la kuhakikisha migogoro ya ardhi inapungua na wananchi wanapata haki na fursa ya kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.

KONEKTI NA WAZIRI


Serikali inaendesha programu maalumu kwa vijana waliojikita kwenye kilimo.

Fursa hizi ziko kwenye mnyororo mzima wa Kilimo.

Kuanzia uzalishaji wa mbegu, mikopo ya vifaa vya kilimo...

Pembejeo za kilimo, kuongeza thamani mazao...

Usafirishaji mazao, uhifadhi mazao...

Karibu upate nafasi ya kupata taarifa kuhusu programu hizi pamoja na namna ya kupata mikopo ya masharti nafuu kwenye sekta ya kilimo.

Ili uweze kuzitumia ipasavyo fursa hizi zilizoandaliwa kwa ajili yako.

Kipindi ni kesho saa 11 jioni LIVE Instagram, Facebook na YouTube: @ Joel Nanauka & Waziri Wa Vijana.

Kama utahudhuria comment neno "NDIO".

Saturday, September 5, 2026

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU MKOA WA PWANI ALHAJ MUSSA MANSOUR AJITOLEA KUJENGA OFISI YA CCM KATA YA MKUZA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Mussa Mansour ametoa vifaa vya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mkuza Wilaya ya Kibaha Mjini.

Akizindua ujenzi wa ofisi hiyo na kuhudhuria Mkutano Maalum wa Kata hiyo Mansour amesema kuwa alipewa ombi na Kata hiyo ambayo inatumia ofisi za tawi kwa ajili ya shughuli zake.

Mansour amesema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo vya ujenzi ni kufanikisha Kata hiyo kuwa na ofisi ili kuwa na ofisi badala ya kutegemea ofisi ambazo siyo zao.

"Nimejitolea ili kuimarisha chama na ningetamani uchaguzi wa ndani ya chama mwakani ufanyike kwenye ofisi hizo kikubwa ni uongozi kufuata taratibu ili tuweze kufikia lengo la kuzikamilisha,"amesema Mansour.

Amesema kuwa aliahidi mchanga, simenti, kokoto nondo na matofali anashukuru kwani vyote amevitoa kilichobaki ni ujenzi tu kuanza na uzinduzi uliifanyika ndiyo ishara ya kazi kuanza.

Naye Mwenyekiti wa Kata ya Mkuza Matata Ngollo amesema kuwa wanamshukuru Mjumbe huyo wa Halmashauri ya Mkoa kwa kujitoa kwake kusaidia ujenzi huo.

Ngollo amesema kuwa wanamshukuru kwani vifaa hivyo vitafanya ujenzi kwa asilimia 80 na itabaki umaliziaji tu hivyo kuifanya Kata nayo kumiliki ofisi yake.

Mjumbe huyo alikuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Maalum wa Kata ambapo alizungumza na viongozi mbalimbali wa ngazi za matawi, alizindua tawi la CCM la waendesha bodaboda tawi la Barckyard, alitembelea kijiwe cha draft na kutoa fedha kwa makundi maalum wakiwemo wajane, wazee, bodaboda  na watu wenye ulemavu na vijana na alitembelea soko la Mkuza.

Wednesday, September 2, 2026

WAMACHINGA WAISHUKURU SERIKALI KUWATENGEA ENEO LA BIASHARA

WAFANYABIASHARA wadogo Mkoani Pwani maarufu kama Wamachinga wameishukuru serikali kwa kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya kufanyabiashara.

Hayo yemesemwa Mjini Kibaha na Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoani humo Filemon Maliga alipokuwa akizungumzia kuhusu zoezi la kusajili wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwenye eneo la hifadhi ya barabara eneo la Maili Moja.

Maliga amesema kuwa wafanyabiashara hao wametengewa eneo lingine kwa ajili ya kufanya biashara mara utaratibu wa eneo jipya utakapokamilika watahamishiwa hapo ili kuendelea na biashara zao.

"Kama unavyoona zoezi linaloendelea na kuwasajili kutegemeana na biashara wanazofanya wakiwemo wauza mitumba, mama lishe, wauza matunda, chips na biashara nyingine,"amesema Maliga.

Amesema kuwa kutokana na uhaba wa ajira watu wengi wameingia kwenye mfumo wa kujiajiri kwa kufanya biashara hivyo hiyo ni ajira kwa kundi hilo kwani watu wanaendesha maisha yao kupitia biashara zao.

"Tunamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutaka wafanyabiashara wadogo nao watengewe mazingira mazuri kwa ajili ya kufanya biashara zao wakiwa kwenye mazingira rafiki hivyo kufanya biashara zao kwa uhuru,"amesema Maliga.

Aidha amesema kuwa kupitia biashara hizo wafanyabiashara hao wanaendesha maisha yao kw kujenga nyumba kusomesha watoto na kuongeza kipato na kujiletea maendeleo.

Naye moja ya wafanyabiashara wa eneo hilo Wilielmina Lazaro amesema kuwa mpango huo ni mzuri kwani walikuwa hawana eneo maalum na hapo walikuwa wakifanya kwenye eneo la hifadhi ya barabara ambapo maandalizi ya ujenzi yataanza wakati wowote. 

Lazaro amesema kuwa wanatunza familia zao pia baadhi wanakopa fedha kupitia biashara zao hivyo kuweza kukuza biashara na kujiletea maendeleo wao na familia zao.

RAIS DK SAMIA SULUHU HASSAN AMWAPISHA NYONGO KUWA MKUU WA MKOA WA PWANI

Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha Stanslaus Haroon Nyongo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwenye hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo tarehe 02 Septemba, 2026.


MPANGO WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NINO

Nimeongoza Kikao cha Kamati ya Wataalam Wilaya ya Gairo kupokea taarifa ya Taasisi na Idara mbalimbali namna tulivyojiandaa na kukabiliana na Mvua za El Nino  Kabla ya Mvua, Wakati wa Mvua na Baada ya Mvua.

KIKAO hiki MUHIMU kimehusisha Taasisi za TARURA, RUWASA, GAUWASA, TANESCO, JESHI LA UOKOAJI ZIMAMOTO, JESHI LA POLICE, Udhibiti Ubora wa Elimu na Idara zote zilizopo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.  

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE.

Monday, August 24, 2026

MJUMBE HALMASHAURI KUU CCM MKOA WA PWANI KUSAIDIA UKAMILISHAJI OFISI UVCCM KATA YA TANGINI

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCMNEC) Mkoa wa Pwani Alhaji Hussein Chuma ameahidi kufanikisha umaliziaji wa ofisi ya Umoja wa Vijana wa (UVCCM) Kata ya Tangini Wilayani Kibaha.

Akifungua Kikao cha Baraza la Umoja huo lililofanyika kwenye Kata hiyo mwakilishi wa Mjumbe huyo Nassoro Shomvi amesema mchango wake ni kwa ajili ya kuhakikisha ofisi hiyo inaanza kutumika.

 Shomvi amesema kuwa UVCCM ni tanuru la kupika vijana ambao ni viongozi wa baadaye wa chama hivyo lazima wawekewe mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zao za kila siku.

"Vijana mnapaswa kukitumikia chama ili kiweze kuhudumia wananchi kwani nyie ndiyo nguvu ya chama na chachu ya jumuiya zote za chama hivyo lazima mpambanie chama wakati wote,"amesema Shomvi.

Kwa upande wake Katibu wa UVCCM Kata ya Tangini Lazaro Benjamin amesema kuwa ili kukamilika ofisi hiyo inahitaji baadhi ya vitu ili kukamilika.

Benjamin amesema mojawapo ni samani za ofisi pamoja na kumalizia vitu vidogo vilivyobakia ili iweze kuanza kutumika pia ukosefu wa mashine kwa ajili ya mradi wa uoshaji wa magari.