Monday, July 27, 2026

ZAHANATI YA KILIMAHEWA YAWAPUNGUZIA UMBALI WANANCHI KUPATA HUDUMA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Fadhili Maganya amepongeza ujenzi wa Zahanati ya Kilimahewa Kata ya Tangini Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kuitaka kuweka dirisha la Wazee ili waweze kupata huduma kwa urahisi wakati wa kupata matibabu.

Maganya ameysema hayo Mjini Kibaha alipotembelea Zahanati hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mkoa wa Pwani kuimarisha uhai wa chama na kutembelea miradi ya maendeleo na kusema kuwa ujenzi huo ni wa mapato ya ndani.

Amesema kuwa wazee waliambiwa kuwa watatengewa dirisha kwa ajili ya kuwapatia huduma hivyo ni vema dirisha hilo likawepo kwa ajili ya kuwahudumia na siyo kusema kuwa wapishwe ili wahudumiwa bali wawe na dirisha lao maalum.

"Tuliahidi kuwa tutawawekea dirisha lao maalum kwa ajili ya kupata huduma hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha lazima ihakikishe inawawekea dirisha lao ili wapate huduma za afya kwani wao lazima wahudumiwe vizuri pasipokuwa na changamoto,"amesema Maganya. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Saguti alisema kuwa lengo ni kurahisha upatikanaji wa huduma za afya kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na ulianzishwa kutokana ongezeko la mahitaji ya huduma za afya kwenye eneo hilo.

Saguti amesema kuwa ujenzi ulianza Juni 2024 Halamshauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 233.5 na wananchi walichangia kiasi cha shilingi milioni 1 na shilingi milioni 50 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba hivyo kufanya gharama za mradi kuwa shilingi milioni 284.6.

Amesema kuwa serikali imeajiri wauguzi 32 ambapo Zahanati hiyo ina watumishi saba wanaotoa huduma na Zahanati hiyo imepatiwa watumishi wawili hivyo hakuna upungufu wa watumishi.

Zahanati ilianza kutoa huduma Aprili 2026 na hadi sasa imeshatoa huduma kwa watu 1,103 na inatoa huduma mbalimbali.


No comments:

Post a Comment